Tafuta

2020.11.20 Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa PIO ya Amerika ya Kusini. 2020.11.20 Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa PIO ya Amerika ya Kusini. 

Papa atoa mwaliko wa kufungua moyo na mioyo&kuponya ulimwengu uliougua!

Papa Francisko ametoa hotuba yake kwa Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa Pio ya Amerika ya Kusini Roma kwa kupendekeza mambo matatu muhimu kwao:kufungua mlango wa moyo na mioyo ya wengine.Pili kutoa msaada na kuwaalika wengine wafanye hivyo.Tatu kuponya ulimwengu dhidi ya ubaya mkubwa unaosumbua.Janga hili linajiwakilisha kwa ubaya mkubwa ambao unasumbua jamii nzima.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametoa hotuba yake kwa Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa ya Pio ya Amerika ya Kusini Roma kwa kushukuru Padre Gilberto Freire, S.J kwa maneno yake kwa niaba ya wote. Katika hotuba yake mkuu wa taasisi hiyo ameonesha changamoto za wakati huu ambazo zimewakumba katika jumuiya yao kwenye uwanja wa mafunzo na ulazima wa kubaki waaminifu katika utume wao kwa kuunda na kuundwa kama makuhani katika huduma ya Watu watakatifu wa Mungu ambao ni wanahija katika Bara la Amerika ya Kusini. Pamoja na kuwa na historia kutengenisha watu wao, lakini haikuharibu ndani mwao ili mzizi ambayo inawaungaha ya kazi ya unjilishaji wa Bara la Amerika. Kwa misingi hiyo, taasisi ya Kipapa ya Amerika ya Kusini ilianzishwa kwa lengo la kuunganisha  makanisa yote mahalia na wakati huo huo kujifungulia katika ulimwengu mzima ambao ni katika mji wa Roma, amesisitiza Papa.

Kuchangia kuponesha ulimwengu

Ni uzoefu wa umoja na ufunguo ambao ndiyo changamoto kubwa kwa sababu iliwezea kuifanya Amerika yenye jumuiya kubwa ya watu  ambayo pia inaweza kuchangia  kuponesha ulimwengu. Injili na ujumbe wake ulipofika katika bara hilo kwa njia ya zana za binadamu, hapakukosekana hata dhambi, lakini kwa neema iliwezeka kupita udhaifu hu na Neno likaendelea kila kona ya Bara amesema Papa.Watu na tamaduni walipokea katika utajiri tofauti  na mitindo mbali mbali ambayo hata leo hii inawezekana kuona. Miujiza hiyo iliwezekana kwa sababu wawe waliofuka n na wale waliokuwa wanapokea waliweza kuwa na uwezo wa kufungua mioyo yao na siyo kuifunga na kuweza kutoa kwa ngazi ya binadamu, utamaduni au dini. Papa Francisko amewaalika katika kipindi hiki ili kupanda  Neno kwa namna ya ukaribu, bila shutumu. Kama anavyopanda Mungu na ambaye hatazami ugumu wa ardhi, wala uwepo wa mawe, na ambaye haondoi mizizi ya magugu mabaya ili asije kung’oa mbegu ya ufalme wa Mungu. Katika hayo Papa anasema lazima ndiyo yaongoze mafundisho yao na katika huduma yao ili kufungulia milango ya mioyo yao na mioyo ya wale ambao wanawasilikiza, kwa utoa msaada na kuwaalika wengine wafanye na wao wema kwa ajili ya wengine. Waponye katika ulimwengu huu wa ubaya ambao unaleta mgogoro na ambao janga limeweza kuweka wazi.

Mambo matatu msingi yakamilishane kibinafsi na kijumuiya

Kwa maana hiyo Papa Francisko amesema ni mambo matatu muhimu ya dhati katika matendo na mbayo yana mambo mawili binafsi na ya kijumuiya ambayo lazima yakamilishane. Mambo hayo Matatu Papa amesema, kwanza kufungua mlango wa moyo na wa mioyo. Hii ina maana ya kufungua moyo kwa Bwana ambaye hachoki daima kubisha hodi mbele ya milango yetu ili aweze kuishi nasi. Lakini pia hata kumfungulia ndugu, kwa sababu ya kutosahau kuwa uhusiano na Mungu unaweza kuwa rahisi ikiwa unaangazia ushusiano na jirani. Pili kutoa msaada na kuwaalika wengine wafanye hivyo. Mungu amewaita katika wito wa kikuhani, na kuwatuma katika mji wa Roma ili kukamilisha mafunzo kwa sababu ana mpango wake wa upendo na huduma kwa kila mmoja. Wachungaji kwa mujibu wa moyo wake wanajikita katika huduma ya kuchunga kundoo, wavue samaki, waongoze na watafute daima ustawi wao. Tatu kuponya ulimwengu dhidi ya ubaya mkubwa unaosumbua. Janga hili limejiwakilisha  kwa ubaya mkubwa sana ambao unasumbua jamii yetu anasema Papa. Utandawazi umeshinda mipaka, lakini siyo katika akili na mioyo. Virusi vinasambaratika bila kuwa na breki, hatuna uwezo wa kutoa jibu zaidi. Ulimwengu unaendelea kufunga milango, kwa kukataa mazungumzo na ushirikiano, unakataa kujifungua katika uwazi zile  jitihda za pamoja kwa ajili ya wema ambao unafikia kila mmoja, Papa amebainisha na kuwatuma.

Kutibu ubaya lazima kuanzia chini ndani ya mioyo

Kutibu ubaya huo lazima uanzie chini, Papa Francisko anaonesha njia kwani amesema  katika mioyo na katika roho ambazo siku moja watakabidhiwa,ili kuwa na mapendekezo ya dhati katika muktakadha wa elimu, katekesi, jitihada za kijamii, uwezo wa kubadili kasumba na kufungua nafasi, kutibu mabaya kumrudishia Mungu watu wake walioungana. Amehitimisha kwa kuwakabidhi kwa Bikira Maria wa Guadalupe, Msimamizi wa Bara la Amerika ya Kusini  ili awasaidie katika matumaini yao, katika nyakati hizi ambazo zinafunguliwa katikati ya ukosefu wa uhakika wa kibinadamu ili waweze kweli kufanana na wito wa Mungu, mahali ambapo watatumwa kuwa mashuhuda wa udugu kibinadamu unaozaliwa na kuwa  watoto wa Mungu. Bwana awalinde!

20 November 2020, 16:14