Tafuta

2020.10.23  VITA KATIKA ULIMWENGU 2020.10.23 VITA KATIKA ULIMWENGU 

Papa Francisko:Mkataba wa UN,ni kumbukumbu ya haki na amani

Miaka 75 baada ya kuanza kutumika Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa,Papa Francisko amerudia kusema kuwa vita lazima viepukwe kwa kuhakikisha utawala wa sheria na kutafuta mazungumzo na usuluhishi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Ikiwa tunataka maendeleo fungamani ya binadamu kwa ajili ya wote, tunatakiwa kuepuka vita kwa kuhakikisha utawala wa sheria na kukimbilia mazungumzo na usuluhishi. Mkataba wa Umoja wa mataifa inaobainisha kwa uwazi na ukweli ndiyo msingi wa haki na amani. Ni katika ujumbe wa Papa Franciso kwenye mitandao ya kijamii katika   siku ambayo Umoja wa Mataifa unatimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 24 Oktoba 1945, mara tu baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, ukiwa na nchi wanachama 51. Leo hii, Umoja wa Mataifa unahesabu jumla ya nchi wanachama 193.

Hata hivyo hivi karibuni Papa Francisko alikuwa ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa Umoja wa Mataifa UN katika fursa ya ya mkutao wao kwenye Juma lao kuu, wakiwa wanaadhimisha 75. Papa alisema miaka 75 ya Umoja wa Mataifa ni fursa ya kuonesha shauku ya Vatica kuwa Shirika hili ni ishara ya kweli na chombo cha umoja kati ya Mataida na huduma ya familia yote ya binadamu. Kwa sasa ulimwengu wetu umepata pigo na janga la Covid-19, ambalo limepelekea kupotea kwa maisha ya wengi. Mgogoro huu uko unaleta mabadiliko katika mtindo wetu wa maisha, kuongezeka kwa mijadala ya mifumo yetu ya kiuchumu, kiafya na kijamii wakati huo huo kuonesha udhaifu wetu kama viumbe. https://www.vaticannews.va/sw/pope/news/2020-09/papa-kwa-un-mgogoro-wa-janga-ni-fursa-kujenga-jamii-ya-kidugu.html

24 October 2020, 13:00