Tafuta

2020.10.08 Kamati ya Watalaam wa Baraza la Ulaya la Moneyval 2020.10.08 Kamati ya Watalaam wa Baraza la Ulaya la Moneyval 

Papa Francisko:Fedha zihudumie binadamu hasa waliodhaifu zaidi!

Katika hotuba aliyoitoa kwa wataalam wa Kamati ya Baraza la Ulaya(Moneyval),ambao wamefika Vatican katika tathmini ya mara kwa mara ya hatua dhidi ya utapeli wa fedha na ufadhili wa ugaidi,Papa Francisko amekumbusha hitaji la fedha zilizo safi ambazo zinahudumia wanadamu,kwa namna ya pekee kwa waliodhaifu zaidi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko tarehe 8 Oktoba 2020 amekutana ma Kamati ya wataalam wa  Baraza la ushauri la Ulaya (Moneyval) ambao wamefika mjini Vatican kwa ajili ya kutathimini hatua za uthibiti dhidi ya utapeli na ufisadi na fedha na ufadhili wa ugaidi. Amemshukuru Rais wa Mamlaka ya Habari za kifedha kwa ajili ya maneno yake. Kazi yao ambayo inajihusisha na uhusiano huo mara mbili kwa lengo hilo ndiyo amethibitisha Papa kuwa iko moyoni mwake. Kiukweli shughuli hiyo inajihusisha katika kulinda maisha na amani ya kuishi binadamu katika ardhi, na kwa fedha ambazo hazikandamizi walio wadhaifu zaidi na wenye kuhitaji, amesisitiza Papa.

Papa Francisko akiendelea na hotuba hiyo amesema kama alivyoandika kwenye Wosia wa Kitume wa Evangelii gaudium anaamini kuwa ni lazima kufikiria kwa upya uhusiano wetu na fedha (taz Evangelii gaudium n.55). Kiukweli, katika visa vingine inaonekana kuwa suala la pesa linatawala mwanadamu. Katika kutaka kulimbikiza utajiri, hakuna anayetazama mahali zinapotokea, shughuli zake au labda sio halali na mahali zinapotokea na kwa mantiki ya unyonyaji ambao unaweza kutawala. Kwa namna hiyo inatokea kuwa baadhi ya mantiki zinagusa fedha na kuchafua mikono kwa damu yaani damu ya ndugu. Na bado inaweza kutokea kwamba rasilimali za kifedha zinatengwa kutokana na ugaidi, zinadhitisha wale mwenye nguvu zaidi na kutoa   dhabihu ya maisha ya ndugu zao kwa kudhibitisha nguvu zao.

Mtakatifu Paulo VI alipendekeza kuwa fedha zinazowekwa kwenye silaha na manunuzi mengine ya kijeshi, zirudishwe kwenye mfuko wa ulimwengu ili kuweza kusaidia walio na mateso zaidi (Waraka wa Populorum progressio,51). Kwa maana hiyo Papa Francisko amebainisha juu ya kurudia wito huo kwa kupendekeza Waraka wa ‘Fratelli tutti’ akiomba kwamba badala ya kuwekeza  katika hofu, juu ya hatari za kinyukilia, kikemia au kibaolojia, wazitumie rasilimali hizo kwa ajili ya kuondoa hatimaye  njaa na kwa ajili ya maendeleo ya nchi zilizo maskini na kwa namna hiyo wakazi wa nchi zao wasiweze  kukimbilia katika kutumia nguvu, au kudangaywa na kulazimaka kuacha Nchi zao kwa kutafuta maisha yenye adhi zaidi. (taz. Fratelli tutti n.262)

Kwa mujibu wa Mafundisho Jamii ya Kanisa Papa Fracisko amesema inaeleza jambo kidogo la kutafakarisha, kwani inasema kulingana na utaratibu wa uchumi na utaratibu wa maadili ungekuwa tofauti sana na mgeni kwa kila mmoja, kwamba wa kwanza ungekuwa hakuna namna ya kuweza kutegemea wa pili (taz Pio XI, waraka wa Quadragesimo anno,190). Lakini kwa kusoma uthibitisho huo katika mwanga wa nyakati za sasa, unabainisha kuwa “kuabudu sanamu ya ndama wa dhahabu wa zamani" (taz Kut 32,1-35), umepata maono mapya bila kuwa na lengo la kweli la kibinadamu (Wosia wa kitume Evangelii gaudium,55). "Kiukweli ubashiri wa kifedha na pesa rahisi kama kusudi la kimsingi linaendelea kuua” (Taz. Waraka Fratelli tutti,168). Sera za kupambana na fedha haramu na kupambana na ugaidi ni nyenzo ya kufuatilia mtiririko wa kifedha, ikiruhusu hatua zichukuliwe pale ambapo shughuli kama hizo zisizo za kawaida au hata za jinai zinapojitokeza.

Yesu aliwafukuza katika hekalu wafanyabiashara (taz Mt 21,12-13; Yh 2,13-17) na alitufundisha kuwa huwezi kutumikia Mungu na utajiri (Mt 6,24). Kiukweli ni kwamba uchumi inapopoteza uso wa mwanadamu, hauwezi kuhudumia mtu badala yake  unahudumia fedha. Huo ndiyo mtindo wa kuabudu miungu kwa  wale ambao wameitwa kutenda katika kupendekeza mpangilio wa  mambo ambayo yanapaswa yaelekezwe kwa ajili ya  faida ya wote na Fedha lazima zisaidie  na siyo kutawala (taz wosia wa Evangelii gaudium, 58; Hati ya Gaudium et spes, 64; Waraka wa Laudato si’,195). Katika kutenda kwa misingi hiyo, Agizo la Vatican limeanzisha hivi karibuni baadhi ya hatua za kuweka uwazi katika usimamaizi wa fedha na kupinga fedha haramu na ufadhili wa kigaidi.

Tarehe 1 Juni iliyopita Papa amesema ametangaza barua ya  Motu Proprio kwa ajili ya kuboresha usimamizi wa rasilimali na kusaidia uwepo wa uwazi, uthibiti na ushindani katika taratibu za ununuzi wa umma katika serikali ya mji wa Vatican na ulazima wa kutoa taarifa katika shughuli za kushukiwa kwa Mamlaka ya Habari na Fedha. Kwa kuhitimisha Papa Francisko amepyaisha shukrani kwa ajili ya huduma yao wanayotenda. Maeneo yao ya shuguli wanayosimami kiukweli inawasukuma kulinda fedha zilizo safi, kwa muktadha wa wafanya bishara  haramu ambao amezuiwa kufikiria katika hekalu hilo takatifu ambalo niubinadamu, kulingana na mpango wa upendo wa Muumba. Amewatakia kazi shje ana wasisahau kusali kwa ajili yake.

08 October 2020, 14:17