Tafuta

2020.10.21 Katekesi ya Papa Francisko 2020.10.21 Katekesi ya Papa Francisko 

Papa Francisko:usisali na kuishi kama vile Mungu na maskini hawapo!

Katika katekesi yake Papa Francisko tarehe 21 Oktoba 2020 amehitimisha tafakari juu tafakari ya Zaburi,katika mzunguko mzima wa sala na kusisitiza kuwa mzaburi anatufundisha kuomba Mungu kwa ajili yetu,lakini pia kwa ajili ya ndugu na ulimwengu wote.Hata hivyo ameelezea taadhari ya maambukizi ya virusi vya corona ambayo inamzuia kutelemka kusalimia watu kama ilivyokuwa kawaida na inamsikitisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika tafakari ya Papa Francisko kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI, Jumatano tarehe 21 Oktoba 2020 amesema  “Tuhitimishe leo katekesi kuhusu sala ya zaburi. Kwanza kabisa tumeona kuwa zaburi mara nyingi zinajionesha katika sura ya uasi  kwa yule ambaye anaishi utafikiri kama Mungu hayupo. Ni mtu bila kuwa na mahali pa kuegemea kutoka juu, bila kuwa na breki katika maneno yake mbele ya macho yaa Mungu na ambaye kwa walimu wa kiroho wanaiita hofu ya Mungu. Kwa sababu hii Mzaburi anawakilisha sala kama hali halisi msingi ya maishi na hofu takatifu ya Mungu, yaani ambayo  inatufanya kuwa binadamu kamili , na ni vikwazo ambavyo vinatuokoa sisi binafsi na kuzuia tusijiweke katika njia ya maisha ambayo yanaweza kuwa ya mraruaji na mchoyo. Sala ni wokovu wa kuwa binadamu halisi.  Kwa kuendelea Papa Francisko amesema hakika kuna hata sala za uongo, sala ambazo zinafanywa tu kwa ajili ya kutaka sifa kutoka kwa wengine.  Kwa yule au wale ambao wanakwenda kwenye misa kwa ajili ya kujionesha tu, na wakati ni wakatoliki au kwa kufanya waonesha mitindo mipya waliyonunua… ili kuonekana picha nzuri katika jamii. Wanakwenda kwenye sala ya uongo, Papa Francisko amesisitiza. Yesu anatoa onyo kwa nguvu kulingana na hiyo (Mt 6,5-6; Lk 9,14). Lakini ikiwa ni roho ya kweli ya sala, ni ile ambayo imejiunda kwa uwazi na ukweli kutoka katika moyo na hivyo inatufanya kutafakari hali halisi kwa macho yake Mungu.

Unaposali kila kitu kinapata uzito wake.  Huo ndiyo mshangao wa sala labda inaanza kwa namna ya ufunyu sana, lakini katika sala jambo hilo linapata nguvu na uzito utafikiri kwamba Mungu anazichukua sala hizo mikono mwake na kuzibadilisha. Huduma mbaya sana ambayo inaweza kufanya kwa Mungu hata kwa mwanadamu ni kusali kwa uchovu, kwa namna ya ukawaida, Papa Francisko amebainisha. Au kusali kama kasuku, yaani bla bla… Hapana. Inabidi kusali kwa moyo. Sala ni kiini cha maisha. Ikiwa ni sala ya kweli hata kaka na dada, wanakuwa watu muhimu. Msemo wa zamani wa wakristo wamonaki, walikuwa wakisali hivi “Heri mmonaki ambaye baada ya Mungu wanakiria kuwa watu wote ni Mungu (EVAGRIO PONTICO, kuhusu sala, n. 123). Kwa sababu hiyo, sala sio dawa ya kupunguza maumivu ya maisha; au, kwa hali yoyote, sala kama hiyo sio ya Kikristo. Badala yake, sala inatia nguvu. Tunaiona wazi katika sala ya “Baba yetu, ambayo Yesu aliwafundisha wanafunzi wake. Ili kujifunza njia hii ya kuomba, Zaburi ni shule nzuri. Tumeona jinsi zaburi hazitumii maneno yaliyosafishwa na mazuri kila wakati, na mara nyingi hubeba makovu ya uwepo. Walakini, maombi haya yote yalitumiwa kwanza katika Hekalu  la Yerusalem na baadaye  katika masinagogi; hata zile za karibu zaidi na za kibinafsi. Hivi ndivyo Katekisimu ya Kanisa Katoliki inavyosema: “maelezo mengi ya sala ya zaburi huzaliwa wakati huo huo katika liturujia, katika Hekalu na moyoni mwa mwanadamu”, (n.2588). Na kwa maana hiyo sala binafsi inachotwa na kumwilishwa kwa watu wa Israeli kabla na ile ya watu wa Kanisa baadaye. Hata zaburi katika nafsi ya kwanza, ambayo huficha mawazo ya karibu na shida za mtu binafsi, ni urithi wa pamoja, hadi kuombewa na kila mtu na kwa kila mtu. Maombi ya Wakristo yana pumzi hiyo, ya mvutano huu wa kiroho ambao unashikilia hekalu na ulimwengu pamoja. Sala inaweza kuanza kwa mwanga hafifu katika kona, lakini baadaye inamalizia mbio zake  kupitia barabara za jiji. Na kinyume chake, pia  inaweza kuchipuka wakati wa kazi za kila siku na kupata utimilifu katika liturujia. Milango ya makanisa sio vizuizi, bali ni utando unaoweza kupenywa, tayari kusikia kilio cha kila mtu.

Katika ya sala ya Zaburi ulimwengu uko wazi kila wakati. Zaburi, kwa mfano, hutoa sauti kwa ahadi ya kimungu ya wokovu kwa walio dhaifu: “Kwa maskini walioonewa na kilio cha maskini, tazama, nitaamka, asema Bwana; Nitawaokoa wale wanaodharauliwa” (zab 12,6). Au inaonya juu ya hatari ya utajiri wa ulimwengu, kwa sababu “mtu katika mafanikio haelewi, yeye ni kama wanyama wanaoangamia” (Zab 48,21), au, tena, zinafungua upeo wa macho kwa Mungu juu ya historia Zaburi 33  : “Bwana hufuta miundo ya mataifa, hufanya mipango ya watu kuwa ya bure. Lakini mpango wa Bwana unadumu milele, na mipango ya moyo wake kwa vizazi vyote. (33,10-11). Kwa kifupi, mahali ambapo yupo Mungu lazima kuna mtu pia. Maandiko Matakatifu ni ya kitabaka. Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda sisi akiwa wa kwanza. Yeye huenda kila wakati mbele yetu. Yeye anatusubiri daima  kwa sababu anatupenda sisi akiwa wa kwanza, anatuangalia sisi akiwa wa kwanza, anatuelewa akiwa wa kwanza. Yeye anatungojea daima. “Mtu akisema, Nampenda Mungu na anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa sababu yeyote asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni”.

Ikiwa unasali rozari nyingi kwa siku, lakini unazungumza juu ya wengine, halafu una chuki ndani, una chuki dhidi ya wengine, huu ni usanii safi, sio ukweli, na sio sawa, Papa Francisko ametoa onyo!  Na hii ndiyo amri tuliyonayo kutoka kwake: “kila mtu ampendaye Mungu lazima ampende pia ndugu yake (1 Yoh 4: 19-21). Maandiko yanaonesha hata kesi ya mtu ambaye, licha ya  kumtafuta Mungu kwa dhati, hafanikiwi kukutana naye; lakini pia anathibitisha kuwa machozi ya maskini hayawezi kamwe kukataliwa, kwa maumivu ya kutokutana na Mungu. Mungu hakubaliani na mtu anayemkana yeye kwani sura yake imewekwa mhuri katika kila mwanadamu. Kuna ukanaji wa Mungu kila siku, ambao unajifanya kuamini Mungu wakati unaweka umbali kwa jirani na unaruhusu kuchukia wengine. Hilo ndilo, chukizo, ni kosa baya zaidi ambalo linaweza kuletwa hekaluni na altareni amesisitiza. Kwa kuhitimisha Papa amasema,sala ya zaburi itusaidie tusiingie katika majaribu ya ukosefu wa kutojali na ambayo ni kusema, kuishi, na labda hata kuomba, kana kwamba Mungu hayupo!

Kabla ya kuanza tafakari ya katekesi yake Papa Francisko ameomba radhi mahujaji wote waliounganika katika Ukumbi wa Papa Paulo VI na kusema “Leo hii tunapaswa kubadilisha mtindo kidogo wa namna ya kufanya katekesi kwa sababu ya virusi vya corona. Ninyi mmetengwa mkiwa bali  pia kwa barakoa na mimi niko mbali na siwezi kufanya kile ambacho nimezoea kufanya, kuwakaribia ninyi kwa sababu kila mara ninapowakaribia ninyi wote mnataka kuja karibu nami na kukusanyika wakati huo ni kupoteza ule umbali, unaotakiwa na kuna hatari ya maambukizi. Ninasikiti sana kufanya hivyo, lakini ni kwa ajili ya usalama wenu. Katika kukaa kwenu mbali basi tutapungina mikono na kusalimiana hivi na kumbukeni kuwa mimi niko karibu nanyi moyoni mwangu”.

21 October 2020, 15:04