Tafuta

2020.10.25 Papa atangaza majina ya makardinali wapya wateule 13  2020.10.25 Papa atangaza majina ya makardinali wapya wateule 13  

Papa atangaza Majina ya Makardinali wapya 13 Wateule

Papa Francisko,mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana ametangaza majina ya Makadinali wateule wapya 13 ,kutoka mabara tofauti ili kuweza kumsaidia katika shughuli zake za Utume wa Kanisa.

VATICAN

Papa Francisko Dominika tarehe 25 Oktoba 2020 mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, amewatangazia waamini na mahujaji wote waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro majina ya Makardinali wapya wateule 13 kutoka mabara tofauti ambao watasimikwa rasmi katika kikao cha Baraza la Makardinali cha tarehe 28 Novemba 2020, katika mkesha wa Dominika ya kwanza ya Majilio. Makardinali 9 karibu hawajafikia miaka 80 na wanayo haki ya uchaguzi wa Papa wa wakati ujao, kuna hata msimamizi wa Konventi ya Assisi, Padre Mauro Gambetti pamoja na Muhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa, Padre R. Cantalamessa (OFMkap).

Majina ya Makardinali wapya wateule 13 ni:

Mons. Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu;

Mons.Marcello Semeraro, Rais wa Baraza la mchakato wa kuwatangaza watakatifu;

Mons. Antoine Kambanda, Askofu Mkuu wa  Kigali (Rwanda);

Mons. Wilton Gregory, Askofu Mkuu Washington(Marekani)

Mons. José Advincula, Askofu Mkuu wa Capiz,(UFilippine);

Mons. Celestino Aós Braco, Askofu Mkuu wa Santiago ya Santiago ya Cile;(Amerika ya Kusini)

Mons. Cornelius Sim, Askuf wa  Puzia ya  Numidia na Msimamizi wa Kitume wa Brunei, Kuala Lumpur;(Asia)

Mons. Augusto Paolo Lojudice, Askofu Mkuu wa Siena-Colle Val d’Elsa-Montalcino (Italia);

Fra Mauro Gambetti, Mfransikani wa Kikonventuali, na Msimamizi wa Jumuiya ya Wafransiskani huko Assisi.

Katika orodha mpya hiyo pia kuna majina mengine 5 ya Makardinali wateule ambao ni Askofu na Askofu  Mkuu na wengine watakaojiunga na Baraza la Makardinali hao.

Papa amesema ni:

Mons. Felipe Arizmendi Esquivel, Askofu mstaafu wa Mtakatifu Cristóbal de las Casas(Mexico);

Mons. Silvano M. Tomasi, Askofu Mkuu wa Aslo, na Balozi wa Kitume;

Fra Raniero Cantalamessa, Mkapuchini, na Mhubiri Mkuu wa Nyumba ya Kipapa;

Mons. Enrico Feroci, Paroko wa Madhabahu ya Bikira Maria wa Upendo wa Mungu(Castel del Leva),Italia.

Na hatimaye Papa Francisko ameomba waamini wote ili kuwaombea Makardinali wapya wateule waweze kuthibitisha wito wao kwa Kristo na kuweza kumsaidia katika utume wake kama Askofu wa Roma  na kwa ulimwengu mzima, kwa ajili ya wema wa Watu watakatifu na waamini wa Mungu.

25 October 2020, 13:37