Tafuta

KITUO CHA AFYA KWA AJILI YA COVID-19 KIMEUNGUA NCHINI ROMANIA KITUO CHA AFYA KWA AJILI YA COVID-19 KIMEUNGUA NCHINI ROMANIA 

Papa aonesha ukaribu wa sala kwa waathirika nchini Romania kutokana na moto

Tarehe 14 Novemba mchana Kituo cha afya katika kitengo cha wagonjwa mahututi wa Covid-19 huko Piatra Neamt,kaskazini Romania,kimeungua moto na kusababisha waathirika.Papa Francisko amewakumbuka kwa sala wale waliopoteza maisha yao na kuwaalika wote kusali kwa ajili yao.

Na Sr. Anggela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, katika Siku ya Maskini duniani amewaalika waamini watambue kuwa siku hiyo ni kwa ajili ya wote na wakati huo huo amekumbusha tukio la moto nchini Romania. 

“Jana, katika hospitali huko Romania, ambapo wagonjwa mbali mbali waliolazwa kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya corona moto ulizuka na ambao ukasababisha waathirika wengi. Ninaonesha ukaribu wangu na kuwaombea na tuwaombee”.

Huo ndiyo ulikuwa mwaliko ambao ameutoa kwa kile kilichotokea Kaskazini mashariki mwa nchi ya Romania. Labda ilikuwa mzunguko mfupi wa umeme ingawa uchunguzi bado haujathibitisha, lakini athari imekuwa mbaya. Katika kitengo cha wagonjwa mahututi wa Covid -19 wa hospitali ya Piatra Neamt karibu kilomita 353 kaskazini mwa mji mkuu Bucharest, watu kumi walifariki na wengine saba kuunguzwa moto sana. Miongoni mwao kati ya wahudumu wa afya ni daktari anayesimamia wodi ambaye anaonesha kuungua mwili wake kwa silimia 80. Mamlaka imeripoti ikionyesha kwamba katika huduma zote za wagonjwa mahututi zilikuwa zinaendelea kuwapokea, wakati  moto ulipozuka, na wagonjwa 16 walikuwa wanahitaji kupewa hewa ya Oksijeni kwa ajili ya mapafu. Moto ulizuka karibu saa 6:30 jioni Jumamosi tarehe 14 Novemba 2020, saa za eneo hilo. Katika kitengo cha Covid kwenye kituo hicho, iliwachukua wazima moto zaidi ya saa moja kuudhibiti moto huo.

15 November 2020, 14:34