Tafuta

Maisha ni matakatifu lazima kulindwa kuanzia kutungwa kwake hadi mwisho wa maisha. Maisha ni matakatifu lazima kulindwa kuanzia kutungwa kwake hadi mwisho wa maisha. 

Argentina:Papa apongeza juhudi za “mujeres de las villas”

Papa Francisko anawapongeza wanawake “mujeres de las villas”,na kuwashukuru kwa moyo wote kwa jitihada yao na ushuhuda wa kupinga mswada wa kutoa mimba na anawatia moyo waendelee mbele.“Nchi inajivunia kuwa na wanawake kama hawa.Tatizo la utoaji mimba siyo suala la dini tu,lakini ni wa maadili ya binadamu,kabla ya jambo lolote la imani ya kidini,Papa amesema.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Katika barua ya Papa Francisko aliyoandika kwa mkono wake inayoonesha tarehe 22 Novemba, Papa anaonesha pongezi na shukrani za kulinda maisha dhidi ya kutaka kuhalalisha nchini Argentina zoezi la utoaji mimba. Katika barua iliyo elekezwa kwa naibu Victoria Morales Gorleri, anajibu barua iliyotumwa kwa Papa na “mujeres de las villas”, yaani mtandao wa wanawake ambao tangu mwaka 2018 wanapambana wakitetea maisha ambayo hayajazaliwa hasa katika mitaa ya watu wa Buenos Aires.  Kwa namna ya pekee, saini za pamoja za ujumbe wao zilikuwa zinaomba msaada kutoka kwa Papa katika jitihada zao kupambana dhidi ya kuhalalisha utoaji kwa ihari  wa mimba, ambapo kwa sasa katika nchi hiyo umezua mjadala mkubwa.

Je ni haki kuondoa maisha au kuwa muuaji?

Katika jibu la Papa, anawashukuru kwa moyo wote wanawake hao “mujeres de las villas”, huku alielezea pongezi na mshangao kwa jitihada yao na ushuhuda na anawatia moyo ili waendelee mbele. “Nchi inajivunia kuwa na wanawake kama hawa”,  anaendelea Papa Francisko kwa kubainisha kuwa“ tatizo la utoaji mimba siyo suala msingi wa dini, lakini ni wa maadili ya binadamu, kabla ya jambo lolote la imani ya kidini”. Kwa maana hiyo Papa anasema ni vema kujiuliza maswali mawili, ili kuweza kupata suluhisho: “Je ni haki kuondoa maisha ya binadamu? Je ni haki kuwa muuaji? Katika Barua hiyo anahitimisha kwa kuwapa baraka wanawake na kuaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

Sauti yetu ni kama ile ya watoto ambao hawajazaliwa

Kwa upande wa wanawake wa “de las villas”, katika barua yao ya pamoja, waafafanua kwa Papa, hasa kwa sababu mswada wa sheria juu ya utoaji wa mimba uliwakilishwa na sehemu kubwa kama suluhisho rahisi kwa vijana ambao wanaishi kwenye mitaa na ambao wanajikuta wamebeba mimba.  Katika barua yao wanasema “tumechoka na ubaridi wa hofu kubwa, hasa ikiwa tunafikiria kwamba muswada huu unakusudia kukuza wazo kwamba utoaji mimba ni uwezekano mwingine katika hali hiyo ya njia za uzazi wa mpango na kwamba walengwa wake wakuu ni wasichana maskini”. “Sauti yetu, kama ile ya watoto ambao hawajazaliwa, haisikilizwi kamwe, wanasisitiza wanawake, Watunga sheria  na waandishi wa habari hawataki kutusikiliza na  katika kukundi chetu (Villas) hatuna  makuhani wa kupaza sauti, na hivyo tutaendelea kuwa peke yetu zaidi. Mabinti zetu vijana wanakua na wazo kwamba hawana haki ya kupata watoto kwa sababu ni maskini”. Kutokana na hayo ndipo wanatoa wito wa mwisho kwa Papa ili waweze kupata msaada wake.

Maandamano ya kupinga utoaji mimba tarehe 28 Novemba

Ikumbukwe Jumamosi tarehe 28 Novemba 2020 nchini Argentina, wanatarajia kufanya maandamamko ya kupinga mswada wa sheria ya utoaji mimba. Hata hivyo tarehe 20 Novemba 2020, Kamati ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya maisha, walei na familia (Cevilaf) ,nchini humo, imesema hii ni kwa mara ya kwanza nchini Argentina katika demokrasia, inaweza kutokea sheria ya namna hiyo ambayo inajumuisha kifo cha mtu ili kumwokoa mwingine, “na kumbe ni kwa ajili ya kuokoa maisha ya wote wawili na ndipo tunaweza kuokoa wote” walisema maaskofu. Hatimaye Maaskofu wanashauri waamini kujitokeza kwa wingi pamoja katika maandamano Jumamosi ijao. Ambayo ni kileleza cha kuonesha haki ya binadamu katika maisha ya kila mtu na ambayo imehakikishwa katika Katiba yao.

26 November 2020, 16:24