Tafuta

Vatican News
2020.10.18 sala ya Malaika wa Bwana 2020.10.18 sala ya Malaika wa Bwana  (Vatican Media)

Papa Francisko:Siku ya kimisionari na shukrani kukombolewa kwa Padre Maccalli!

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana amekumbusha siku ya kimisionari ulimwenguni,ambapo amewaalika wakristo kuwa wafumaji imara wa udugu.Shukrani kukombolewa kwa Padre Maccalli na kuwatia moyo wavuvi 18 walioshikiliwa nchini Libia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, amewakumbusha siku ya kimisionari Ulimwenguni iliyoadhimishwa tarehe 18 Oktoba ambayo inaongozwa na kauli mbiu “Mimi hapa, nitume! Wafumaji wa udugu. Papa akiendelea amesema “ni jinsi gani neno wafumaji lilivyo zuri. Kila Mkristo ameitwa kuwa mfumaji wa undugu. Kwa njia ya pekee ni wamisionari, makuhani, walei, watu waliowekwa wakfu ambao wanapanda Injili katika uwanja mkubwa wa ulimwengu. Tuwaombee na tuwape msaada wetu thabiti”.

Kukombolewa kwa Padre Maccalli

Katika mantiki hiyo, aidha Papa Francisko amependelea kumshukuru Mungu kwa kupata uhuru uliotarajiwa sana wa Padre Pierluigi Maccalli na kuomba waamini wampatie  salam zao kwa kumpigia  makofi kwa sababu alikuwa ametekwa nyara miaka miwili iyopita huko Niger nchini Mali. “Tunafuraha hata kwa sababu pamoja naye walikombolewa hata mateka wengine wawili”, ameongeza, tuendelea kusali kwa ajili ya wamisionari na makatekista, hata wale ambao wanateseka au wanatekwa nyara katika sehemu mbali mbali za ulimwengu”, amesema Papa Francisko.

Kutia moyo wavuvi waliofungwa huko Libia

Papa Francisko akiendelea amependa kutoa neno la kutia moyo na msaada kwa wavuvi ambao wamesimamishwa zaidi ya mwezi mmoja nchini Libia na familia zao. Amewakabidhi kwa Mama Maria nyota ya bahari, ili aweze kuwasaidia kutunza uhai  wa  matumaini ya kuweza kuwakumbatia kwa haraka wapendwa wao. Papa Francisko aidha ameombea mazungumzo yanayoendelea ambayo  yanafanyika kwa kiwango cha kimataifa, ili yawe muhimu kwa mustakabali wa Libia. “Kaka na dada, ni wakati umefika wa kukomesha uhasama wa kila aina na kukuza mazungumzo ambayo huleta amani, utulivu na umoja nchini. Tuombe pamoja kwa ajili ya wavuvi na kwa ajili ya Libia, kwa kimya”. Papa Francisko ameomba.

Heshima kwa picha ya Mama wa miujiza -Peru

Kwa kuhitimisha amewasalimia wote kuanzia kwa waroma, na mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za nchi. Kwa namna ya pekee amewasalimia na kuwabariki kwa upendo jumuiya ya waperu mjini Roma ambao wamekusanyika kwa ajili ya kutoa heshima ya picha ya Mama wa Miujiza. Ameomba wapigiwe makofu jumuiya ya Peru. Amewasalimia hata watu wa kujitolea kutoka Shirika la Italia la Ulinzi wa Wanyama na Uhalali wa sheria.

18 October 2020, 14:20