Tafuta

Inahitajika kuwahamasisha watoto wetu na vijana wetu kujifunza kuhusika,kufanya kazi katika vikundi,kuwa na mtazamo wa huruma ambao unakataa utamaduni wa kubagua. Inahitajika kuwahamasisha watoto wetu na vijana wetu kujifunza kuhusika,kufanya kazi katika vikundi,kuwa na mtazamo wa huruma ambao unakataa utamaduni wa kubagua. 

Papa ahimiza Waskolopi kuelimisha mtu na kazi ya uumbaji!

Katika ujumbe wa Papa Francisko kwa shirika lwa Maskini wa Mama wa Mungu wa shule za watawa amesema watawa wako mstari wa mbele katika zoezi la kuelimisha.Anawaalika kupyaisha jitihada kwa shauku za mwanzilishi wa Shirika la Waskolopi kwa ajili ya elimu ya watoto maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa  Mkuu wa Shirika la Maskini wa Mama wa Mungu wajulikanao (Waskolopi) katika fursa ya mkutano wa kimataifa wa wakuu wa mashirika ya kitawa kimataifa na Muungano wa mama wakuu wa Mashirika wanaofanya kwa njia ya mtandao kutokana na janga la corona  kuanzia tarehe 12 hadi 14 Novemba  unaoongozwa na mada ya Changamoto za ujenzi wa mkakati wa Elimu Kimataifa. Papa Francisko anatoa pia salam kwa wahusika wa mashirika mbali mbali ya Maisha ya Kitawa ambao wanashiriki Mkutano huo  na wale ambao wamewezesha kufanikishamkutano huo. Maisha ya kitawa daima yamekuwa mstari wa mbele katika shughuli ya kielimu. Hii inajionesha kwa mfano wa mwanzilishi wa Shirika la Waskolopi  Mtakatifu Yosefu Calasanzio, ambaye alijenga shule za msingi kwa watoto hata kwa watawa ambao walikuwa wanawafundisha huko Estadilla na mapema zaidi nyumba za watawa zilizohifadhiwa na kueneza utamaduni asili. Kutokana na mizizi hiyo ya karama tofauti Papa Francisko amebainisha kwamba zimeibuka katika nyakati zote za kihistoria ambazo, kwa zawadi ya Mungu, zimeweza kutoa mazoezi ya mahitaji na changamoto za kila wakati na kila mahali. Leo  hii Kanisa linatualika tufanye upya azimio hili, kuanzia na utambulisho  wetu  wenyewe, Papa amewashukuru na kwa kuchukua ya ushuhuda huo kwa kujitoa na shauku kubwa.

Katika mkutano wao, Papa  amependa kuwakumbusha jitihada saba msingi wa mkakati wa elimu kimataifa ambao  wao  wanahamasisha. Jitihada saba ambazo amependa kuzifupisha katika mitazamo mitatu ya matendo ya dhati na ambazo ni Kuzingatia, kukarimu na kuhusisha. Akianza kufafanua amesema kuzingatia  kile kilicho cha maana kunamaanisha kumweka mtu huyo katikati, thamani yake, hadhi yake, ili kutoa umaalum wake mwenyewe, uzuri wake, upekee wake na, wakati huo huo, uwezo wake wa kuwa katika uhusiano na wengine na ukweli unaoumzunguka ”. Ili kufanikisha hili, ukarimu unahitajika. Hii ni pendekezo la  kujiwekwa katika usikimu wa mwingine kwa upokeaji wa huduma zetu, watoto na vijana. Hiyo inamaanisha kuwa wazazi, wanafunzi na mamlaka wawe  mawakala wakuu wa elimu,  wawe makini katika kusikiliza aina nyingine ya sauti, ambazo sio tu  kiurahisi za mzunguko wetu wa elimu. Hii itawazuia kujifunga kwa kujilinganisha kwao na itawasababishia kufungua kilio  kwa kila mtu tangu kuumbwa kwake. Kwa maana hiyo inahitajika kuwahamasisha watoto wetu na vijana wetu kujifunza kuhusika, kufanya kazi katika vikundi, kuwa na mtazamo wa huruma ambao unakataa utamaduni wa kubagua.

Jambo la tatu na la mwisho wa hatua ni maamuzi, yaani kushirikisha. Mtazamo wa kusikiliza, uliofafanuliwa katika ahadi hizi zote, hauwezi kueleweka kama kusikia tu na kusahau, lakini lazima iwe jukwaa ambalo linamruhusu kila mtu kushiriki kikamilifu katika kazi hii ya elimu, kila mmoja akiwa na umaalum wake na jukumu lake. Kuhusisha na kujihusishana kunapendekeza  kufanya kazi ili kuwapa watoto na vijana fursa ya kuuona ulimwengu huu ambao tunawaachia kama urithi na jicho la kukosoa, linaloweza kuelewa shida katika uwanja wa uchumi, siasa, ukuaji na maendeleo, na pendekeza suluhisho ambazo kiukweli zinamhudumia mwanadamu na familia nzima ya wanadamu kwa mtazamo wa ikolojia funamani. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amewatakia mkutano mwema akiwasindikiza kwa sala na  juhudi za Taasisi zote zilizowakilishwa katika tukio hilo, na kwa watu wote waliowekwa wakfu na walei wanaofanya kazi katika uwanja wa elimu, akimwaomba Bwana kwamba, kama alivyofanya kila wakati, maisha ya wakfu ni sehemu muhimu ya Mkataba wa kimataifa wa elimu. Amewakabidhi kwa Bwana na kuwaomba Mungu awabariki na Bikira Mtakatifu awalinde.

12 November 2020, 15:56