Tafuta

2020.10.20 Mkutano wa Kimataifa wa sala kwa ajili ya amani. 2020.10.20 Mkutano wa Kimataifa wa sala kwa ajili ya amani. 

Papa Francisko:sisi tunapendelea Mungu wa tamasha.Neno Jiokoe mwenyewe siyo Injili!

Tuombe Mungu msulibiwa neema ya kuungana zaidi na udugu zaidi. Na ikiwa tunashawishiwa kufuata mantiki za ulimwengu,tukumbuke maneno ya Yesu, asemaye “anayetaka kujiokoa maisha yake atapotea, lakini apotezaye maisha yake kwa sababu yangu na Injili ataokoka( Mk 8,35).Ni katika tafakari ya Papa Francisko wakati wa Sala ya Kuombea Amani Kadiri ya Moyo wa Assisi Jumanne tarehe 20 Oktoba 2020,alasiri,katika Kanisa Kuu la Maria,Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni zawadi kusali pamoja. Ninashukuru na kuwasalimia ninyi nyote kwa namna ya pekee Patriaki wa kiekumene, kaka yangu Bartholomew, Askofu Heinrich Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kiinjili nchini Ujerumani na kwa bahati mbaya Askofu Mkuu wa Justin Werlby wa Canterbury hakuweza kufika kwa sababu ya janga. Ndivyo Papa Francisko ameanza tafakari yake wakati wa Sala ya Kuombea Amani Kadiri ya Moyo wa Assisi Jumanne tarehe 20 Oktoba 2020 Alasiri, masaa ya Ulaya. Hii ni sala ambayo imeandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ambayo imewashirikisha waamini wa Madhehebu mbali mbali ya Kikristo katika Kanisa kuu la Mtakatifu Maria wa Aracoeli (Santa Maria in Aracoeli) mjini Roma. Na baada ya sala ya kiekumene Papa Francisko ameungana na viongozi wakuu wa dini mbali mbali duniani kwenda kwenye Uwanja wa manispaa ya Roma “Campidoglio ili “kusali kwa ajili ya kuombea amani ulimwenguni. Akiendelea Papa amesema somo la mateso ya Bwana yaliyosomwa yanaonesha kabla ya kifo cha Yesu na kuzungumza juu ya kishawishi ambacho anakumbana nacho, kuhusu kifo cha msalaba. Wakati anaishi kipindi kigumu cha uchungu na upendo, wengi bila huruma wanaendelea kumsonga dhidi yake kwa kiitikio “jiokoe mwenyewe” (Mk,15,30).

Ni kishawishi cha kiajabu sana ambacho kinasonga wote hata sisi wakristoNi kishawishi cha kufikiri kujikoa binafsi au kukidhi binafsi na kuwa na wazo tu kichwani la matizo  na masuala binafsi, wakati ya wa mengine yote yanayobaki hakuna kinachohesabiwa. Ni hisia za binadamu, lakini zilizo mbali sana na ndiyo ya mwisho zinazochangamotisha Mungu msalabani. Jiokoe mwenyewe. Walisema wakiwa wa kwanza waliokuwa wanapita kwa mbali (Mk 15,29). Hao walikuwa ni watu wa kawaida na ambao walikuwa wanamsikiliza Yesu anazungumza na kutenda miujiza. Na sasa wanasema, “jiokoe mwenyewe, shuka msalabani”. Hawakuwa na huruma bali kutaka miujiza, kumwona anashuka kutoka msalabani. Labda hata sisi wakati mwingine tunapendelea Mungu wa tamasha badala ya yule mwenye huruma, Mungu mwenye nguvu mbele ya macho ya ulimwengu na ambaye anapendekeza nguvu ili kumwondoa kila anayemtakia mabaya. Lakini huyo siyo Mungu bali ni umimi wetu Papa Francisko amesema. Ni mara ngapi tunataka Mungu wa vipimo vyetu, badala ya kugeuka sisi kuwa vipimo vya Mungu Mungu kama sisi, badala ya kugeuka kuwa kama Yeye!  Na ndivyo hivyo badala ya kuabudu Mungu tunataka utamaduni wa umimi. Ni utamaduni ambao unakua na kukuzwa kwa njia ya kutojali wengine. Kwa wapita njia walimwitaji Yesu ili kukidhi haja zao. Lakini kwa kuona anaishia msalabani hawana tena haja naye. Alikuwa mbele ya macho yao, lakini akiwa mbali na moyo wao. Sintofahamu zilikuwa zikiwafanya wawe mbale ya uso wa kweli wa Mungu.

Jiokoe mwenyewe. Katika hatua ya pili wakuu wa makuhani na waandishi wanakuja juu. Hawa walikuwa wale ambao wamemkuhumu Yesu kwa sababu kwao alikuwa anawakilisha hatari. Lakini sisi sote ni wataalam wa kuwekwa wengine kwenye misumari licha ya kujiokoa wenyewe. Kinyume chake Yesu anaacha awambwe msalabani kwa ajili ya kutufundisha tusibebeshe mabaya juu ya wengine. Wakuu wa kidini walikuwa wanamkumbuka kiukweli kwa sababu ya wengine. “Uliwaokoa wengine, huwezi kujiokoa mwenyewe (Mk 15,31). Walikuwa wanamfahamu Yesu, na walikuwa wanakumbuka uponyeshaji aliokuwa ameutenda na kuunganisha yote kwa ukatili wakisisitiza kwamba kuokoa, kusaidia wengine hakuleti maana yoyote; Yeye ambaye alikuwa ameangaikia wengine, alikuwa anapotea mwenyewe! Shtaka ni la kubeza na linachukua maneno ya kidini, kwa kutumia mara mbili neno jiokoe. Lakini Injili ya jiokoe mwenyewe siyo Injili ya Wokovu. Ni Injili iliyo ya uongo zaidi, ambayo inaweka misalaba juu ya wengine. Injili ya kweli kinyume chake inabeba misalaba ya wengine.

Jiokoe mwenyewe. Hatimaye hata wale waliokuwa wamesulibishwa na Yesu wanaungana na hali ya changamoto na Yeye. Jinsi gani ilivyo rahisi kukosoa wengine, kuzungumza dhidi ya wengine, kuona ubaya wa wengine na siyo binafsi. Hadi kufikia kuwatupia makosa kwa walio wadhaifu zaidi na waliobaguliwa! Lakini ni kwa nini wale waliokuwa wamesulibiwa walimkasirikia Yesu? Kwa nini hawakumtoa msalabani. Wanamwambia “jiokoe mwenyewe na sisi! (Lk 23,39). Wanamtafuta Yesu tu kwa ajili ya kusuluhisha shida zao. Lakini Mungu haji mara nyingi kutuokoa na matatizo yetu, ambayo daima yanajiwakilisha, lakini kwa ajili ya kutuokoa na shida za kweli, zile za ukosefu wa upendo. Ndiyo sababu kuna  mabaya binafsi, kijamii, kimataifa na kimazingira. Kujifikiria tu binafsi ndiye baba wa mabaya yote Papa amesisitiza.  Lakini mmoja wa maharamia hao alimtazama Yesu na kumwona upendo wa upole. Na akapata mbingu kwa kuwa alifanya jambo moja tu, la kuondoa umakini binafsi na kumwelekea Yesu, kuondokana na ubinafsi na kumwelekea aliyekuwa naye ubavuni mwake (Lk 23,49), Papa Francisko amesisitiza.

Papa Francisko amesema juu ya Kalvari ilivyotokea duru kubwa kati ya Mungu aliyekuja kutokumboa na mtu ambaye alikuwa anataka kujiokoa mwenyewe; kati ya imani kwa Mungu na utamaduni wa umimi; kati ya mtu ambaye anashtaki na Mungu anayeomba msamaha. Na ukawaida wa ushindi wa Mungu, uhuru wake  ukashuka juu ya ulimwengu. Kutoka katika msalaba, ukashuka msamaha na kuzaliwa upya udugu. “Msalaba unatufanya kuwa ndugu”(Papa BENEDIKTO XVI, Maneno ya kuhitimisha Njia ya Msalaba, 21 marzo 2008). Mikono ya Yesu iliyofunguliwa wazi msalabani, inaonesha mabadiliko kwa sababu Mungu hanyoshei kidole dhidi ya mwingine, bali anamkumbatia kila mmoja. Kwa sababu ni upendo peke yake unazima chuki, upendo peke yake  mwisho unashinda, hadi ukosefu wa haki. Ni upendo peke yake unatengeneza nafasi ya mwingine. Ni upendo peke yake ambao ni njia kamili ya umoja kati yetu.

Tutazame Mungu msulibiwa na kumwomba neema ya kuungana zaidi na udugu zaidi. Na ikiwa tunashawishiwa kufuata mantiki za ulimwengu, tukumbuke maneno ya Yesu, asemaye “ anayetaka kujiokoa maisha yake atayapoteza, lakini apotezaye maisha yake kwa sababu yangu na Injili ataokoka (Mk 8,35). Kile ambacho kwa macho ya mwanadamu ni kupotea ndiyo wokovu wetu. Tujifunze kutoka kwa Bwana, aliyetukomboa kutokana na kujikana yeye mwenyewe(Fil 2,7) ,kujifanya mwingine. Kutoka kwa Mungu hadi kwa mwanadamu, kutoka katika roho ya nyama, na mfalme mtumishi.  Yesu anatualika hata sisi kujifanya wengine na kwenda kukutana na wengine. Kadiri tutakavyokuwa karibu na Bwana Yesu ndivyo tutakuwa wazi na ulimwengu kwa sababu tutahisi uwajibikaji kwa wengine. Na mwingine atakuwa njia ya wokovu binafsi, kila  binadamu, kwa kila historia yake na imani yake. Tuanzie na maskini, ambao wanafanana na Yesu. Askofu Mkuu wa Constantinople, Mtakatifu Yohane Chrysostom, aliandika kuwa “kama pasingekuwapo na maskini, sehemu kubwa ingebomolewa wokovu wetu”(Barua II kwa wakorinti XVII,2). Bwana atusaidie kutembea pamoja katika njia ya udugu, ili kuwa wahudumu waaminifu wa Mungu kweli, Papa Francisko amehitimisha. 

HOTUBA PAPA
20 October 2020, 16:51