Tafuta

2020.10.10 Jimbo Kuu la Ravenna -Carvia katika fursa ya Mwaka wa Dante 2020.10.10 Jimbo Kuu la Ravenna -Carvia katika fursa ya Mwaka wa Dante 

Papa Francisko:Hata sisi tunaweza kutajirishwa na uzoefu wa maisha ya Dante!

Papa Francisko akikutana na uwakilishi wa Jimbo kuu la Ravena-Cervia katika fursa ya maadhimisho ya miaka miasaba tangu kifo cha Mshairi na mwandishi wa vitabu mashuhuri Italia,ameshauri kufuata nyayo zake ambazo zinaweza kusaidia kuvuka vizingiti vigumu kwa furaha katika mchakato wa hija ya historia ya maisha.Anawashauri hata vijana kusogelea zaidi kazi yake aliyoiacha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 10 Oktoba 2020 amekutana mjini Vatican na uwakilishi wa Jimbo Kuu la Ravenna-Cervia, Italia wakiwa katika fursa ya ufunguzi wa Miaka 700 tangu kuzaliwa kwa Dante Alighieri, mshairi na  mwandishi  wa vitabu maarufu  nchini Italia na kumshukuru Askofu Mkuu kwa namna ya pekee kwa maneno yake.  Mji wa Ravenna kwa upande wa Dante ulikuwa ni kimbilio, kwanza alikuwa huko Verona na kwa hakika katika mji wao mshahiri huyo alipitia miaka yake ya mwisho na kumpelekea kukamilisha kazi yake. Kwa mujibu wa utamaduni alitunga wimbo wa  mwisho wa ‘Paradiso’ yaani mbinguni akiwa Ravenna.

Papa Francisko akiendelea na hotuba yake amesema, Ravenna alihitimisha kwa njia hiyo safari yake ya mwisho na kuhitimisha kazi yake kwa kuwaachia wengine waige mfano huo. Mshairi Mario Luzi amebainisha wazi thamani ya mwendelezo wake ambo umeangazia thamani yake na ugunduzi bora ambao ni uzoefu wa uhifadhi wa uhamisho. Kwa mujibu wa  Papa Francisko amesema hiyo inatufanya kufikiria haraka Biblia, kuhusu kuchukuliwa  mateka  watu wa Israeli huko Babilonia ambao wanaundwa kwa namna ya kusema kama vile  mwanzo wa maonesho ya kibiblia. Kwa namna inayofanana hata kwa Dante uhamishoni ulikuwa na maana yake, hadi kufikia kuwa ufunguo wa tafsiri si tu ya maisha lakini pia ya safari ya kila mwanaume na wanamke katika historia na zaidi ya historia kwa  “siku ambayo Kanisa kuadhimishwa kuinuliwa kwa Msalaba Mtakatifu”. Papa anasemea Wazo linakwenda katika msalaba wa dhahabu ambao kwa hakika mshairi aliona huko juu kileleni katika anga la blu wakati wa usiku wa nyota miatisa au kwa hiyo, aliyepambwa na kung'aa  kwa Kristo kwa kutumia picha ya Mbingu( taz.Wimbo XIV, 104).

Mwaka 1965 katika fursa ya miaka 700 tangu kuzaliwa kwa Dante, Mtakatifu Paulo VI alitoa zawadi huko Ravenna ya Msalaba wa dhahabu kwa ajili ya kaburi lake, ambao umebaki hadi sasa na wakati huo alisema “bila ishara hiyo ya dini na matumaini”( Hotuba kwa Baraza, tarehe 23 Januari 1966). Msalaba huo katika fursa ya maadhimisho ya miaka hiyo unarudia tena  kung’ara katika eneo amblo linahifahifadhi masalia ya mshairi huyo. Kwa maana hiyoo Papa amesema unaweza kuwa mwaliko wa amatumaini,  yaani matumaini ambayo Dante ni nabii. (Ujumbe wa miaka 750 tangu kuzaliwa kwa Dante alghieri 4. Mei 2015).

Ni matumaini ya Papa Francisko kwamba miaka 700 tangu kifo cha Mshairi huyo kichachue kutazama tena Maandiko yake ambayo yanatambua kwa dhati  hali yetu na kuacha nafasi ya kutafakari juu ya safari yetu ya uongofu, kutoka kwenye machafuko kuwa wenye hekima, kutoka katika dhambi kuwa watakatifu na kutoka kwenye udhaifu na kuwa wenye furaha, kutoka kwa tafakari ya kutisha ya kuzimu hadi ile ya heri  ya mbinguni” (Mt. Paulo VI 7 Desemba 1965). Dante kwa hakika anatualika kwa mara nyingine tena  kutafuta maana ya kupotea na kupumbazwa na michakato yetu ya kibinadamu. Kwa kutolea mfano , Papa amesema inawezekana kuonekana kuwa karne hizi saba zilizopita haziwezi kujazwa tena kati yetu  wanaume na wanawake wa kipindi cha kisasa, na kilichobobea katika ulimwengu, lakini  yeye bado ni mtangazaji wa kushangaza wa msimu wa dhahabu,  wa ustaarabu wa Ulaya. Na vilevile kuna jambo linatuambia kwamba sivyo ilivyo kwani vijana, kwa mfano  hata waleo hii wanaweza kuiga.

Ikiwa vijana wanao uwezekano wa kukaribia shairi la Dante kwa namna yao kwa upande mmoja, bila shaka wanaweza kukutana na umbali wote wa mwandishi na ulimwengu wake; lakini  bado, kwa upande mwingine, wanaweza kuhisi sauti ya kushangaza. Hii hufanyika hasa pale ambapo fumbo linaacha nafasi ya ishara, ambapo mwanadamu anaonekana wazi na utupu , ambapo shauku ya raia hutetemeka zaidi, au kupendeza kiukweli, uzuri na mwishowe kupendeza kwa Mungu na kuhisi kuvutwa kwake kwa nguvu. Kwa maana hiyo Papa amewaalika kuchukua fursa hiyo kushinda na hata kama alivyokuwa akiwaalika Mtakatifu Paulo VI kwamba  tunaweza kutajirika katika uzoefu wa Dante kwa ajili ya kupitia giza nene la maisha ya dunia hii na kuhitimisha kwa  furaha katika  hija yetu katika historia na kufika hatima ambayo tunaona na kutamani kila mwanadamu.

Ikumbukwe Dante Alighieri, alizaliwa kati ya Mei 21 – Juni 20 mwaka  1265, huko Florence, Italia na alifariki dunia kati ya 13/14 Septemba 1321, huko RavennaItalia. Ni mshairi wa Kiitaliano, mwandishi wa nathari, nadharia ya fasihi, mwanafalsafa wa maadili, na mfikiriaji wa kisiasa. Anajulikana sana kwa shairi kuu la ‘La commedia’, ambalo baadaye liliitwa ‘La divina commedia’ (The Divine Comedy). Dante anajulikana kwa kuanzisha matumizi ya lugha ya kienyeji katika fasihi wakati ambapo mashairi mengi yaliandikwa kwa Kilatino, na kuifanya ieleweke tu kwa wasomaji walioelimika zaidi. Mfano “De vulgari eloquentia yake (On Eloquence in the Vernacular) yake ilikuwa mojawapo ya utunzi wake wa kwanza wa wasomi wa lugha ya kienyeji. Matumizi yake ya lafudhi ya Toscana kwa kazi yake kama vile “The New Life’ (1295) na Divine Comedy ilisaidia kuanzisha lugha ya kisasa ya Kiitaliano, na kuweka mfano kwamba waandishi muhimu wa baadaye wa Italia kama Petrarch na Boccaccio waliweza kufuata. Dante alisaidia sana kuanzisha fasihi ya Italia, na picha zake kuhusu “Kuzimu”, “Utakaso na Mbingu” zilitoa msukumo kwa kiwango kukubwa sana cha kiungo cha nchi za  Magharibi.

10 October 2020, 15:33