Tafuta

ETHIOPIA:Migogoro ETHIOPIA:Migogoro  

Papa anasali kwa ajili ya Ethiopia:vurugu ziishe na maisha yalindwe!

Kwa mujibu wa uthibitisho wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican ametoa taarifa kuhusu wito wa nguvu uliotlewa na Papa kuhusu usitishwaji wa migogoro ambayo inazidisha umwagaji wa damu Kaskazini mwa Ethiopia na mamia ya waathirika na uwepo wa maelfu ya wakimbizi wa mgogoro huo.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Papa Francisko anafuatia habari kutoka Ethiopia, ambapo mapigano ya kijeshi yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa na kuathiri Mkoa wa Tigray na maeneo ya karibu. Kama matokeo ya vurugu hizo, mamia ya raia wamekufa na makumi ya maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao kwenda Sudan. Wakati wa sala ya Malaika wa Bwana tarehe 8 Novemba kutokana na tukio hilo la migogoro inayoendelea alikuwa amesema “Wakati ninawashauri kukataa vishwaishi vya mapigano ya silaha, ninawaalika kila mtu katika sala na heshima ya kidugu, katika mazungumzo na suluhisho la   amani dhidi ya mizozo”.

Mapigano hayo ambayo yameongezeka siku hadi siku, tayari yamesababisha hali mbaya ya kibinadamu. Papa Francsiko, katika kuwaalika kuombea nchi hiyo, anatoa rai kwa wahusika wa sehemu zote mbili za mzozo kuacha vurugu hizo, ili kulinda maisha, hasa raia na kurejesha amani kwa watu. Kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu kutokana na Covid-19 kumesababisha mvutano. Aidha kuna kisingizio kulingana na kabila la Tigray ambalo linashtumu serikali ya shirikisho kwa kutotaka kumpa uhuru Tigray.

Sababu ambazo mtaalam anayejihusisha na masuala ya  kiafika Anna Bono amelezea kwa njia ya simu katika studio za Vatican News kwamba, kuna ufichaji wa wa kile ambacho ni mzizi halisi wa mzozo, ambao ni kwamba hadi kufikia  Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, kudhibiti mamlaka kuu ilikuwa hasa ni kikundi cha Tigray. Baadaye ni hatua ya kwanza mnamo Novemba 4 wakati Waziri Mkuu alipoamua kutuma wanajeshi katika mkoa wa waasi akidai kwamba Tplf ilishambulia kituo cha jeshi la shirikishi. Tangu wakati huo eneo lote limetengwa.

Hata hivyo baada ya kukutana na wajumbe maalum wa Umoja wa Afrika (AU), Abiy ametangaza kwamba serikali yake inajaribu kuhakikisha usalama wa raia na mikondo ya kibinadamu na kwamba itawakaribisha wakimbizi wa Ethiopia waliokimbilia Sudan kutokana na uhasama. Walakini, Waziri Abiy amesisitiza kwamba serikali yake itaendeleza mashambulio ambayo sasa, baada ya mwisho wa masaa 72, inajiandaa kuingia katika hatua ya mwisho na shambulio kwa mji mkuu wa mkoa, Makallé. Kulingana na makadirio ya  Umoja wa Mataifa (UN), katika wiki tatu za mzozo tayari kumekuwa na mamia ya vifo na karibu watu 40,000 waliokimbia makazi yao ambapo wamekimbilia Sudan ambayo haina rasilimali ya kuwadhibiti na kuwasaidia. Takwimu ni ngumu kudhibitisha na mawasiliano ya simu yaliyokatwa na uwezekano wa ufikiaji wa mkoa wa kaskazini mpakani na Eritrea imefungwa.

28 November 2020, 11:40