Tafuta

2020.10.28 Papa Francisko amvisha Pallio Patriaki mpya Pierbattista Pizzaballa, Patriarki wa Yerusalemu ya kilatini 2020.10.28 Papa Francisko amvisha Pallio Patriaki mpya Pierbattista Pizzaballa, Patriarki wa Yerusalemu ya kilatini 

Papa Francisko amemvisha Pallio Askofu Mkuu Pizzaballa

Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020,Papa Francisko kabla ya kwenda katekesi amemvisha Pallio Patriaki mteule Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta Vatican.Pia Patriaki mteule ameandika barua kwa jimbo lake kuwa siwezi kutoroka 'uzito' wa Neno hilo. Ni ni neno la uvumilivu uliokomaa,wa kungojea kwa uangalifu,wa uaminifu wa kila siku na mzito, sio wa hisia na wa muda mfupi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko amemvalisha Pallio Patriaki wa Yerusalemu, Pierbattista Pizzaballa, katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta, Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 saa 8.30 masaa ya Ulaya kabla ya kwenda katika katekesi yake.  Ilikuwa ni  ibada rahisi, lakini yenye mfano wa hali ya juu, ambapo Papa amesali sala ya baba Yetu pamoja na Patriaki mpya na badaye  akamkabidhi utume  wake, kwa Mama Maria  Mama a Mungu kwa kusali sala ya Salamu Maria. Alikuwapo Padre Flavio Pace, Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki na kati ya wengine hata baadhi ya wawakilishi wa Upatriaki wa Yerusalem ya Kilatini na wanashirika la Ndugu wadogo wafransiskani ambamo ndilo shirika la Askofu Mkuu Pizzaballa.

"Pallio ambalo litanitofautisha katika vipindi vya siku kuu , kwenye utume wangu katikati yenu, anaandika Patriaki, katika salam yake ya kwanza kwa watu wa jimbo lake amesema linatukumbusha kuwa  tulichagua katika ubatizo kuchukua sisi wenyewe nira ya Kristo, uzito na utukufu wa msalaba, ambao ni upendo alioutoa katika kifo chake.  Miaka minne iliyopita, wakati wa kuhitimisha utume wangu kama  msimamizi wa Nchi Takatifu , Baba Mtakatifu ametaka kuniteua kuwa  msimamizi wa kitume wa Upatriaki wa Yerusalemu ya kilatini” anakumbuka katika barua hiyo kwa waamini wake Patriaki mteule. Kwa maana hiyo  anasema nilitaka kutafsiri jina hilo, ambalo bado haliachi kushangaza na kunisumbua, kwa mwanga wa neno kurudi, kama wanafunzi wa Emmaus, hata mimi pia nimehisi kualikwa kurudi Yerusalemu kuanza tena safari, ili gundua tena jumuiya na kuongeza jitihada. Na kwa hivyo ninaombwa wakati huu kubaki. Ni Neno la  uvumilivu uliokomaa, wa kungojea kwa uangalifu, kwa uaminifu wa kila siku na uzito, sio wa hisia na wa muda mfupi. Awali ya yote ni juu ya mwaliko wote kutoka kwa Bwana kwa mitume wake kabla ya Kupaa mbinguni ambao kwao, walikuwa  bado wameshangaa na kufadhaika, wakijaribiwa kwenda  njia zao wenyewe, au kutatua kila kitu mara moja, ili karibu kulazimisha nyakati za Mungu, Yesu akwaambia: “Kaeni mjini mpaka mpate kujazwa nguvu kutoka juu” (Luka 24, 49). Na kwa maana  hiyo mimi pia ninabaki kutembea katikati yenu na nanyi, kwa imani na matumaini”.

Akitoa wito amesema Patriaki “Tunasumbuliwa na shida za zamani na mpya: siasa ni za muda mfupi na haziwezi kuona na ujasiri, maisha ya kijamii yaliyozidi kugawanyika na kupasuka, uchumi ambao unatudhoofisha zaidi na zaidi, na hatimaye janga hili, kwa kuwekewa  ugumu zaidi  na kinyume na maisha tuliyozoea”. Lakini, anaongeza Patriaki mpya “Ninafikiria pia shule zetu katika shida kubwa zaidi, za jamuiya zetu za kikanisa ambazo wakati mwingine ni dhaifu, kwa kifupi shida ni nyingi ndani na nje yetu, ambazo tunazijua tayari. Yote haya, hata hivyo, yanatufundisha kuwa na uchungu lakini pia, na tumaini, kwa matarajio, kwamba hatua za mtu na miondoko lazima iwe nyingine, ikiwa anataka kujiokoa mwenyewe na ulimwengu”.

28 October 2020, 17:23