Tafuta

Askofu Mkuu Samuel KLEDA, wa Jimbo Kuu katoliki  Douala, Kamerun  Askofu Mkuu Samuel KLEDA, wa Jimbo Kuu katoliki Douala, Kamerun  

Baba Mtakatifu amemteua Askofu wa jimbo la Eséka nchini Kamerun!

Papa Francisko amemteua Padre François Achille Eyabi kuwa askofu wa Eséka nchini Kamerun.Hadi uteuzi wake alikuwa ni makamu askofu wa Jimbo. kuu Douala

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre François Achille kuwa wa Askofu wa jimbo katoliki la Eséka nchini Kamerun. Hadi uteuzi alikuwa ni Makamu Askofu na Paroko wa Kanisa kuu Douala. Askofu Mteule François Achille Eyabi alizaliwa tarehe 30 Septemba 1961 huko Ngambe (Edéa). Masomo yake ya msingi na sekondari alisomea katika Seminari ndogo ya Bonépoupa na kuendelea na kidato cha tano sita huko Edéa, na baadaye katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo ya Nylon huko Douala.

Alipata daraja la Upadre kunako tarehe 30 Julai1988 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Douala, lakini baada ya kugawa jimbo kunako mwaka 1993 akahamishiwa kwenye Jimbo la Edéa. Majukumu mengine ya kichungaji ni uparoko katika parokia mbali mbali, makamu askofu katika jimbo. Na baadaye 1996-2000, alitumwa Roma kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana, (mafunzo ya Taalimungu na baadaye Udaktari katika Taalimungu Takatifu. Kunako 2001-2004, Gambera wa Seminari kuu ya Kikanda huko Douala na kuendelea hadi (2005-2011); Paroko wa Kanisa kuu na Katibu wa Kitengo cha Elimu Katoliki cha Jimbo.

 

14 November 2020, 16:17