Tafuta

Mafundisho jamii ya Kanisa yanakubaliana na maono ya wawekezaji kutarajia malipo ya haki kutoka kwa rasilimali zinazopatikana na  kuzielekeza kwa ufadhili wa mipango inayolenga kuhamasisha jamii na kwa pamoja. Mafundisho jamii ya Kanisa yanakubaliana na maono ya wawekezaji kutarajia malipo ya haki kutoka kwa rasilimali zinazopatikana na kuzielekeza kwa ufadhili wa mipango inayolenga kuhamasisha jamii na kwa pamoja.  

Papa Francisko:Faida inayosahau binadamu inamfanya mtu kuwa mtumwa!

Mafundisho jamii ya Kanisa yanakubaliana na maono ambayo wawekezaji kadhaa wanatarajia malipo ya haki kutokana na rasilimali zinazopatikana na baadaye kuzielekeza kwa ufadhili wa mipango inayolenga kukuza jamii na wema wa pamoja.Ni maneno ya Papa Francisko,Jumatatu tarehe 5 Oktoba 2020 alipokutana na Wakuu na Wafanyakazi wa Taasisi ya Benki ya kuwekeza na kutoa mikopo nchini Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Papa Francisko tarehe Jumatatu tarehe 5 Oktoba 2020 amekutana na Wakuu na Wafanyakazi wa Taasisi ya Benki ya kuwekeza na kutoa mikopo. Amewakaribisha na kumshukuru Mwenyekiti na uwakilishi wa maafisa wakuu watendaji kwa maneno yake mazuri ya utangulizi. Mkutano huo unafanyika katika fursa ya kumbukizi la miaka 100 tangu kuzaliwa kwa taasisi yao. Ilianzishwa kwa jina la 'Cassa Piemontese' kufuatia na  muungano wa kisiasa wa Taifa, jina likabadilishwa kuwa Cassa Depositi e Presisiti, Yaani Banki ya kuwekeza na kutoa mikopo. Tangu wakati huo kazi ya taasisi yao imejikita katika uhusiano endelevu na mahitaji ya Nchi, kwa wenye shida ya mara kwa mara ya kuwekeza, kisasa, msaada kwa serikali za mitaa, msaada kwa mafunzo ya kitaalam na tija za uzalishaji.

Msimamo huo wa maendeleo, hata leo bado unawataka wae na ukarimu wa jitihada, amesema Papa. Tufikirie changamoto zilizotokea katika nyanja ya kijamii na kiuchumi kufuatia na janga la corona ambalo hadi sasa linaendelea. Tufikirie matukio ya kuanguka sana kwa uchumi na ulivyo udhaifu wa baadhi ya mitindo ya uzalishaji, ambayo inahitaji upyaisho au mabadiliko kabisa. Tufikirie kuingilia kati kwa namna ya kununua na kuuza bidha katika hatari ya kubadilishana soko katika mikono halisi ya  walio wachache kwa mantiki ya ulimwengu. Haya yanajitokeza katika maeneo mahalia na taaluma mahali, kama ililvyo hata hali halisi ya Italia na Ulaya, Papa Francisko amebainisha.

Mafundisho jamii ya Kanisa yanakubaliana na maono ambayo wawekezaji kadhaa wanatarajia malipo ya haki kutoka kwa rasilimali zinazopatikana na baadaye kuzielekeza kwa ufadhili wa mipango inayolenga kuhamasisha jamii na kwa pamoja. Wazo la kikristo hata hivyo Papa amesema siyo kinyume cha misingi ya matarajio  ya faida. Badala yake ni kinyume na ile ya kutafuta faida kwa gharama zote ambayo inamsahau binadamu na kumfanya awe mtumwa,na kuangukia kuwa kama kitu kati ya vitu vingi katika mchakato huo.

Usimamizi wa biashara daima unahitaji mwenendo wa haki na wazi kutoka kwa kila mtu, ambaye haianguikii katika  ufisadi. Katika shughuli za uwajibikaji binafsi ni lazima kujua namna ya kutofautisha wema na ubaya, ameshauri Papa Francisko. Kwa hakika hata katika uwanja wa uchumi na fedha, nia sahihi, uwazi na utaftaji wa matokeo mazuri ni sawa sawa na haupaswi kamwe kutenganishwa. Ni suala la kutambua na kwa ujasiri kufuata hatua za vitendo ambavyo nia  yake ni  heshima na kweli ya kuhamasisha mwanadamu na kwa  jamii.

Katika kazi yao amesema Papa Francisko, wanaitwa kusimamia siku kwa siku, umakini mkubwa na kuwa na  uhusiano na hali halisi ambazo zinakugeukia kuwa msaada. Taasisi kama yao inaweza kushuhudia kwa dhati na ujasiri mshikamano, kwa kupendelea kuzinduliwa kwa uchumi halisi, kama nguvu ya maendeleo ya watu, familia na jamii nzima. Pia kwa njia hii inawezekana kuongozana safari  taratibu ya taifa na kulitumikia taifa kwa ajili ya faida ya wote, kwa juhudi na kuzidisha kuifanya ipatikane mali zaidi katika ulimwengu huu.(Taz. waraka Evangelii gaudium, 203).

Hayo ndiyo yalikuwa matashi mema ya Papa Francisko ambayo amefafanua katika tukio la kumbukumbu yao, akiwahimiza waendelee na hatua yao kwa ukarimu. Msaada wa Roho Mtakatifu uwasindikize na kuwafanya wawe  wajenzi wa haki na amani. Wao kama wawalikishi wa ‘Cassa Depositi e Prestiti’ yaani Benki ya uwekezaji na mikopo amewakikishia kuwakumbuka katika sala zao na amewapatia baraka ya kitume huku akiwaomba wamkumbuke katika sala zao.

05 October 2020, 13:45