Tafuta

Furaha ya watu katika maisha Furaha ya watu katika maisha 

Papa amemtua Padre François Abeli Muhoya Mutchapa kuwa Askofu wa Kindu

Papa Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Kindu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)Mhesh.Padre François Abeli Muhoya Mutchapa,padre wa Jimbo la Kindu,ambaye hadi uteuzi wake alikuwa katika huduma ya kichungaji ya Parokia ya Mtakatifu Maria na Mtakatifu Mauro Jimbo la Tivoli(Italia).

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Kindu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Mhesh. Padre François Abeli Muhoya Mutchapa, Padre wa Jimbo la Kindu, ambaye hadi uteuzi wakw alikuwa katika huduma ya kichungaji ya Parokia ya Mtakatifu Maria na Mauro Jimbo la Tivoli (Italia). Askofu Mteule François Abeli Muhoya Mutchapa, alizaliwa tarehe 9 Februari 1974  huko Kindu. Baada ya ya shule  ya Msingi alingia seminari ndogo ya Mama yetu wa Mitume huko Kindu (1987-1991), baadaye akaendelea na mafunzo ya malezi huko jimbo la  Kasongo (1991-1992). Tangu 1992 hadi 1995 mafunzo ya falsafa katika seminari kuu ya Monsinyo  Cleire wa Kasongo na 1999 hadi 2000 Taalimungu seminari kuu ya Mtakatifu Pio X huko Murhesa Bukavu.

Alipewa daraja la upadre tarehe 6 Januari 2002 kwa ajili ya jimbo la Kindu. Baada ya upadrisho alijikita katika utume mbalimba wa parorokia na seminari, vituo vya caritas na mjumbe wa masuala ya uchumi wa jimbo 2003 hadi 2013. Aliendelea na  masomo katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana hadi  Udaktari katika Historia na Urithi wa Tamaduni wa Kanisa (2013-2020), wakati huo huo akiwa anatoa huduma yake ya kichungaji katika Jimbo la Tivoli, kama kwenye parokia ya Mtakatifu Maria na Mtakatifu Mauro (2016-2020).

18 November 2020, 17:47