Tafuta

2020.09.15 Picha ya Bikira Maria wa Rosari huko Pompei 2020.09.15 Picha ya Bikira Maria wa Rosari huko Pompei 

Papa Francisko:Rosari ni silaha inayotulinda dhidi ya mabaya yote na vishawishi.

Mara baada ya katekesi yake,Papa Francisko amesalimia waamini kwa lugha mbambali,ambao amewakumbusha kumbu kumbu ya Bikira Maria wa Rosari.Mama Maria kila wakati katika matokeo anashauri kusali Rosari,hasa mbele ya hatari zinazokabili ulimwengu.Rosari ni silaha dhidi ya mabaya na vishawishi.Papa amehimiza kusali rosari na daima kuwa nayo mikononi au mifukoni.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya katekesi yake, Jumatano, tarehe 7 Oktoba 2020, Papa Francisko amewasalimia waamini kwa lugha mbambali, ambao kwa upand ewa Wapolond amesema "leo tunaadhimisha kumbukumbu ya Bikira Maria wa Rosari. Mama Maria kila wakati katika matokeo anashauri kusali Rosari, hasa mbele ya hatari zinazokabili ulimwengu. Hata leo hii katika kipindi cha janga la corona, ni lazima kubaki na rosari mikononi na kusali kwa ajili yetu, kwa ajili ya wapendwa wetu  na kwa ajili ya watu wote".  Papa amewakabidhi wote chini ya ulinzi wa Malkia wa Rosari na kwa moyo  wote amewabariki.

Kwa upande wa lugha ya Kijerumani, kwa namna ya pekee amewageukia vijana kutoka Uswiss ambao wanashiriki 'Wiki ya  ufahamu' kuhusu Kikosi cha Ulinzi cha Kipapa kutoka Uswiss. “Leo ni kumbukumbu ya Bikira Maria wa Rosari inayotukumbusha umuhimu wa sala ya kutafakari. Kwa kujikita katika tafakari ya wokovu inatuonesha daima na zaidi uso wa upendo wa Mungu mwenyewe  ambaye tumeitwa kuendelea kumtafakari katika umilele". Papa ameongeza kusema " Mama Maria awe kiongozi salama katika safari ya kuelekea kwa Bwana”.

Papa Francisko vile vile katika  salam hizo hata kwa  waamini wanaozungumza lugha ya kiarabu, ameendelea kujikita na mada hiii kuhusu  siku ya Mama Maria wa Rosari na kuwaalika kasali  rosari lakini pia kutembea nayo daima mikononi mwao au katika mifukoni mwao. "Kusali Rosari amekazia,  ni sala nzuri sana ambayo tunaweza kumzawadia Bikira Maria. Ni kutafakari juu ya hatua za maisha ya Yesu Mwokozi akiwa na Mama yake Maria na ambayo ni silaha inayotulinda na mabaya yote na vishawishi", amehitimisha wa kuwabariki wote.

 

07 October 2020, 14:30