Tafuta

Kifo cha Maradona maarufu wa soka:Papa anamkumbuka katika sala

Watu wengi mashuhuri ulimwengu wa soka kwa ujumla,wanaomboleza kwa kufikiriwa na wengi kuwa mchezaji bora wa nyakati zote.Diego Armando Maradona,mchezaji wa Argentina ambaye Papa Francisko alikutana naye 2014 katika fursa ya mpira wa amani na 2015 katika mantiki ya kuanzisha mipango ya Scholas Occurentes.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ulimwengu wa soka duniani unaomboleza kifo cha Diego Armando Maradona, kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, aliyefariki dunia siku ya Jumatano tarehe 25 Novemba 2020 akiwa na umri wa miaka 60. Watu wengi mashuhuri wa soka kwa ujumla, wanaomboleza kwa kufikiriwa na wengi kuwa mchezaji bora wa nyakati zote, lakini na ambaye alikuwa ni mtu mdhaifu. Papa Francisko amemkubukwa kwa upendo katika mkutano naye kunako mwaka 2014,  katika fursa ya Mpira kwa amani, baadaye mwaka 2015 katika mantiki za  kuanzisha mipango ya Scholas Occurentes.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Diego Maradona, kwa mujibu wa taarifa na msemaji wake, amethibiishwa kuwa amefariki dunia kutokana na mshutuko wa moyo, wiki mbili baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali mahali ambapo alikuwa amefanyiwa upasuaji wa kichwa  hivi karibuni. Ni Mchezaji aliyeiongoza Argentina kutwaa kombe la dunia mwaka 1986, na ambaye anachukuliwa na mashabiki wa soka kama mmoja wa wachezaji wakubwa kuwahi kuandika historia ya mchezo ulimwenguni. Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, Maradona amelazwa hospitali mara tatu kwa hali mbaya ya afya kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya na ulevi. Hivi karibuni, alilazimika kukaa karantini nyumbani kutokana na janga la COVID-19. Serikali ya Argentina imetangaza siku tatu za maombolezo wakati Napoli nchini Italia  ambayo wakazi wake wanamfikiria kama nyumba yake ya pili wamefanya siku moja ya maombolezo na mkesha uliofanyika siku ya kifo chake katika uwanja wa Mtakatifu Paulo.

Papa Francisko amesema kwa mujibu wa  Msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni ya kwamba amehabarishwa kuhusu kifo cha Maradona na amefikiria kwa heshima zile fursa alizoweza kukutana naye kwa miaka hii, pia kumkubuka kwa sala, kama alivyo fanya siku zilizopita mara baada ya kupata taarifa kuhusu hali yake ya afya” . Kuanzia katika viwanja vya vumbi la Buenos Aires hadi vichochoro vya Napoli. Kituko cha michezo wa Maradona, ambaye alipaa kileleni mwa ulimwengu na timu yake ya kitaifa mnamo 1986, ni historia ya mpira wa miguu. Ni historia ambayo haitasahaliwa ya ushindi wa mchuano na Uingereza na utulivu usiosahalika kati ya wapinzani, ambayo ilikuja baada ya bao hilo na ngumi iliyopewa jina “Mano de Dios”. Ushindi wake huko Napoli pia ni sehemu ya historia, ambapo alishinda michuoano mawili, mnamo 1987 na 1990, na Kombe la Uefa.

Juhudi za Maradona za mshikamano na “Scholas Occurentes” haizizishii na mechi ya Olimpiki mnamo 2014. Na aliporudi nchini Italia, bingwa huyo alishiriki katika mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Redio ya Vatican, ambapo aliweza kuelezea mipango ambayo inaonekana na ambayo kila wakati unasifika kwa jina la elimu na mshikamano. Hiyo ndiyo sura ya mkutano mpya kati ya Papa na Maradona ambaye katika maneno ya Papa Francisko yamejaa pongezi na heshima kwake.

26 November 2020, 16:35