Tafuta

2020.11.11 Udienza Generale 2020.11.11 Udienza Generale 

Francisko:Mkristo anayeomba haogopi chochote.Anajiaminisha kwa Roho Mtakatifu!

Katika Katekesi ya Papa katika mada ya sala amesisizia juu ya huruma,ujasiri na unyenyekevu wakati wa sala na ndiyo mambo makuu ambayo lazima yambatanishwe katika kila mazungumzo na Mungu.Mkristo anayesali haopgopi. Ikiwa hatutasali,hatutakuwa na nguvu ya kwenda mbele.Mifano mitatu ya Injili ya Luka kuonesha jinsi ya kusali daima bila bila kuchoka:rafiki wa kuomba mkate usiku wa manane,Mjane na hakimu na Mfarisayo na mtoza ushuru.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatica.

Papa Francisko katika katekesi yake Jumatano tarehe 11 Novemba 2020, akiwa katika makataba ya Jumba la Kitume Vatican ameendeleza mada ya sala. Na katika utangulizi huo ameanza kusema “Tunaendelea na Katekesi kuhusu sala. Kuna mtu ameniambia kwamba “Wewe unaongelea sana juu ya sala. Siyo lazima”. Ndiyo ni ya lazima. Kwa sababu ikiwa sisi hatusali, hatutakuwa na nguvu za kwenda mbele katika maisha. Sala ni kama oksijeni ya maisha. Sala ni kuvutia kwetu uwepo wa Roho Mtakatifu ambaye anatupeleka mbele daima. Ndiyo maana mimi ninazungumzia sana kuhusu sala”, Papa Francisko amefafanua. Akiendelea na katekesi yake amesema Yesu alitoa mfano wa sala ya inayoendelea daima, katika mazoezi na msisitizo.  Huo ndiyo mfano wa Yesu. Mazungumzo yasiyoisha na Baba katika ukimya na katika kujiunda, ndiyo kitovu cha maisha yake yote ya utume. Injili zinatuonesha hata shauri nyingi alizotoa kwa wafuasi ili wasali daima na bila kuchoka. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatukumbusha kuwa kuna mifano mitatu iliyomo katika Injili ya Luka ambayo inasisitiza tabia hii kusali kwa Yesu (KKK, 2613)

Papa  amefafanua kuwa, sala awali ya yote sala lazima iwe ya   huruma …kama mfano wa mtu ambaye alimpokea mgeni wa ghafla, usiku wa manane na kwenda kubisha mlango kwa rafiki yake na kumuomba mkate. Lakini Rafiki akajibu “hapana!” kwa sababu alikuwa tayari amelala, lakini yeye akaendelea kumsihi hadi kulazimisha aamke na kumpatia mkate (Lk11,5-8). Ombi la huruma. Lakini Bwana ni mwenye uvumilivu na sisi, yeyote abishaye hodi kwa imani na msisitizo  mlango wa moyo wake,  Yeye hafungi kamwe. Mungu daima anajibu. Baba Yetu anajua vema ni kitu gani tunahitaji. Msisitizo hautumiki kumjulisha au kumshawishi, lakini hutumika kulisha hamu na matarajio ndani yetu, Papa amebainisha.

Mfano wa Pili ni ule wa mwanamke mjane na hakimu,  ambaye alikwenda kwa hakimu ili amsaidie kupata haki yake. Huyo hakimu lakini mfisadi  ambaye hakuwa anajali, hatimaye kutokana na msisitizo wa mwanamke huyo, aliamua kumtimizia haki yake (Lk 18,1-8).  “Yeye alifikiria ni bora kutoa suluhisho la tatizo hilo ili aondokane naye asiendelee kulalamika mbele yangu”. Mfano huu unatufanya tuelewe kwamba imani sio kimbilio la muda, lakini ni tabia ya ujasiri ya kumwomba Mungu, hata “kujadili” naye, bila kujiachilia kwa uovu na udhalimu Papa Francisko amebainisha.

Mfano wa tatu, Papa Francisko amebainisha unawakilishwa na ule wa mfarisayo na mtoza ushuru ambao walikwenda kusali Hekaluni. Wa kwanza akamwelekea Mungu kwa kujidai mastahili yake; na mwingine alihisi kutostahili hata kuingia ndani ya madhabahu hayo. Mungu lakini hasikilizi sala ya kwanza yaani ya wenye kiburi,  wakati  anasikiliza wale wenyenyekevu (Lk 18,9-14). Hakuna sala ya kweli bila roho ya unyenyekevu na ndiyo ambayo inatupeleka kuomba, na kusali… Papa amesisitiza.  Mafundisho ya Injili yako wazi, lazima husaida daima hata kama kila kitu ambacho utafikiri hakiwezekani, wakati inaonekama kuwa Mungu ni kiziwi na kipofu na utafikiri ni kupoteza wakati. Hata kiwa angani ni giza, Mkristo haachi kuomba.

Maombi yake yanaenda sambamba na imani. Na imani, katika siku nyingi za maisha yetu, inaweza kuonekana kama udanganyifu, juhudi tasa: na kuna wakati wa giza maishani mwetu. Na hapo, ndipo daima unafikiri imani ni udanganyifu. Lakini kufanya mazoezi ya sala kunamaanisha pia kukubali juhudi hii. Watakatifu wengi wamepitia uzoefu huo wa usiku wa imani na ukimya wa Mungu, na watakatifu hao waliweza kuomba daima. Katika usiku wa manene anayesali siyo peke yake kamwe.

Yesu kwa hakika siyo shuhuda peke yake na mwalimu wa sala, ni zaidi ya yote. Yeye anatupokea katika sala yake ili nasi tuweze kusali na Yeye na kwa njia yake. Hii ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa sababu hii, Injili inatualika kusali kwa Baba na kwa jina la Yesu. Mtakatifu Yohane anatumia maneno hayo ya Bwana. “Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwa ndani ya mwana (Yh, 14, 13). Na Katekisimu inaelezea kuwa “uhakika wa kusikilizwa katika maombi yetu msingi wake ni Yesu (KKK n.2614). Uhakika huo unatoa mabawa katika sala ya mtu aliyokuwa daima anatamani kuwa nayo. Je! Tunawezaje kukosa kukumbuka hapa maneno ya Zaburi ya 90, yaliyojaa uaminifu, yakitoka katika moyo unaotarajia kila kitu kutoka kwa Mungu: “Atakufunika kwa manyoya yake, chini ya mabawa yake utapata kimbilio; uaminifu wake utakuwa ngao yako na silaha zako. Hautaogopa hofu ya usiku au mshale unaoruka mchana, tauni inayotangatanga gizani, maangamizi ambayo huharibu adhuhuri”(Zab 90, 4-6).

Ni katika Kristo kwamba maombi haya mazuri yanatimizwa, ni ndani yake ambayo hupata ukweli kamili. Bila Yesu, sala zetu zingehatarishwa kuwa juhudi za wanadamu tu, na wakati mwingi zimepotea. Lakini yeye ametawaa kila kilio, kila kwikwi, kila shangwe, kila ombi ... yaani kila sala ya binadamu, amesisitiza Papa.  Kwa kuongeza amesema Na tusisahau Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huomba ndani yetu. Ni Yeye ambaye anatuongoza kusali, anatuongoza kwa Yesu: yeye ndiye Zawadi. Ni zawadi ambayo Baba na Mwana wametupatia  ili kwenda mbele kukutana na Mungu. Na Roho Mtakatifu, tunapoomba, ndiye Roho Mtakatifu ambaye anasali mioyoni mwetu. Kristo ndiye kila kitu kwetu, hata katika maisha yetu ya maombi. Mtakatifu Agostino alisema haya katika  maelezo ya kuelimisha, ambayo tunapata kutoka  katika Katekisimu pia kwamba: Yesu atuombee kama kuhani wetu; anaomba ndani mwetu kama kiongozi wetu; tunamuomba sisi kama Mungu wetu. Basi, na tutambue sauti yetu ndani yake, na sauti yake ndani yetu” (n. 2616). Ni kwa sababu hiyo kwamba Mkristo anayeomba haogopi chochote. Anajiaminisha kwa Roho Mtakatifu, ambaye tumepewa kama zawadi, na ambaye huomba ndani mwetu na kutuongoza katika maombi. Na kwa njia hiyo Papa Francisko kwa kuhitimisha amesema na “Awe ni Roho Mtakatifu mwenyewe, Mwalimu wa sala, ambaye atufundishe njia ya sala.”

KATEKESI PAPA
11 November 2020, 15:30