Tafuta

shambulizi jijini Vienna shambulizi jijini Vienna 

Papa atuma salam za rambi rambi kufuatia shambulizi la Vienna:vurugu na chuki viishe!

Katika ujumbe wake kwenye telegram uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin,Katibu wa Vatican,Papa anaonesha masikitiko yake kuhusu mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea huko Vienna nchini Austria,anawaombea wathirika na familia zao na kuwakabidhi roho za marehemu katika huruma ya Mungu,pia anaomba uhamasishwaji wa kuishi kwa amani katika jamii.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma salam zake rambi rambi  kwa Kardinali Schönborn Askofu Mkuu Vienna kufuatia na shambulizi la kigaidi lilitotokea tarehe 2 Novemba 2020, Papa katika ujumbe wake, uliotiwa  saini na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican amesema kushutushwa  kwa kina na taarifa za matendo ya kutumia  nguvu huko Vienna na ambayo yamesababisha mauti na uchungu kwa watu wasio na hatia. Papa analezea kuungana na uchungu na familia za waathiriwa na watu wote wa Austria na kwa maana hiyo yuko karibu na waliojeruhiwa na anasali kwa ajili ya uponywaji wao. Aidha Papa Francisko anawakabidhi roho za marehemu waathiriwa katika huruma ya Mwenyezi Mungu na anamuomba Bwana aweze kumaliza vurugu hizi na chuki ili kuweza kuhamasisha amani ya kuishi katika jamii. Kwa moyo wote Papa anawasindikiza wote waliokumbwa na mkasa huo kwa Baraka yake.

Ni upendo peke yake unazima chuki

Papa Francisko ameonesha uchungu wake hata katika Tweet @Pontifex: “Ninauchungu na kwikwi, kutokana na shambulizi la kigaidi huko Vienna na ninasali kwa ajili ya wathirika na familia zao. Inatosha vurugu! Tujenge pamoja amani na udugu. Ni upendo peke yake unashinda chuki! ameandika Papa.

Shambulizi la kigaidi kusababisha vifo 6

Shambuzli lilitotokea tarehe 2 Novemba usiku huko Vienna limesababisha vifo vya watu sita na miongoni mwao hata mshambuliaji. Na kuongezeka baadaye majeruhi 22 ambao kwa sasa wamelazwa katika mahospitali ya Vienna. Watu sita wako hali mbaya amesema hayo Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Austria, Karl Nehammer, na kuongeza kusema kwamba  hatua za uchunguzi zinaendelea. Hata hivyo pia Wizara ya Mambo ya ndani wamethibitisha  kuwa watu 14 wamewekwa mbaloni kwa muda. Polisi wa Austria wamejaribu,katika masaa haya, kujenga upya kuhusu mienendo ya shambulio hilo, wakitazama kwa njia ya video zaidi ya elfu ishirini ambazo zilionekana kwenye vyombo vya kijamii tangu jana usiku. Watu wanne wanafikiriwa kuhusika na hivyo  Serikali imesisitiza asubuhi ya leo mwaliko kwa Watu wa Vienna wasiondoke nyumbani kwao na wasiende katikati ya jiji, ambapo wanajeshi 75 wanalinda maeneo nyeti.

03 November 2020, 16:22