Tafuta

2020.10.23 LAUDATO SI 2020.10.23 LAUDATO SI 

Papa Francisko:Ekolojia fungamani inahitaji uongofu wa kina!

Papa Francisko ametuma ujumbe kwa washiriki wa Mkutano wa ‘EcoOne’ wa Kimataifa wa harakati za kulinda mazingira za Shirika la kitume la Wafokolari ambapo ni matarajio kuwa shughuli ya mkutano wao zilete mchango na kuhamasishwa katika moyo wa watu hasa kuwa na uwajibikaji shirikishi kwa ajili mmoja na mwingine na zaidi ekolokia inahita uongofu wa kinakama watoto wa Mungu ili kupyaisha jitihada za kuwa wasimamizi wa zawadi yake

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko Ijumaa tarehe 23 Oktoba 2020, ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano wa kimataifa uitwao EcoOne wa  harakati za Kiekolojia za Shirika la kitume la Wafokolari ambapo  utakaohitimishwa tarehe 25 Oktoba 2020.  Papa  anawashukuru kwa kianzishwa jambo hilo na uwakilishi wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya watu, kwa kushirikiana ili kuwezesha tukio hilo. Mkutano wao umeongozwa na mada njia mpya kuelekea ekolojia fungamani, baada ya miaka 5 tangu kutangazwa kwa Laudato si, ambapo Papa Francisko amesema unabainisha maono ya uhusiano wa kibinadamu na utunzaji wa mazingira  nyumba yetu ya pamoja kuanzia na mitazamo mbali mbali kama vile maadili, sayansi, jamii na taalimungu.

Papa Francisko  katika ujumbe wake amekumbusha jinsi Chiara Lubich  mwanzilishi wa Shirika la Kitume la Wafokolari, alivyosema kuwa ulimwengu unachukua ndani mwake karama ya umoja, kwa kuiamini kuwa ndiyo matarajio yake ambayo yanaweza kuongoza kazi yao katika utambuzi kuwa kila kitu kinaunganisha pamoja na inahitajika kuwa na wasiwasi kwa ajili ya mazingira yaliyo unganishwa na upendo wa kweli, ili kuweza kuwa binadamu na jitihada zinazoendelea kuwa na mtazamo wa matatizo ya kijamii ( Laudato 91).

Miongoni mwa matatizo kuna dharura mpya na ambayo inajumuisha mambo yote ya  kijamii na kiuchumi na ambayo inapaswa kutafakari ukweli wa jinsi tulivyo kama ubinadamu mmoja na kama  watu  wanaosafiri  katika mwili mmoja wa kibinadamu na kama  ndugu  katika ardhi hii ambayo inatukaribisha sisi sote (Fratelli tutu, 8). Mshikamano kati yetu na ulimwengu unaotuzunguka unahitaji kuwa na utashi thabiti wa maendeleo na vipimo vya dhati ambavyo vinasaidia hadhi ya kila mtu na katika uhusiano wa kibinadamu, wa kifamilia na kikazi na wakati huo huo kufafanua sababu za mifumo ya umaskini na kazi ili kuweza kulinda mazingira asili.

Lazima kufikia ecolojia fungamani na ungofu wa kina kwa ngazi binafsi na kijumuiya. Papa Francsiko amebainisha kwamba wanapoangalia changamoto kubwa tunazotakiwa kukabiliana nazo za hivi sasa, pamoja na mabadiliko ya tabianchi, hitaji la maendeleo endelevu na mchango ambao dini inaweza kuutoa kwa shida ya mazingira, ni muhimu kuvunja hasa zile mantiki za unyonyaji na ubinafsi na kukuza mazoezi ya maisha ya kiasi, rahisi na ya unyenyekevu(Rej Laudato si’, 222-224).

Ni matarajio yake kuwa shughuli ya mkutano wao zilete mchango na kuhamasisha katika moyo wa kaka na dada kuwa na uwajibikaji shirikishi kwa ajili  mmoja na mwingine na kama watoto wa Mungu ili kupyaisha jitihada za kuwa wasimamizi wa zawadi ya Mungu (Mw 2,15).Amehitimishwa ujumbe wake kwa kuwashukuru kwa ajili ya utafiti wao na kwa ajili ya jitihada zao za kushirikiana katika kutafuta njia mpya za kuweza kufikia ekolojia fungamani na kwa ajili ya wema wa familia ya binadamu na uliwenguni na amewabariki.

23 October 2020, 16:00