Tafuta

Papa Francisko na Bwana Sánchez Pérez-Castejón kiongozi wa Uhispania Papa Francisko na Bwana Sánchez Pérez-Castejón kiongozi wa Uhispania 

Papa Francisko akutana na Rais Sanchez wa Uhispania

Katika mkutano na Kiongozi mkuu wa Uhispania Papa ameumbuka kuwa utume wa kisiasa ni kufanya Nchi kuwa na maendeleo mshikamano na kukuza taifaMiongoni mwa mada zilizokuwa katika mkutano huo ni dharuru ya kiafya,mckato wa ushiriksihwaji wa Ulaya na uhamiaji.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Papa Francisko Jumamosi tarehe  24 Oktoba 2020  amekutana na Rais wa Serikali Uhispania Bwana Sánchez Pérez-Castejón, na baadaye kamekutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Ushirikiano wa nchi za nje. Katika mazungumza yao wamegusia masuala ya pamoja kati ya Vatican na Uhispainia na pia juu ya fursa za mazungumzo ya mara kwa mara kati ya Kanisa mahalia na mamlaka  tawala  Hatimaye wameelezea masuala yanayohusu kimataifa kama lile la dharura ya kiafya na mchakato wa ufungamanishwaji wa ulaya na uhamiaji.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msema wa vyombo vya habari amesema kuwa katika mazungumzo yao na kiongozi huyo Papa Franciso amemwakikishia Bwana Sanchez kwamba siasa sio sanaa tu, lakini kwa Wakristo ni tendo la hisani, linalohimiza na mara nyingi hupelekea hata kujitoa maisha ya mtu binafsi. Kiukweli amesisitiza mwanasiasa  ana utume  mgumu sana mikononi mwake, kwani ni katika  kuendeleza nchi, kuimarisha taifa na kuifanya nchi ikue.

Akiendelea, kati ya maendeleo ya taifa, Papa Francisko amesisitiza, wakati mwingine inamaanisha ugumu wa kuelewa na maeneo. Lakini labda jambo gumu zaidi kwa upande wa Papa ni kuifanya  taifa likue kwa sababu ameongeza "humo ndipo tunaingia kwenye uhusiano wa uungwana". "Nchi ni jambo ambalo tumepokea kutoka kwa wazee wetu na ambayo lazima tuweze kuwapatia  watoto wetu”. Papa pia amemwambia Sanchez kwamba ni jambo la kusikitisha sana wakati itikadi zinachukua hatima ya taifa. Hatimaye, Papa Francisko amesisitiza kuwa siasa ni huduma na kwamba lengo lake  kama huduma na ambalo utume wake ni moja ya mtindo uliopokee wa juu kabisa wa hisani.

24 October 2020, 12:50