Tafuta

2020.11.21 KITABU CHA PAPA:-CIELO-SULLA-TERRA 2020.11.21 KITABU CHA PAPA:-CIELO-SULLA-TERRA 

Francesco:Ukristo hubadili ulimwengu ukiwa una msimamo wa Injili

Kuna kitabu kipya cha Papa katika duka la vitabu Vatican (Lev)chenye jina“Mbingu duniani.Kupenda nakutumikia ili kuubadilisha ulimwengu”. Dibaji ni ya Martin Junge,Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni ambaye ameandika:“Pamoja tunashuhudia huruma ya Mungu kwa kukiri imani katika huduma yetu ya pamoja katika ulimwengu.”

VATICAN NEWS

Wakati Ukristo unapojikita katika Injili ndiyo unatoa ubora wake katika ustaarabu, na wakati huo huo unapoteza bora wake wakati unapoishia kuharibu na kujitambulisha na mantiki na miundo ya kiulimwengu. Ndivyo anaandika Papa katika maandishi ambayo hayajachapishwa na ambayo yanaonekana katika kitabu kiitwacho “Mbingu duniani. Kupenda na tumikia ili kuubadilisha ulimwengu”. Ni kitabu hicho hicho chapisho la Vatican kitatolewa katika duka la vitabu Vatican siku ya Jumanne tarehe 24 Novemba 2020, na ambacho kimejumuishwa katika safu za vitabu vya kiekumene kama kile cha “Kubadilishana zawadi” na ni ukusanyaji wa  maandiko mbali mbali ambayo tayari yamesemwa na Papa Francisko juu ya mada ya imani ambayo inabadilisha kuwa upendo kwa wengine. Dibaji ya kitabu hicho ni kutoka kwa mchungaji  Martin Junge, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni.

Katika maandishi Papa Francisko anasisitiza nguvu ya kubadilisha ya Ukristo kwa karne nyingi, kuanzia kutafakari thamani ya kila mtu. Ulimwengu mpya, wa haki na kidugu ambao ulizaliwa kama matokeo ya bure ya imani iliyofanyiwa uzoefu tu. Ukristo, anabainisha haukubadilisha ulimwengu wa zamani na mbinu za ulimwengu au hiari za maadili, lakini ni kwa nguvu ya Roho wa Yesu aliyefufuka. Mto mzima wa kazi ndogo au kubwa za upendo, mkondo wa mshikamano ambao umekuwa ukipita katika historia kwa miaka elfu mbili, una chanzo hiki kimoja tu anasisitiza Papa. Upendo huzaliwa kutokana na hisia ya huruma, kutokana na mshangao, kutokana na neema.

Tangu mwanzo kabisa, wa kihistoria, upendo wa Wakristo umekuwa na  tahadhari  na umakini kwa mahitaji ya watu dhaifu zaidi, wajane, maskini, watumwa, wagonjwa, waliotengwa, Huruma, kuteseka na wale wanaoteswa, kushirikishana. Lakini hata hivyo hisotria hiyo inageuka kuwa ukosoaji wa dhuluma na kujitoea ili kukabiliana nayo kadiri inavyowezekana. Kwa sababu kumtunza mtu kunamaanisha kumkumbatia hali yake yote na kumsaidia kujikomboa kutoka kwa kile kinachomkandamiza zaidi na kumnyima haki zake. Ukuu wa Neema anahitimisha Papa hauongozi kupuuza, badala yake huongeza nguvu mara mia na huongeza unyeti dhidi ya dhuluma”.

Katika utangulizi wake, Mchungaji   Martin Junge, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri la Ulimwengu, anakumbuka kwa shukrani kubwa maneno ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Maadhimisho ya Pamoja ya Magueuzi huko Lund mnamo 2016.  Yeye anaadika kuwa :“Yesu anatukumbusha: Bila mimi humwezi kufanya lolote  (Yohane 15.5). Yeye ndiye anayetuunga mkono na kututia moyo kutafuta njia za kufanya umoja kuwa ukweli unaozidi kuonekana”. Katika liturujia hiyo ya kukumbukwa, anaandika Junge, “sisi Wakatoliki na Walutheri kwa pamoja tulithibitisha kujitoa kwetu kwa njia inayoongoza kutoka katika  vita hadi ushirikiana.

Safari hii inawezekana tu kwa sababu ya Kristo, ambaye huponya majeraha na kumbukumbu zetu zote, akituweka huru kutoka kwa maumivu ya uzoefu wa zamani, kukumbatia zawadi ya upatanisho ambayo Kristo ameweka kati yetu.” Hii ina maana ya kujitoa ameelezea Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kilutheri Ulimwengu na “ambayo huanza kutoka kwa mtazamo wa umoja na siyo kwa mtazamo wa mgawanyiko kwa sababu kinachotuunganisha ni zaidi ya kile kinachotugawanya. Na ni kujito ambayo inakuwa huduma ya pamoja kwa walio wachache na wanaoteseka: Pamoja tunashuhudia huruma ya Mungu kwa kukiri imani na kwa huduma yetu ya pamoja katika ulimwengu”.

23 November 2020, 16:16