Tafuta

2020.10.28Katekesi ya Papa  2020.10.28Katekesi ya Papa  

Papa Francisko:Yesu ni kongozi wetu katika maombi kwa Mungu!

Kila mara tunaposali Yesu daima yupo pamoja nasi na kwa ajili yetu, anatutangulia kwa maana daima yuko mstari wa mbele na ni kiranja mkuu.Ni tafakari ya Papa Francisko,Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Ukumbi wa Paulo VI Vatican amesema katika sala ya Yesu ilifungua mbinguni ili kupeleka kwa Mungu hata wale ambao wanajiona hawastahili na kwa kila hali halisi ya maisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika katekesi ya tarehe 28 Oktoba 2020 ambapo pia Mama Kanisa katika liturujia  ya siku alikuwa anaadhimisha Siku kuu ya Watakatifu Simoni  na Yuda Taddei, Papa Francisko kwa mahujaji na waamini waliounganika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI ameanza kusema  “Katika mchakato wetu wa katekesi kuhusu sala baada ya mchakato wa Agano la Kale, sasa tunafikia Yesu. Hatua yake ya utume kwa umma unaanzia katika Ubatizo kwenye mto  Yordani. Injili zote zinakubaliana  kwa kuonesha umuhimu wa  tukio hilo. Wanasimulia jinsi watu wote walivyokuwa wakiunganika katika sala na kubainisha wazi jinsi mkusanyiko wao wa pamoja  ilivyokuwa wazi wa tabia ya toba  (Mk, 1,5; Mt 3,8). Watu walikuwa wanakwenda kwa Yohane ili kubatizwa na kusamehewa dhambi. Kuna tabia ya toba  na uongufu”.

Yesu yuko mbinguni anasali na sisi tunaposali

Papa Francisko amesema kuwa lazima kuliweka kichwani kuwa Yesu ni mwenye haki na siyo mdhambi. Lakini yeye alipendelea kushuka hadi kufikia sisi wadhambi, na Yeye anasali na sisi, tunaposali, Yeye yuko nasi na  anasali: Yeye yupo pamija nasi kwa sababu yuko mbinguni anasali kwa ajili yetu. Yesu anasali kwa ajili ya watu wake, daima anasali nasi . Kamwe hatusali peke yetu kwa maana daima tuko na Yesu” Papa amesisitiza hilo! Tendo la kwanza la Yesu wakati wa maisha yake ni kushiriki sala ya pamoja na watu, sala ya toba, mahali ambapo wote walikuwa wakijitambua kuwa ni wadhambi. Kwa maana hiyo “lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? (Mt 3,14). Kwa njia hiyo Yesu anasisitiza kuwa tendo lake ni kutii mapenzi ya Baba (Mt 3,15). Hilo ni tendo la mshikamano na hali ya ubinadamu wetu; Yeye anashiriki na wadhambi wa watu wa Mungu. Yeye hakubaki ukingoni mwa mto Yordani, kwa kuonesha utofauti wake na kuwa mbali na watu wasiotiii, lakini  Yeye aliingia kwa miguu yake kwenye maji ya utakaso, amesisitiza Papa Francisko na kwamba anajifanya mdhambi. Huo ndiyo ukuu wa Mungu aliyemtuma Mwanaye akajinyenyekza na kujionesha kama mdhambi.

Njia ya kwenda mbinguni ni ngumu lakini Yesu anaifungua

Yesu siyo Mungu aliye mbali na hawezi kamwe kuwa hivyo. Kujifanya kwake mtu kumeonesha  wazi namna alivyotimilika na kwa upande wa kibinadamu siyo rahisi kufikiria hilo. Na kwa maana hiyo Yeye anazindua utume wake. Yesu anajiweka katika mstari wa mbele kwa watu  ambao wanafanya toba, kama vile kuifungua mikono yake kwa njia ya kwamba sisi sote baada yake tuweze kuwa na ujasiri wa kupita. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inaelezea kwamba, huu ni utimilifu wa nyakati. Lakini njia  hiyo na safari ni ngumu, anasema Papa japokuwa Yesu anakwenda akiwa anafungua njia hiyo. “Sala ya mwanadamu ambayo Baba alikuwa anasubiri kutoka kwa  mwanae, anaishirikisha  hatimaye Mwanae mzao wa pekee katika ubinadamu wake, na watu na kwa ajili ya watu (KKK 2599). Yesu anasali na Sisi na  lazima tuzingatie vichwani mwetu na katika roho kwamba Yesu anasali na sisi, Papa Francisko amesisitiza. Siku hiyo katika ukingo wa mto Jordan ulikuwa umejaa ubinadamu wote na matatizo yake wakiwa katika sala. Kulikuwa na watu wadhambi, wale ambao walikuwa wanafikiri  hawawezi kupendwa na Mungu na wale ambao walikuwa hawajaribu hata kwenda mbali na upendo wa hekalu, lakini pia  wale ambao walikuwa hawasali kwa sababu hawakuhisi kustahili. Yesu alikuja kwa ajili ya wote, hata kwa ajili yao, na akaanza kuungana nao, kwa maana hiyo alikuwa kama kiranja mkuu.

Yesu kamwe hakosi mahali pa kukimbilia na makazi ya milele

Papa Francisko amesisitiza kuwa hasa katika Injili ya Luka, inaweka wazi hali ya sala ambayo ilijionesha wakati wa ubatizo wa Yesu kwamba “Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye akabatizwa, naye alipokuwa anaomba, mbingu zilifunguka”(Lk 3,21). Katika kusali Yesu anafungua mlango wa mbingu na ndimi za moto kutoka Roho Mtakatifu zikashuka juu yake. Na kutoka juu ikasikika sauti nzuri isemayo “Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nipendezwaye”(Lk 3,22). Sentesi hii rahisi inafungia ndani mwake ile tunu msingi na kutufanya tuelewa jambo fulani la fumbo la Yesu na moyo wake ambao daima uko kwa baba yake. Katika makona mengi ya maisha na ulimwengu ambao atafika na kuhukumu hata uzoefu mgumu na uchungu ambao atatakikiwa kuubeba, hata ikiwa atafanya uzoefu ambao umewekwa kuegemea kichwa chake (Mt 8,20), na  hata kama karibu naye amezungukwa na chuki na mateso, Yesu kamwe hakosi mahali pa kukimbilia na makazi, anaishi milele katika Baba. Huo ndio ukuu wa pekee wa sala na Yesu. Roho Mtakatifu anachukua nafasi ya utu wake na sauti ya Baba ambaye anasema kupendezwa naye, Mwana ambaye kwa utimilifu anafanana naye. Sala hii ya Yesu ambaye akiwa ukingoni wa mto Yordan ni mtu kweli na atakuwa hivi maisha yake milele, katika pentekoste atageuka kuwa neema ya sala kwa wabatizwa wote katika Kristo. Yeye alipata zawadi hiyo na anatualika kusali kama yeye alivyokuwa anasali.

Yesu anatufanya tuone majeraha ya baba

Kwa maana hiyo ikiwa wakati mwingine wa sala za jioni tuhaisi uchovu na utupu na tunafikiria kuwa maisha yote hayana maana basi ni lazima  ghafla kufikiria  kwamba sala ya Yesu inageuka kuwa yetu. Tutasikia kwa maana hiyo sauti kutoka mbinguni yenye nguvu zaidi  na kupaa  kutoka chini kabisa ndani mwetu, kwa maneno ya upendo yasemayo “ Wewe ni mpendwa wa Mungu, wewe ni mwanangu, wewe ni furaha ya Baba wa Mbinguni.  Papa Francisko ametoa mfano kwamba wengine wanaweza kusema “ mimi siwezi kusali na sijuhi namna ya kufanya, sijisikii na sisitahili… Katika wakati huo sala yako na ya  Yesu ni  yake Mungu. Jikabidhi kwake, kwani Yeye anasali kwa ajili yetu. Katika muda huo ambao mbele ya Baba anasali kwa ajili yetu, ni mwambezi na anatufanya tuone Baba majeraha yake kwa ajili yetu. Sisi sote tunaamini hili na ndiyo jambo kuu. Tutasikia hilo basi ikiwa sisi tunaamini hilo.” Kwa hakika sisi na kwa kila mmoja anaweza kusema hayo maneno ya Baba hata kama tumesukumwa kwenye dhambi zaidi ya kila aina. Yesu hakushuka katika maji ya Jordan kwa ajili yake tu, bali kwa ajili ya wote.  Walikuwa ni Watu wote wa Mungu waliokuwa wanakaribia ziwa Jordan ili kusali, kuomba msamaha, na kubatizwa kwa ajili ya maondoleo ya dhambi.

Yesu alituzawadia utatu ili uchipuke mioyoni mwetu

Ni kama asemavyo mtaalimungu mmoja  kuwa “walikuwa wanakaribia Yordan Roho zao zikiwa tupu na miguu peku(Liturujia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji). Yesu kwa unyenyekevu alikuwa hivyo na ili kusali unyenyekevu unahitajika. Mbingu zilifunguka kama Musa alivyotengenisha maji ya Bahari ya shamu, kwa sababu sisi sote tuweze kukatisha tukiwa nyuma yake. Yesu alituzawadia sala yake mwenyewe, kuwa ni mazungumzo ya upendo na Baba. Alituzawadia kama mbegu ya Utatu na ambayo inataka ichipuke ndani ya mioyo yetu kwa maana hiyo, basi tuipokee zawadi hiyo na zawadi ya sala kwa maana yeye yuk nasi na hatutakosea katu, amehitimisha. Hata hivyo Papa Francisko amerudia kuhimiza juu ya kukaa mbali na watu kama ilivyo kuwa wiki iliyopita kufiatia na sheria na kanuni za kuzuia maambukizi ya covid. Yeye anawakumbuka katika sala na wapo moyoni mwao

28 October 2020, 14:02