Tafuta

2020.10.24 Mkuntano wa Wanafunzi wa na walimu wao wa  Kitivo cha Taalimungu cha Kipapa 'Marianum'  na , 2020.10.24 Mkuntano wa Wanafunzi wa na walimu wao wa Kitivo cha Taalimungu cha Kipapa 'Marianum' na , 

Papa Francisko:kwa wanachuo wa Marianum amesema Dunia bila mama hakuna wakati ujao

Katika mkutano wa Papa na walimu na wanafunzi wa Kitivo cha Taalimungu cha Kipapa “Marianum”,Roma,amewakumbusha kuwa nyakati tunazoishi ni nyakati za Maria,mama anayezaa maisha na mwanamke anayetunza watu wa Mungu.Je ni mama wangapi hawapati hadhi yao inayostahili?Ni swali la Papa Francisko akitazama sura ya Mama wa mbingu na mama yetu Maria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi tarehe 24 Oktoba 2020 amekutana na wakuu na wanafunzi wa Kitivo cha kitaalimungu cha Kipapa * Marianum Roma. Katika hotuba yake amejikita kutazama sura ya Mama maría na hasa akiomba kujiuliza juu ya elimu ya Maria inasaidia nini leo hii Kanisa na ulimwengu. Jibu  ambalo ametoa ni kuitikia Ndiyo. Kwenda katika shule ya Maria kwa imani na maisha. Yesu ni mwalimu kwa sababu ni mfuasi wake, anafundisha alfabeto mpya ya maisha ya binadamu na kikristo. Lakini pia kuna mantiki nyingine ambayo inafungamana na leo hii. Tunaishi katika kipindi cha Mtaguso Mkuu wa  II wa Vatican . Hakuna mtaguso mwingine katika historia ambao umeweza kutoa maana kubwa ya nafasi ya somo la Maria ambaye inaelezwata katika haya ya VIII ya Lumen Gentium yaani Mwanga wa mataifa ambayo inahitimishwa kwa namna moja kama mhutasari mzima wa Hati ya Mafundisho kuhusu Kanisa.

Papa Francisko amesema hiyo inatuelezea kuwa nyakati ambazo tunaishi ni nyakati za Maria. Lakini tunahitaji kugundua kwa upya kwa mujibu wa mantiki ya Mtaguso Mkuu. Katika  Mtaguso uliwekwa mwanga uzuri wa Kanisa wa kurudi katika kisima na kuondoa lile vumbi ambalo lilikuwa limeangukia juu yake katika mchakato wa karne, kwa namna ya kushangaza ya Maria, na ambayo kwa dhati inawezekana kugundua vema zaidi katika kwenda katika moyo wa fumbo lake. Pale panabubujika mambo mawili Papa Francisko amesisitiza ambayo yanaelezwa na Maandiko matakatifu kwamba yeye ni mama na mwanamke. Papa Francisko akifafanua maana ya Mama amesema, alitambuliwa na Elzabeth kama mama wa Bwana, Theotokosi Mama wa Mungu pia ni mama yetu sisi sote. Kiukweli kwa mtume Yohane  na katika yeye ina maana kila mmoja wetu, Bwana juu ya msalaba alimwambia “tazama huyo ni mama yako (Yhn 19,27). Yesu katika masaa yale alikuwa akitoa maisha yake kwetu  sisi na roho yake. Na hakuacha kazi yake itimizwe bila kutupatia mama, kwa sababu alitaka kuwa katika maisha tutembee na mama, aliye bora zaidi ( Evangelii gaudium 285).

Papa Francisko akitoa mfano halisi amesema Mtakatifu Francis wa Assisi alikuwa anapenda mama yake. Kwa upande huo  wameaandika kuwa alikuwa na upendo Mama wa Bwana Yesu, kwa sababu Mama yetu alimfanya Mungu kuwa ndugu yetu na kama mama anaweza kufanya Kanisa na ulimwengu kuwa ndugu zaidi.( reje (Mt. BONAVENTURA, Legenda major, 9,3: FF 1165). Kanisa linahitaji kugundua tena moyo wa mama, ambao pigo la umoja; lakini Dunia yetu inahitaji pia, kurudi kuwa nyumba ya watoto wake wote. Mama yetu anatamani,  na anataka kuzaa ulimwengu mpya, ambapo sisi sote ni ndugu, ambapo kuna nafasi kwa kila mtu bila kuwapo na kubaguliwa na jamii zetu( Frtelli tutti 287).

Papa Fracisko akiwageukia wote amesema Marianum inaitwa kuwa taasisi ya kidugu si kwa sababu tu ya kuwa na hali ya kifamilia ambayo inawatofautisha lakini pia kwa kufungulia uwezekano mpya wa kushirikiana na taasisi nyingine ambazo zitawasaidia kuwa na maono zaidi na kubaki katika mchakato wa hatua za nyakati. Wakati mwingine kuna hofu ya kujifungua, kwa kufikiria kupoteza sifa maalum zinazowahusu, lakini ni lazima kuthubutu ili kutoa maisha, kuzaa wakati ujao na huwezi kukosea kwa sababu inafanya kama wafanyavyo mama. Na Maria ni mama ambaye anatufundisha sanaa ya kukutana na kutembea kwa pamoja . Hii ni njia nzuri kabisa ya kuwa na familia kubwa, Marianum  inajumuisha tamaduni za kitaalimungu, tasaufi tofauti ambazo zinachangia hata mazungumzo ya kiekuemene na kidini.

Sehemu nyingine ya pili, Papa Francisko ameeleza kuwa,  mama María ni mama. Katika mafundisho ya Maria na labda katika Agano la kale. Iinasema “Mwokozi amezaliwa  na mama ( Gal 4,4). Katika Injili baadaye Maria ni mwanamke, Eva mpya ambaye kutoka Cana hadi Calvari anaingilia kati kwa ajili ya wokovu (Yh 2,4; 19,26). Hatimaye anaonekana ni  mwanamke aliyevikwa na  jua  na anatunza uzao wa Yesu ( Uf 12,17). Kama mama anafanya Kanisa kuwa familia, kwa maana hiyo mwanamke anawatunza watu wote yaani sisi. Si kwa bahati mbaya kwamba zipo ibada za watu ambazo zinachota uasili wa Mama huyo Papa Francisko amebainisha. Ni muhimu kwamba shule ya Maria ifuate kwa umakini, ihamasishe na wakati mwingine itakase  na kubaki daima makini kwa ishara za nyakati za Maria ambaye anaendelea kutembea katika wakati wetu, Papa Francisko amesisitiza.

Miongoni mwa haya, kuna jukumu la wanawake: muhimu kwa historia ya wokovu, na inaweza  kuwa ya  Kanisa na kwa ulimwengu. Lakini ni wanawake wangapihawapati hadhi yao inayostahili! Mwanamke, aliyemleta Mungu ulimwenguni, lazima awe na uwezo wa kuleta zawadi zake katika historia. Kuna haja ya ustadi na mtindo wake unaohitajika. Taalimungu inahitajika, ili isiwe ya kufikirika na ya dhana, lakini  ya kusimulia na hai. Mafundisho ya Mama Maria hasa yanaweza kusaidia kuleta tamaduni, pia kupitia sanaa na mashairi, uzuri ambao unabadilisha na kukuza tumaini. Na inaitwa kutafuta nafasi zinazostahili zaidi kwa wanawake katika Kanisa, kuanzia na heshima ya kawaida ya ubatizo.

Kwa sababu Kanisa, kama alivyosema, ni mwanamke. Kama Maria yeye ni mama. Kwa kutoa mfano amesema Padre Rupnik alitengeneza picha, ambayo inaonekana kuwa picha ya Mama, lakini ya sio ya mama.  Inaonekana kwamba Mama yuko mbele, na badala yake ujumbe ni kwamba Mama hayuko mstari wa mbele kwa maana anampokea Yesu, kwa mikono yake, anapiga hatua mbele ya kumshusha ngazi akiwa amemshikilia mikono  kwa ajili ya kutukabidhi kwani ni  mama yetu. Na Kristo anaonekana kama mtoto, lakini ni Bwana na Sheria mkononi mwake. Yeye ni kama mtoto wa mwanamke, dhaifu, akishikilia vazi la mama. Kazi hii ya Padre Rupnik ni ujumbe Papa Francisko amesisitiza.  Je Maria ni nani kwetu sisi? Swali la Papa Francisko  na kwamba ambaye kwa kila mmoja wetu anamfanya ashuke Kristo Mungu mkamilifu. Kristo mtu ambaye alijifanya mdhaifu kwa ajili yetu. Tunamuona Mama yetu namna hiyo,  yeye anayemfanya Kristo aingie, ambaye hufanya Kristo kupita, ambaye alimzaa Kristo, na hubaki kuwa mwanamke kila wakati. Ni rahisi sana ... Na tumwombe  Mama yetu atubariki, amehitimisha

24 October 2020, 12:19