Tafuta

2020.06.20  Maadhimisho ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Makanisa ya Suda Kusini 2020.06.20 Maadhimisho ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Makanisa ya Suda Kusini  

Papa amemteua Padre Matthew Remijio Adam Gbitiku kuwa Askofu wa Wau

Tarehe 18 Novemba 2020 Papa Francisko amemteua askofu wa jimbo la Wau nchini Sudan Kusini Mhs.Padre Matthew Remijio Adam Gbitiku ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni Makamu mkuu na chuo cha kimataifa cha Taalimungu cha Wamisionari wa Kikomboni wa Moyo wa Yesu huko Nairobi,Kenya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amemteua askofu wa jimbo la Wau nchini Sudan Kusini Mhs. sana Padre Matthew Remijio Adam Gbitiku, M.C.C.J., ambaye hadi uteuzi wake alikuwa ni Makamu mkuu na chuo cha kimataifa cha Taalimungu cha Wamisionari wa Kikomboni wa Moyo wa Yesu huko Nairobi, Kenya. Askofu mteule Matthew Remijio Adam Gbitiku, M.C.C.J., alizaliwa tarehe 5 Mei 1972 huko Mboro, jimbo Wau.  Masomo ya katika Seminari ndogo ya Bussere huko Wau (1984-1986). Shule ya Sekondari ya Wengiball (1986-1989) na baadaye alijiunga na Shirika la wamisionari wa Komboni.  Masomo ya Falsafa katika Seminari kuu ya Kanda ya Mtakatifu Paulo huko Khartoum, Sudan (1995-1997) na kumalizia unovisi jijini Kampala, Uganda (1997-1999).Masomo ya Taalimungu katika Taasisi kuu ya Masomo ya Kitaalimungu ya Juan XXIII-ISET, huko  Lima (Peru).  Alipewa daraja la Upadre tarehe 3 Oktoba 2004 kwa ajili ya Wamisionari wa Komboni wa Moyo wa Yesu (M.C.C.J).

Baada ya upadrisho alishika majukumu mbali mbali huko Omdurma (Khartoum), msimamizi wa Kiroho wa Shirika ma Legionari ya Maria, Jimbo Kuu Khartoum na mshauri wa Chama cha Kikundi cha Rongo (2004-2008). Tangu 2008 hadi 2010 masomo ya Taalimungu ya Kiroho, Cho Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma. Mkurugenzi wa Miito ya kikuhani na Mjumeb wa Kikundi cha waamamishaji wa Miito ya Jimbo Kuu katoliki Khartoum (2010-2012); Mkurugenzi wa kiroho katika  seminari Kuu ya Kanda ya Mtakatifu Paulo, huko Khartoum (2012-2013); Makamu wa Jimbo Kuu Khartoum (2013- 2017 na tangu 2017 hadi uteuzi wake alikuwa  Makamu mkuu na chuo cha Kimataifa cha Taalimungu cha Wamisionari wa Kikomboni wa Moyo wa Yesu huko Nairobi, Kenya.

18 November 2020, 17:40