Tafuta

2020.10.25 Sala ya Malaika wa Bwana 2020.10.25 Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Francisko:nguzo mbili msingi wa ukristo ni upendo wa Mungu na jirani!

Upendo wa Mungu na jirani ndizo nguzo mbili msingi za kuonesha upendo wa dhati kwa mkristo.Ikiwa ninasema ninampenda Mungu na sipendi jirani yangu,sio halali.Ikiwa mioyo yetu itaendelea kufungwa kwa kaka au dada,ni wazi kuwa mbali na ufuasi kama Yesu anavyoomba.Ni Tafakari ya Papa Francisko tarehe 25 Oktoba wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji katika uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Yesu anaanzisha nguzo mbili msingi kwa waamini wa nyakati zote. Nguzo hizo ni msingi  wa maisha yetu. Kwanza maisha ya maadili na ya kidini hayawezi kupunguzwa kuwa utii wa wasiwasi na wa kulazimishwa, bali lazima uwe na upendo kama kanuni yake. Nguzo ya pili ni kwamba upendo lazima ujitahidi  kwenda pamoja na bila kutenganishwa katika kumwelekea Mungu na jirani. Ndiyo maneno ya tafakari ya Papa Francisko akiongozwa na Injili ya siku kutoka Mtakatifu Matayo 22:34-40, ambapo inasimulia jinsi Yesu alivyo wajibu wale waandishi wa sheria wakimjaribu kujua ni amri ipi ilikuwa msingi katika sheria nzima ya Mungu.

Papa Francisko akiendelea na tafakari yake amesema, Yesu kwa maana hiyo anaweka bayana juu ya uhusiano usio tengenishwa katu na ambao upo kati ya upendo wa Mungu na jirani. Kwa hakika Yesu anajibu “umpende Mungu wako kwa moyo wako wote, roho yako yote na akili yao yote, na kuongezea kuwa amri ya pili ni mpende jirani yako kama unavyojipenda. Na kwa maana hiyo ndizo nguzo mbili msingi kwa waamini wa nyakati zote. Hii ni kama mchezo wa vioo  mahali ambapo upendo kuelekeza kwa Mungu na kwa jirani vinaangazia mmoja na mwingine, na kwamba hakuna kimoja kilichopo bila kuwa na kingine ,na ndiyo maana picha inyaoibuka hapo kwa kuonesha sisi wenyewe jinsi gani tunavyopaswa kuishi kwa dhati yaani kuwa wakristo,Papa anafafanua.

Yesu anahitimisha jibu lake kwa maneno haya: “Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii”. Hii ina maana kwamba amri zote ambazo Bwana alitoa kwa watu wake lazima ziwekwe katika uhusiano na upendo wa Mungu na jirani. Kiukweli Papa amethibitisha, amri zote zinasaidia kuelezea aina mbili za upendo usiogawanyika. “Upendo wa Mungu ujifafanua zaidi ya yote katika sala na kwa namna ya pekee kuabudu, ambapo sisi mara nyingi tunadharau sana” amesema Papa. Upendo kwa jirani,na ambao unaitwaupendo kidugu ni kwa ajili ya ukaribu, wa kusikiliza, kishirikishana na kumtunza mwingine!

Papa Francisko akitoa mfano amesema "mara nyingi tunaacha kumsaidia mwingine kwa sababu ni msumbufu au ananipotezea muda",   kiongezea amesema “wakati mwingine hatujali kusikiliza  na hatuna muda wa kutoa faraja kwa wenye wenye shida  lakini tunao muda mwingi wa kupoteza kupiga gumzo, kwa maana hiyo  hapo ndipo unaonekana muungano wa amri hizo".

Kuwa na muungano na Mungu ndiy zawadi inayotakiwa kuombwa kila siku, kwa njia hiyo ni ahadi binafsi ili maisha yetu yasiruhusu kamwe hali hiyo na zaidi katika mantiki ya ulimwengu ili hatimaye kuweza kuelekeza katika mahitaji ya ndugu. Uthibitisho wa safari yetu ya uongofu na utakatifu daima uko katika upendo wa jirani. Ikiwa ninasema ninampenda Mungu na sipendi jirani yangu, hii sio halali. Ikiwa tutaendelea kuwafungia mioyo yetu kaka au dada ni wazi kuwa  tutaendelea  kuwa mbali na ufuasi  kama Yesu anavyoomba". Papa Francisko amethibitisha.

25 October 2020, 15:23