Tafuta

20202.11.26 Ukurasa wa kwanza wa Osservatore wa Dominika ya 13-20 Desemba 1970 20202.11.26 Ukurasa wa kwanza wa Osservatore wa Dominika ya 13-20 Desemba 1970 

Kile kisu ambacho kilisimama sentimita chache kabla ya kuufikia moyo!

Ni miaka 50 iliyopita Papa Paulo VI alishambiliwa mara baada ya kutelemka uwanja wa Ndege wa Manila nchini Ufilipino tarehe 27 Novemba 1970 baada ya safari yake ndefu.Kisu kilisimama sentimita chache kabla ya kuufikia moyo wa Papa Montini.

VATICAN NEWS

Mtu aliyevaa kama kuhani ambaye alishika msalaba kwa mkono mmoja na mwisngine ukiwa na upanga ameuficha. Ndiyo ulioshambulia Papa wa miaka sabini na tatu aliyekabiliana safari ndefu zaidi ya upapa wake. Shambulio hili lilizuia tu shukrani kwa wepesi wa wahudumu wake  wa karibu Hiyo ilitokea miaka hamsini iliyopita, ambapo ilikuwa kwa hakika tarehe 27 Novemba 1970, wakati Papa Paulo VI alipokuwa na zira yake kutembelea Bara la Asia na  Ausatralia. Hija ya kitume ambayo ilikuwa imepata chachu kutokana na Baraza la kwanza wa maaskofu wa Asia ya Mashariki na yote yalikuwa yanakusudiwa kwa hakika kukutana na watu wanaoishi upande wa pili wa ulimwengu, na ujumbe ambao ulikuwa wazi ukifafanua maana ya utamaduni wa imani na utajiri wa muungano wa ukatoliki mzima.

Alikuwa ni Papa Paulo VI mwenyewe aliyewakilisha kwa waamini, wakati wa katekesi yake juu ya ziara yake ya kitume na ambayo kituo cha kwanza kilikuwa ni Manila kwa siki Tatu na baadaye aweze kuendelea katika visiwa vingine, kwa maana hiyo siky nyingine  tatu katika jiji la Sydney, nchini Australia, baadaye kuendelea jijini Jakarta Indosia. Lakini pia kuendelea na safari hadi Hong Kong. Papa Motnini akiendelea na kueleza alisema "ni kwa masaa machache lakini inatosha, tu na  tunatumaini kushuhudia kila kitu bila ubaguzi kwa watu wakuu wa China kwa heshima na upendo wa Kanisa Katoliki na wafanyakazi wetu”. Hatimaye  kituo cha mwisho kilichokuwa kimepangwa ni Colombo. Safari ndefu na ngunu lakini, Papa Montini alifafanua kuwa "nguvu na wajibu vimewasha mapenzi hayo”.

Papa Paulo aliondoka tarehe 26 Novemba na ndege, na kushuka Teheran kwa ajili ya kiufundi mahali alipoweza kupokelewa na kiongozi Persia Reza Pahlavi. Aidhahata Kituo kisichopangwa pia kiliamuliwa huko Dhaka, mashariki mwa Pakistan wakati huo, akitaka kukutana  na watu walioathirika na kimbunga. Papa Montini alitaka kutoa msaada wa fedha  kwa juhudi za misaada ambayo ni pamoja na  mkusanyiko uliofanywa  kwenye ndege kati ya waandishi wa habari walioandamana naye safarini.

Asubuhi ya Novemba 27, mara tu alipofika kwenye uwanja wa ndege wa Manila, Papapa Paulo VI alipata shambulio ambalo lingemgharimu maisha. Katika safari, kwa mujibu wa katibu wake  binafsi Padre Pasquale Macchi aliandika katika kumbukumbu zake kuwa  “Papa alionywa mapema kuwa shambulio linawezekana, kabla ya kuanzia safari ya Nchi Takatifu hadi ile ya mwisho hukp Mashariki ya Mbali. Huduma za siri pia zilihatadharisha kwa Sekretarieti ya Serikali. Na kila wakati  lakini Papa alikwenda kwenye safari zake bila wasiwasi wowote, akimtumaini Mungu".  Wakati huu, hata hivyo, Papa alipata pigo.

“Wakati akisalimiana na viongozi, makadinali na maaskofu,” aliandika katibu wake, "Papa alishambuliwa na mchoraji wa Bolivia, Benjamin Mendoza y Amor, mwenye umri wa miaka thelathini na tano, aliyekuwa amevaa kama kuhani, ambaye alikuwa ameshika msalaba wa dhahabu mkononi mwake na mwingine  uliyofichwa na kitambaa, ni kriss yaani (kisu cha Malaysia na blade ya kuzunguka). Kwa pigo moja alimjeruhi Papa shingoni, kwa bahati nzuri alilindwa na kola ngumuna lingine kifuani karibu na moyo". Katika barua iliyoandikwa na Papa mwenyewe siku hiyo anasema "Ikiwa nakumbuka vizuri, baada ya salam kwa huyo mtu ... nilimwona kwa kuchanganyikiwa mtu huyo... ambaye alikimbilia kunielekea. Mimi nilidhani alikuwa mmoja wa wengi ambao walitaka kunisalimu au kubusu mkono wangu, au kusema kitu ... baada ya kufika mbele yangu nilihisi pigo kali”.

27 November 2020, 14:46