Tafuta

2020.11.02 Papa akiwa katika mapango ya Vatican kuombea mapapa waliotangulia mbele ya haki 2020.11.02 Papa akiwa katika mapango ya Vatican kuombea mapapa waliotangulia mbele ya haki 

Mons.Fischer:watakatifu wetu wanatuambia kuwa bado tunaishi

Washiriki wa sherehe hii katika Kanisa dogo ni katika muungano na wale wote waliotutangulia na ambao wanalala hapa katika usingizi wa amani,watakatifu wetu jirani ambao hutukumbusha kila siku kwamba tunakunywa wakati wa maisha,bado tunaishi.Katika salamu yake,mwanzoni misa msimamizi wa chuo cha Teutonic,Monsinyo Hans-Peter Fischer, mbele ya Papa Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika salamu yake, mwanzoni mwa maadhimisho ya  misa, msimamizi wa chuo cha Teutonic, Monsinyo Hans-Peter Fischer, mbele ya Papa akimkaribisha amesisitiza kuwa “washiriki wa sherehe hiyo katika Kanisa dogo ni  katika muungano  na wale wote waliotutangulia na ambao wamelala hapo  katika usingizi wa amani  watakatifu wetu, jirani ambao hutukumbusha kila siku kwamba tunapokunywa wakati wa maisha, bado tunaishi”. Msimamizi  huyo amemkumbusha  pia Papa kwamba katika taasisi hiyo  makuhani wageni, ambao ni wasomi wa Sanaa ya Kikristo na historia ya Kanisa, wanatoka katika  tamaduni na watu tofauti”.

Tunakaribisha zawadi ya huruma yake kama baba na rafiki

Sisi sote, ameelezea, “tunazungumza lugha tofauti, tuko wengi lakini hakuna kitu ambacho kimetuzuia kuweza kukutana na kufurahia kuwa pamoja”, kwa sababu “tunajua kuwa kuna Mtu anatufanya kuwa ndugu na dada.  Katika kuelezea furaha na shukrani kwa uwepo wa Papa Francisko, mwanahija kati ya mahujaji, Monsinyo Fisher ameelezea mapenzi ya wote waliokuwapo kuingia kwa kina ndani ya moyo wake na mafundisho yake, wakikaribisha zawadi kuu ya huruma ya baba na rafiki.

Maombi kwa ajili ya uongofu baada ya janga

Katika maombi ya  waamini, wamwomba Bwana kwa ajili ya  Papa, ili tabia  yake, na kwa njia ya Roho Mtakatifu na upendo wa watu wa Kikristo, aendelee  kumsaidia na kumuongoza katika kazi yake ya utakaso wa Kanisa.  Kwa ajili ya wahamiaji, ili maisha yao yaliyokatika, wakikimbia vita, majanga ya asili na mateso, waweze kukaribishwa, walindwe, wanahamasishwe na kuunganishwa kwa sababu wanaweza kujifunza kitu kutoka kwa kila mtu na hakuna mtu asiye na maana.

Kuomba kwa ajili ya  wafu bila uso, sauti, jina

Hatimaye maombi yao yalikuwa ni kwa ajili ya watu wa Mungu, ili wapate  kufanya uzoefu wa Kanisa la kibinadamu na la karibu zaidi, jamuiya yenye mtindo wa familia ambayo inakuwa na juhudi za watu binafsi na familia, ili iweze kuwa uwepo ambao unajua jinsi ya kuunganisha upendo wa ukweli na upendo kwa kila mtu. Na kwa wote waliokufa, bila uso, bila sauti na bila jina, ili Mungu Baba awapokee katika amani ya milele, ambapo hakuna wasiwasi tena na wala maumivu.

Maombi katika makaburi ya Teutonic na kwenye Mapango

Mara baada ya maadhimisho ya Misa hiyo, Papa Francisko, akifuatana na msimamizi huyo Monsinyo Fischer, wamehamia kwenye kaburi dogo la Teutonic na kulibariki kwa kunyunyizi maji matakatifu, baadaye wamejiunda kwenye  maombi mbele ya kaburi na baadaye kuvuka njia zote na kusimama kwa ufupi mbele ya mawe ya kaburi na kaburi ili kufikia njia ya kutoka nje. Hatua chache, Papa ameshuka kwenye Mapango ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro  ambapo amekaa kwa muda wa maombi ya faragha mbele ya makaburi ya Mapapa waliokufa.

Karibu na Mtakatifu Marta,kuna  Kanisa lililoanzishwa katika karne ya nane

Kanisa la Bikira Maria wa Huruma kwenye Makaburi ya Teutonici, ambalo liko mita kadhaa kutoka Nyumba ya Mtakatifu Marta, anakoishi Papa Francisko, lilianzishwa, pamoja na Chuo na Eneo la Makaburi, katika karne ya nane mahali ambapo kulikuwapo na hospitali ya wagonjwa, ambapo chakula na nguo ziligawiwa kwa maskini wote ambao walimiminika pale. Katika fursa ya Mwaka Mtakatifu wa 1450 mahujaji wengi walifika Roma, na iliamuliwa kukarabati Kanisa na makaburi. Mnamo 1454 washiriki wa asili ya Wajerumani wa Curia ya Kirumi waliungana na kutegeneza Jumuiya kwa ajili ya marehemu masikini. Mwisho wa karne ya 15, Kanisa la sasa lenye ukumbi mmoja lilijengwa,na  mtindo uliojulikana sana nchini Ujerumani.

Chuo cha makuhani ambao ni wasomi wa akiolojia ya Kikristo

Mnamo mwaka wa 1597 Ushirikiano wa Wajerumani ukawa ni Jumuiya ya ndugu wa Mama Yetu katika uwanja Mtakatifu wa Ujerumani ndani ya mji wa Vatican na kupewa Kanisa. Mnamo mwaka 1876, chuo cha makuhani wanaosoma akiolojia ya Kikristo na historia ya Kanisa na taaluma zinazohusiana ziliongezwa kwenye takwimu hiyo na mnamo 1910, kufuatia na dhoruba kali iliyosababisha uharibifu mkubwa kwa Kanisa, jengo hilo likakarabatiwa.

02 November 2020, 20:20