Tafuta

2020.10.18 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.10.18 Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Francisko:tulipe kodi na kuwa shuhuda wa Injili

Papa Francisko wakati wa tafakari ya Injili ya Siku ya Dominika kabla ya sala ya Malaika wa Bwana amewahimiza waamini kuwa raia waaminifu na wakati huo huo kushuhudia upendo wa Mungu kwa wanaume na wanawake wa leo hii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Dominika tarehe 18 Oktoba 2020, Papa Francisko kama kawaida yake ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro kusali sala ya Malaika wa Bwana. Akianza tafakari hiyo amesema “Injili ya Dominika  kutoka (Mt 22,15-21) inatuonyesha Yesu akipambana na unafiki wa wapinzani wake. Wao wanampa pongezi nyingi sana mwanzoni, lakini baadaye wanauliza swali la ujanja ili kumweka katika shida na kumdhalilisha mbele ya watu. Wanamuuliza: “Je! Ni halali, au sio, kulipa ushuru kwa Kaisari?” (Mt 22,17) yaani kulipa kodi kwa Kaisari? Papa amesema, na wakati huo, huko Palestina, utawala wa Dola ya Kirumi haukuvumiliwa na unaeleweka kiukweli! Walikuwa wavamizi hasa kwa sababu za kidini, kwa umati wa watu, katika ibada ya mfalme, na pia kama iliyobainishwa na picha yake kwenye sarafu, ilikuwa tusi kwa Mungu wa Israeli”.

Wapinzani wa Yesu wana uhakika kuwa hakuna njia mbadala ya swali lao: ama “ndiyo” au “hapana”. Walikuwa wakingojea, hasa kwa sababu kwa swali hili walikuwa na uhakika wa kumtia Yesu pembeni na kumfanya aingie mtegoni. Lakini Yeye, yaani Yesu, anajua uovu wao na anajiweka huru kutoka kwenye mtego wao. Anawauliza kwa kuwaonesha sarafu yaani pesa ya kulipa kodi, ya mchango na anaichukua mikononi mwake na anauliza picha iliyochapishwa ni ya nani. Wale wanajibu kuwa ni ya Kaisari, ambaye ni mfalme. Kwa njia hiyo Yesu anajibu: “basi mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu”(Mt 22,21).

Katika jibu hili, Yesu anajiweka katika ubishani. Yesu daima yuko juu ya yote. Kwa upande mmoja, anatambua kuwa kodi kwa Kaisari lazima ulipwe na pia kwetu sisi sote, Papa Francisko amesisitiza, “kwani kodi lazima ulipwe, na kwa sababu picha katika sarafu ni yake; lakini zaidi ya yote anakumbuka kuwa kila mtu hubeba ndani yake picha nyingine, na ambayo tunaibeba moyoni, katika roho yaani ile ya Mungu, na kwa njia hiyo ni kwake Yeye, na ni kwake yeye tu, kwamba kila mtu anadaiwa kwa uwepo wake mwenyewe, kwa maisha yake mwenyewe”, Papa amefafanua

Katika hukumu hiyo Yesu anapata si katika mantiki tu ya kutofautisha kati ya hali ya kisiasa na hali ya kidini, lakini yanaibuka maelekezo yaliyo wazi kwa ajili ya utume wa waamini wa nyakati zote, hata leo hii kwa ajili yetu. Kulipa Kodi Papa amesema ni wajibu wa kila  raia kama ilivyo hata sheria za haki za serikali. Wakati huo huo ni lazima kuthibitisha ukuu wa Mungu katika maisha ya binadamu, na katika historia kwa kuheshimu haki ya Mungu kwa chochote kinachomhusu Yeye.

Kufuatia na hiyo Papa Francisko amesema ndiyo unatokeza utume wa Kanisa na kwa wakristo  ya kuzungumza juu ya Mungu na kumshuhudia kwa wanaume na wanawake wa nyakati zao. Kila mmoja wetu kwa nguvu ya ubatizo ameitwa kuwa uwepo hai katika jamii na  kwa kuongozwa na Injili, kwa njia ya  kiini cha uhai wa Roho Mtakatifu. Hii ni katika kujikita kwenye jitihada kwa unyenyekevu na wakati huo huo kwa ujasiri katika kutoa mchango binafsi wa ustaarabu wa upendo, mahali ambamo haki na udugu vinatawala. Kwa kuhitimisha Papa amesema “Maria Mtakatifu atusaidie sisi sote kuutoroka kila unafiki na kuwa raia waaminifu na wenye kujenga. Atusaidie sisi wafuasi wa Kristo katika utume wa kushuhudia kwamba Mungu ndiye kitovu na maana ya maisha.

18 October 2020, 14:17