Tafuta

2020.10.07 Katekesi ya Papa 2020.10.07 Katekesi ya Papa 

Papa: wanahitajika wakristo jasiri wa kusema wazi kile kisichotakiwa kufanywa!

Katika tafakari ya katekesi ya Papa Francisko kwenye ukumbi wa Paulo VI amaerudia kwa upya mwendelezo wa sala baada ya mzunguko wa kipindi cha Kazi ya uumbaji wa ulimwengu uliojeruhiwa na janga la corona.Papa amesema kusali siyo kupamba roho,bali ni kakabiliana na Mungu ambaye anasukuma kwenda kutumikia ndugu.Kwa mfano wa Eliya wanatakiwa wakristo jasiri wa kusema wazi kisichotakiwa kufanyika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumatano tarehe 7 Oktoba 2020 Papa Francisko ameendelea na mada ya sala katika Katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika ukumbi wa Papa Paulo VI mjini Vatican. Somo lililoongoza tafakari ya Papa katika katesi ni kutoka kitabu cha kwanza cha Wafalme (1 Re 19,11-13). Mahali ambapo Bwana anamwambia Eliya atoke nje na kusimama juu ya mlima kwa uwepo wa Bwana. Ppa Francisko akianza amesema " Leo ni mwendelezo wa katekesi kuhusu sala ambayo tuliikatisha kwa ajili ya kufanya katekesi juu ya Utunzaji wa Kazi ya Uumbaji na sasa ni kuendelea na sala hiyo  ambapo tunakutana na mmoja wa watu wanaokaribia zaidi Maandiko Matakatifu kama Nabii Eliya. Yeye anakwenda zaidi ya mipaka ya wakati wake na tunaweza pia kuona uwepo wake katika vipindi kadhaa vya Injili. Yeye anaonekana karibu na Yesu akiwa pamoja na Musa, wakati wa Kung’ara  kwa Yesu ( taz Mt 17,3). Yesu mwenyewe anamtaja kama sura muhimu ya ushuhuda na Yohane Mbatizaji (taz Mt 17,10-13). 

Katika mwendelezo wa tafakari kuhusu sala, Papa amesema katika Biblia Eliya anaonesha kutokeza kwa ghafla kwa namna ya maajabu katika kijiji kidogo kilicho pembeni (taz 1Waf 17,1) na mwisho ataondoka  kimaajabu akiwa katika  mtazamo wa macho ya mfuasi wake Elisha ambapo atachukuliwa mbinguni na gari la moto pamoja na farasi wa moto ( taz 2Wafal 2,11-12). Kwa hakika huyo ni mtu hasiye na asili kamili, hasa bila kuwa na mwisho kutokana na  kunyakuliwa kwenda mbinguni na ndiyo maana  kurudi kwake kulitarajiwa tena  kama tukio la Masiha. Ni kama mwombezi. Na hivyo ndivyo walikuwa wakisuburi kurudi kwa Eliya. Maandiko yanawakilisha Eliya kama mtu wa imani angavu, Papa amebainisha. Jina lake mwenyewe linaweza kuwa na maana ya “Yahwe” yaani ni Mungu”. Hili linafungia ndani siri ya utume wake. Itakuwa hivyo kwa maisha yake yote. Ni mtu mnyoofu, asiye jaribiwa na mambo uchoyo. Ishara yake ni moto, ambayo ni picha ya nguvu ya mUngu inayotakasa. Yeye akiwa wa kwanza alijaribiwa kwa nguvu na kubaki na imani. Ni mfano wa watu wote wenye imani ambao wanatambua majaribu na mateso, lakini hawakati tamaa na kulaumu kwa nini walizaliwa.

Papa Francisko amesema, sala ni kiini kinachomwilisha mara kwa mara kuishi kwake. Kwa maana hiyo ni mmoja wa watu wapendwa zaidi katika utamaduni wa kimonastiki, hadi kufikia kwamba baadhi walichagua kuwa kama baba wa kiroho wa maisha ya utawa kwa Mungu. Elia ni mtu wa Mungu, ambaye analisimama kidete kama mtetezi wa ukuu wa Aliye juu. Licha ya hayo hata yeye analazimika kukabiliana na udhaifu wake binafsi. Ni vigumu kueleza ni uzoefu gani uliweza kumsaidia, kwa kushinda kwake manabii wa uongo katika mlima wa Karmeli (taz 1Wafal 18,20-40). Kwani pamoja na hayo kuna mshangao ambao unaonesha ndani mwake akisema kwamba “yeye si bora kuliko baba zake” (taz 1Wafal 19,4). Katika sala inatokea daima hili. Wakati wa sala ambao tunahisi na kutuvutiwa, hata shauku na kipindi cha sala wakati wa uchungu, wa ukavu, wa majaribu… Sala ndiyo ilivyo. Kujiachia uchukuliwe na Mungu,  kujiachia hata kujaribiwa katika hali mbaya sana hata vishawishi…… Ndani ya roho ya yule anayesali hata kwa udhaifu wake binafsi ni wenye thamani kubwa wakati wa kukwezwa juu, hasa wakati inapoonekana kwamba maisha ni kama farasi wa ushindi na mafanikio. Hii ndiyo hali halisi ambayo inapatikana katika miito mingine mingi ya kibiblia, hata katika Agano Jipya kwa mfano kufikiria Mtakatifu Petro na Paulo. Na maisha yao yalikuwa namna hiyo.  Kipindi cha furaha na kipindi kigumu na cha mateso.

Eliya ni mtu wa maisha ya kutafakari kwa kina na wakati huo huo kujishughulisha na maisha ya  kazi, anahangaikia matukio ya wakati wake. Ni mwenye uwezo wa kupambana dhidi ya mfalme na malkia baada ya hawa kumuua Nabothi ili kumiliki shamba lake la mizabibu (taz 1 Wafak 21,1-24). Papa Francisko kwa kukazia amesema tunahitaji sana waamini, Wakristo wenye bidii, ambao wamekwa na  watu na wana majukumu ya usimamizi na ujasiri kama wa Eliya, na kuweza kusema kwamba “ Hili haifai kufanywa! Na Hayo ni mauaji!”.  Amekazia. Tunahitaji roho ya Eliya. Maombi sio kujifungia tu  ndani na Bwana ili kuweka mapambo kwenye nafsi yako: hapana, hiyo siyo sala. Hii ni sala ya uongo. Maombi ni kukabiliana na Mungu na kuruhusu mwenyewe akutume ili  ukawatumikie ndugu. Jaribio la sala ni upendo thabiti kwa jirani yako. Kinyume chake: wamini huweza kutenda katika ulimwengu baada ya kukaa kimya kwanza na kuomba; vinginevyo kitendo chao ni cha msukumo, na hakina utambuzi;  ni mbio kali bila lengo lote. Na waamini wanapofanya hivyo, hufanya dhuluma nyingi kwa sababu hawaendi  kwa Bwana kwanza kuomba, ili kugundua kile wanachopaswa kufanya.

Hii ni kutaka kutuonesha kuwa pasiwepo mambo mawili tofauti  katika maisha ya yule anayesali. Kwa maana hiyo ni katika uwepo mbele ya Bwana na pia kwenda kukutana na ndugu ambaye Yeye anamtuma. Uthibitisho wa sala ni upendo wa dhati kwa jirani. Sura ya Biblia inaacha mshangao kwamba hata imani ya Elia alitambua maendeleo. Kwa maana  yeye alikulia katika sala, sala imuunda hatua moja baada ya nyingine. Sura ya Mungu iligeuka kwake yeye kuwa  nzuri wakati wa safari. Hata kwa  kufikiria hitimisho lake katika uzoefu maalum, Mungu alipojionesha kwa Elia juu ya Mlima (1Wafal 19, 9-13).  Alijionesha si katika dhoruba kali, si katika tetemeko au moto,  lakini katika sauti ndogo tulivu. Ni katika ishara hiyo ya kinyenyekevu ambayo Mungu anawasiliana na Elia na ambaye hadi wakati huo alikuwa ni nabii anayekimbia na ambaye alikuwa amepoteza amani. Au bora tafsiri ambayo inaangazia vizuri uzoefu huo katika uvumi  wa upepe kwa ukimya. Namna hiyo Mungu alijionesha kwa Eliya. Mungu anakuja kukutana na mtu aliyechoka, mtu ambaye alikuwa anafikiria ameshindwa kwa kila kitu na katika upepo mwanana inamfanya atulie moyoni mwake na kuwa na amani.

Kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema hili ndilo tukio la Elia lakini ambalo utafikiri  limeandikwa kwa ajili yetu sote. Usiku mmoja inawezekana kuhisi bila kuwa na faida  na upweke. Na kumbe hapo ndipo sala inakuja na kubisha mlango wa mioyo yetu. Kama alivyopokea nusu joho lake mtume Elisha nasi tunaweza kulipokea wote.  Na hata kama tunaweza kuwa tumekosa kitu au kuhisi kwamba tuko hatarini na kuwa na hofu, kwa kurudia kwa Mungu kwa njia ya sala, tutarudi kwa miujiza hata kwa utulivu na amani. Hicho ndicho tunafundishwa mfano wa Eliya.

KATEKESI PAPA

 

07 October 2020, 14:17