Tafuta

Dhoruba Iota na  Eta Katika Amerika ya Kati Dhoruba Iota na Eta Katika Amerika ya Kati 

Maombi ya Papa Francisko kwa waliopata pigo cha dhoruba kali Amerika ya Kati

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana Papa Francisko wazo lake limewaendea watu wa Amerika ya Kati ambao wanateseka kutokana na madhara ya mvua kali na mafuriko yaliyosababaishwa na dhoruba mbili kali.Ametoa ushauri ya kipindi cha safari Majilio ambayo inafundisha unyoofu wa moyo,sala na umakini kwa ajili ya walio karibu nasi hasa wenye kuhitaji zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko kabla ya kuondoka dirishani amewaalikwa waamini wote kuwa wema hasa hatika hali halisi ngumu ambayo imesababishwa na janga mbele yetu. Kwa kufanya hivyo amelekeza mambo chanya ya kufuata ili kufanya safari ya Majilio kuwa njema. Mambo hayo amesema ni kuwa na “Umakini mkubwa, busara na uangalifu kwa majirani ambao wanaweza kuwa na uhitaji zaidi, na vilevile kuwa na wakati mfupi wa sala ambayo inafanyika ndani ya familia kwa urahisi”. Papa Francisko amesisitiza tena na kusema  “vitu hivi vitatusaidia sana kwa maana hiyo ni umakini zaidi, busara na uangalifu kwa majirani wenye kuwa na mahitaji zaidi, pamoja na dakika chache za sala ndani ya  familia kwa urahisi”.

Kufuatia na na dhoruba kali iliyopewa jina Eta na Iota iliyopiga Amerika ya Kati hivi karibuni  imesababaisha zaidi ya vifo 200 na idadi isiyojulikana ya waliopotea na wakati huo huo kusababisha  madhara ya mamia ya milioni. Dhoruba hizo kali zimeongozana kabla ya  kufikia hata wiki mbili kwa kuwachia majanga makubwa sana, mafuriko makubwa na uharibifu mkubwa katika Amerika ya kati na visiwa vya Caribbien na Colombia. Dhoruba Eta ilifanya pigo kwa mara ya kwanza tarehe 3 Novemba na ile ya Lota tarehe 16 Novemba kwa kusababisha kunyesha mvua kubwa sana ambayo imeleta ugumu ya ardhi na milima kutelemka kwa matope mengi.

30 November 2020, 09:27