Tafuta

2020.10.07 'Papa wangu' ni Gazeti la Kispanyola ambapo kuna mahojiano ya Papa Francisko 2020.10.07 'Papa wangu' ni Gazeti la Kispanyola ambapo kuna mahojiano ya Papa Francisko 

Papa Francisko:Roho ya udugu inaweza kutufanya tuondokane na janga tukiwa bora!

Katika mahojiano yaliyofanywa na Mkurugenza wa gazet la “Papa wangu” toleo la kispanyola,Mwandishi Carmen Magallon,anaelezea kuwa Papa anaalika wote katika kipindi cha janga kufikiria si kwa ajili ya wakati uliopo bali kwa kizazi kijacho cha vijana."Ni lazima kubeba uzito wa wakati ujao na kuandaa ardhi ili wengine wapate kufanya kazi.",anasisitiza Papa.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Hatupaswi kufikiria wakati uliopo bali wa kizazi kijacho. Ndiyo ufunguo wa mada msingi wa maisha wakati wa janga na hata mapendekezo kwa ajili ya kishinda kipindi hiki cha mgogoro kwa mujibu wa mahojiano yaliyofanywa kwa Papa na mkurugenzi wa gazeti la ‘Papa wangu’, toleo la kispanyola. Janga liko linabadilisha ulimwengu na kuongezeka kwa  mgogoro anasema Papa. Haiwezekani kutoka katika hali hii kwa namna ile ile. Tuondane humo tukiwa bora zaidi au vibaya zaidi. Lakini namna ambayo tunaweza kuondoka vema inategemea na uamuzi tunaouchukua wakati huu wa mgogoro anasisitiza Papa.

Papa Francisko anauliza maswali muhimu. Itakuwa mtindo upi ambao  tutawaaachia kizazi endelevu? Kwa mujibu wake hili ni kutaka kuonesha namna ya kufikiria kwamba tu sisi binafsi au wakati wetu uliopo. Badala yake ni kutazama wakati ujao katika matarajio ya ubinadamu unaotamani kubaki katika wakati kama sehemu ya uubaji. Lazima kubeba uzito wa wakati ujao, kuandaa ardhi ili wengine waweze kufanya kazi. Huo ndiyo utamaduni ambao lazima kuufanyia kazi katika mgogoro wa janga, Papa Francisko amesisitiza.

Jinsi  gani ya kujibu uchungu uliosababaishwa na janga? Kwa mujibu wa Papa anakumbuka awali ya yote ile ishara ndogo au kubwa za watu wengi katika ulimwengu ambazo wametimiza kwa ajili ya kusaidia wenzao. Lazima kujibu kwa namna hiyo uchungu huo anashauri kwa kutafuta namna ya kuwa karibu nao.  Ni kipindi cha ukimya cha ukaribu na cha kuwajibika na kubaki na muungano. Watakatifu wa mlango wa jirani ni wengi, anaeleza Papa akikumbuka watu wote mabo wamejikita katika kutoa huduma kwa yule ambaye alikuwa anamahitaji zaidi. Watu hao hawakutaka kukimbia, bali kukabiliana na matatizo na walitafuta suluhisho katika matendo yao. Papa Francisko amekumbuka zaidi jitihada ambazo kwa ajili ya maisha hazihusiani na mada ya afya. Kwa maana hiyo anashauri kujitahidi kusaidia hata wale ambao wamebaguliwa na mfumo, kwa wale ambao hawana kazi.

Tupo mbele ya changamoto kubwa ya kijamii anasema Papa. Utamaduni wa ubaguzi, umejikita ndani ya namna ya kufanya uhusiano. Kwa maana hiyo haiwezekani kufuata mitindo hiyo ya kiuchumi ambavyo haina usawa kati ya mambo mengi msingi. Janga kwa ujumla amesema limetufanya kuona jinsi tulivyozoe kuona hali hizo za ubaguzi. Ubagi wa wazee, ubaguzi wa maskini, ubaguzi wa watoto na wanaozaliwa. Kila maisha yanastahili kulindwa na kuheshimiwa, amesema Papa. Kwa mujibu wa Papa anaongeza kusema kuwa sisi sote tunaalikwa kukabiliana kwa ujasiri utumaduni wa kibaguzi. Utamaduni ambao unahatarisha kila mara. Dhidi ya utumaduni wa kibaguzi lazima kuupinga kwa njia ya mitindo mingine ya kuishi. Utamaduni wa ukarimu, wa kupokea, wa ukaribu na udugu. Leo hii zaidi ya hapo awali tunaomba kuwa na roho ya kidugu, ya kwenda kukutana na mwingine hasa aliye mdhaifu zaidi na aliye athirika zaidi wa kuweza kumtunza.

Swali ambao aliulizwa na mwandishi wa Gazeti hili la ‘Papa wangu’ linahusu hasa wakati ule maalum wa sala katika kipinndi cha janga, iliyoongozwa na Papa Francisko. Papa anakumbuka jinsi ambavyo mwanzoni alikuwa anaogopa kuteleza na kuanguka kwenye ngazi. “Moyo wangu ulikuwa unafikiria watu wa Mungu ambao walikuwa wanateseka na ubinadamu ambao ulikuwa ukabiliwa na mgogoro wa janga la virusi na ndivyo nilifaya uzoefu wa siku hiyo ya terehe 27 Machi”. Ilikuwa kama kuzungumza na kivuli. Kwa kuwakosa kimwili na watu nilisaidiwa na simu pamoja na barua”. Mwishowe, Papa anathibitisha kuwa hakuna kichocheo cha kutoka kwenye mgogoro. Lakini tutapata njia ya kubadilisha dhana ya uchum, hasa “ sasa tuanzie na wapembezoni.  “Nimezungumzia juu ya pembezoni, lakini lazima pia tujumuishe nyumba ya pamoja ambayo ni ulimwengu, utunzaji wa ulimwengu”.

Udugu kama unavyokumbushwa na Waraka ambao umetangazwa “Fratelli tutti ni moja ya funguo za kujenga wakati ujao. Kwa kugusia juu ya usambazaji wa chanjo dhidi ya virusi vya corona, unasisitiza mwisho kuwa  haiwezi kumilikiwa na nchi, na maabara ambayo kikundi cha serikali na washirika wake walioigundua kwa kusudi hili. Chanjo ni urithi wa ubinadamu, wa wanadamu wote, ni wa ulimwengu wote”. “Kwa sababu afya ya watu wetu, kama janga linalotufundisha, ni urithi wa pamoja, ni wa faida ya wote”. Papa anakumbusha kuwa, ndiyo kigezo.

Akijibu swali kuhusiana na wimbi la wahamiaji Papa anasisitiza kuwa ikiwa hatushughulikii na kuwasaidia wahamiaji tunapoteza sehemu kubwa ya ubinadamu, wa utamaduni ambao wanauwakilisha. Wakati wa kipinid cha karantini wahamiaji wengi wamejikita kufanya kazi katika mashamba na kwa kutunza usafi wa mji na wamejikita katika huduma mbali mbali. Ni uchungu sana kuona kwamba hawatambuliwi na kuthamaniwa, Papa amesema kwa masikitiko.  Vivelevie anasahuri Papa kutafakari kwa kina  kuhusu sababu za uhamiaji kama vele kesi ya Lebanon na Siria. Ni familia nzima ambazo zinakimbia vita ambavyo havijulikani. Je nchi zetu kweli zinaweza kubaki bila kujali mbele ya maumivu ya hali hii? Anauliza swali.  

Kati ya mada nyingi pia kwenye mahojiano ni yale ya kanisa maskini. Kuna makuhani, walei, watawa kike, maaskofu, anaelezea Papa, ambao wamejitoa sana kufikia lengo hili. Kuna mifano mizuri ambayo inaongoza njia hii. Tumaini lake ni jibu kwa wanadamu wote. Ubinadamu anauwezo wa kujibu, hasa katika sehemu za pembezoni mwa maisha na ikiwa umepangwa. Kwa kutoa mfano amesemea “Ninapenda kufikiria roho ya watu, ya wale wa kiroho ambao inawaruhusu kuendelea mbele kila wakati.” Papa akikumbuka watu walioteswa , kama Yazidi na Rohingya, anasisitiza kwamba lazima kwenda  kwa watu ambao wanateseka. Ikiwa binadamu hawataweza kuwajibika ina maana kuwa katika haki hii hakuna tumaini. Katika muktadha wa maadhimisho ya miaka 500 ya kuongoka kwa mtakatifu Iginatius wa Loyola Papa Francisko anaelezea shauku yake ya kutaka kwenda Manresa, nchini Uhispania mahali alipoanzia mchakato wa safari ya uongofu wake. “Ninaamini kwamba uongofu wa Mtakatifu Ignatius pia ni mkutano wa moyo na unaweza kutualika kutafakari juu ya uongofu wetu wa kibinafsi, kuomba zawadi ya uongofu wa  kupenda na kutumikia zaidi kwa mtindo wa Yesu Kristo”.

08 October 2020, 14:37