Wasiwasi na maombi ya Papa kwa ajili ya Nigeria!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Ninafuatilia kwa wasiwasi hasa habari inayokuja kutoka Nigeria. Ndivyo Papa Francisko ameanza mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana akiwaeleza waamini na mahuaji waliounganika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, na hasa kufuatia na mivutano ya ulimwengu hasa kwa upande wa mapigano ya hivi karibuni kati ya polisi na waandamanaji vijana nchini humo. Papa amesema tuombe kwa Bwana ili kila aina ya vurugu iepukwe kila wakati katika kutafuta mara kwa mara maelewano ya kijamii kwa njia ya kuhamasisha haki na wema wa wote.
Matukio ya mwezi huu Oktoba katika nchi ya Afrika inayoangalia Ghuba ya Guinea
Vuguvugu la maandamano lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi Oktoba, baada ya video kwenye mitandao ya kijamii kuenea ikioonyesha mawakala wa SARS kumuua kijana katika mji wa kusini mwa Ughelli nchini humo mnamo tarehe 3 Oktoba, lakini mamlaka ya Nigeria inasema video ilikuwa ya uwongo. Mtu aliyetengeneza video hiyo alikamatwa na kuongeza hasira ya waandamanaji. Kwa namna ya pekee kuna maandamano dhidi ya matumizi ya nguvu na polisi, hasa na Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi (SARS), vitengo ambavyo vimeshutumiwa kwa miaka mingi kuhusu ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ambao waandamanaji wanataka kukomeshwa. Hata hivyo pia waandamanaji wameanza kutoa wito wa kuwepo mageuzi kwa jumla katika nchi hiyo.