Tafuta

2019.09.04  Padre Luigi Maccalli - Niger 2019.09.04 Padre Luigi Maccalli - Niger  

Padre Maccalli anatoa shukrani kwa Papa na Radio Vatican!

Shukrani za dhati kwa Papa na Kanisa lote zimetolewa na Mmisionari wa Italia aliyekuwa ametekwa nyara huko Niger miaka miwili iliyopita na kukombolewa tarehe 8 Oktoba 2020 nchini Mali.Ameeleza hayo akihojiwa na Vatican News na kusema wamisionari wanashiriki mateso na vurugu lakini wanatoa msamaha na ndiyo amefanya kwa wale waliokuwa wamefunga minyororo na kushika silaha mikononi mwao kwani hawakujua wanafanya nini.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Ni maneno ya dhati ya shukrani yaliyotolewa na Mmisionari wa Italia alieyekuwa ametekwa nyara huko Niger miaka miwili iliyopita na kukombolewa tarehe 8 Oktoba 2020 nchini Mali. Papa Francisko amependelea kumsalimia Padre huyo Maccalli wakati wa sala ya Malaika wa Bwana, katika Siku ya Kimisionari Ulimwenguni. Akiohojwa na Vatican News amesema “Wamisionari wanashiriki mateso na vurugu lakini wanatoa  msamaha na ndiyo nimefanya  kwa wale waliokuwa wamenifunga kwani hawakujua wanafanya nini. "Tumpigie makofu Mpadre Gigi Maccalli", ndivyo Papa Francisko ameomba mara baada ya sala ya malaika wa Bwana kwa washiriki kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican tarehe 18 Oktoba 2020 kwa kuonesha namna hii furaha ya Kanisa baada ya kukombolea kwa mmisionari aliyetekwa nyara huko Niger kunaki tarehe 17 Septemba 2018 na kuachiwa huru huko Mali tarehe 8 Oktoba 2020. Furaha hiyo pia Papa amesema. “Tunafuraha hata kwa sababu pamoja naye walikombolewa hata mateka wengine wawili,  tuendelea kusali kwa ajili ya wamisionari na makatekista, hata wale ambao wanateseka au wanatekwa nyara katika sehemu mbali mbali za ulimwengu”.

Imekuwa ni mshangao na furaha kubwa kwa Padre Maccali ambaye hakutegemea maneno ya Papa Francisko katika siku ambayo Mama Kanisa alikuwa anaadhimisha siku ya Kimisonari na ambayo inakumbisha usukaji wa udugu , ambao wametawanyika katika kila kona ya dunia kupeleka uhai  wa maji  na  utulivu  ya Injili. Mawazo yake yanamwendae hata Sr. Gloria Narváez, mtawa wa Colombia ambaye yumo mikononi mwa wanajiahadi tangu mwaka 2017 na anaomba waendelea kusali kwa ajili yake na kwa ajili ya kukombolewa. Padre Luigi ni mtawa wa Shirika la Wamisionari wa Afrika mwenye asili kutoka Cremona Italia ambaye akihonjwa na Vatican News  amesema bado na hisia ya kuwa katika hatua ya kushuka kutokana na kile kilichomtokea. Amekiri kwamba anahisi kama bado anafukuzwa katika vita kwa sababu nyuma yake ameishi ndani ya chuki na dharau ya watu wenye msimamo mkali, walakini, alihisi faraja ya kusikiliza redio Vatican, iliyomsindikiza katika  gerezani kwa miezi 4 ya mwisho na kuwa msaada katika wakati mgumu zaidi. “ Sikuw na jambo  lingine zadi ya sala" amesema Padre Pierluigi Maccalli.

Kwa upande wa Padre amekiri pia alivyoshangaa kusikiliza maneno ya Papa kwa maana alikuwa pamoja na dada yake wanafuatilia sala ya Malaika wa Bwana. Dada yake alikumbatia na ikawa kipindi cha nguvu sana, na kama ilivyokuwa mikumbatio aliyoipata mara baadaya kutelemka Roma na familia yake, baadaye watu wa eneo lake na sasa Papa na Kanisa lote. Kiukweli Padre Macalli amesema hana maneno mengine zaidi ya kusema asante kwa wote kumkumbuka katika sala na msaada wao, kwani ni nguvu yao na dama alikuwa anategemea kwamba lolote lile lingeweza kutokea, mapema au mbali zaidi, na alikuwa na matumaini ya kuweza kuwakumbatia familia  yake na ambao alikuwa anawahurumia sana kwa mawazo na marafiki wote waliokuwa wanamsindikiza.

Akijibu kuhusu tukio la siku ya kimisionari, linaloongozwa  kwa kauli mbiu ya ufumaji wa udugu  anasema kwake yeye miaka miwili ilikuwa ni migumu kwa maana ya kusubiri aweze kuachiwa huru. Hadi sasa alikuwa bado hawajiweka sawa katika mawazo, hisia kwa maana bado yupo kwenye mawazo lakini uzoefu huo ulikuwa ni wa nguvu. Na kwa wakati huo huo alikuwa anawaza ni jinsi gani alivyoibiwa miaka miwili ya utume wa kimisionari, na kumbe  akagutuka kuwa ni kinyume kwani miaka miwili imekuwa yenye matunda kwa sababu utume wa kimisionari ni utume wa Mungu na kwa maana hiyo upo mikononi mwa Mungu tu. “Kiukweli nimefanya  uzoefu huu ambao ninaufafanua kama mfukuzwaji wa vita, nilihisi chuki na dharau kwenye ngozi yangu, kwa sababu niliwakilisha kwao kama adui wa kupigana. Lakini uzoefu huu wa kifungo uliniruhusu kuhisi katika ushirika na waathirika wote wasio na hatia wa vurugu na vita: sisi wamisionari mara nyingi tunakuwa walengwa rahisi wa kulipiza kisasi, na mateso katika sehemu nyingi za ulimwengu. Sisi ni waathirwa wasio na hatia na mashuhuda kwa ulimwengu wa udugu wa ulimwengu wote”.

Padre Maccalli aidha amesema “Sisi tuko hatarini, ningesema hasa, kwa sababu tukiwa hatuna silaha ya kutumia nguvu na unyanyasaji, tunaamini kwamba Shalom  yaani amani itashinda uovu, tunaamini kwamba haki na amani vitabusiana na ukweli na upendo vitakutana. Hapa, na maisha yetu na, kwa wengine hata kwa kuuawa tukiwa wafiadini, tunavunja vurugu kwa kutoa msamaha kwa wote, kama nilivyoitoa kwa wale ambao waliokuwa wananilinda na kuniweka katika minyororo. Nilijisemea, kimoyo moyo nikitazama hawa vijana waliokuwa na Kalashnikov mikononi: “Hawajui wanachofanya”. Vile vile Padre amesema "Ninaamini na kukiri kabisa, baada ya miaka hii miwili, kwamba sala binafsi na pamoja  ambayo nilisikia na kushuhudia na vikundi vya wamisionari, majimbo ambayo kila tarehe 17 ya kila mwezi walikusanyika kufanya mkesha wa maombi na kuandamana kwa sala pamoja,  ni jambo la lazima kwa kusuka mtandao wa amani na undugu. Na sala yangu, katika eneo lile la mbali la Sahara, ilikuwa nguvu yangu, sikuwa na kitu kingine chochote".

Padre maccalli anayo ya kusisimua kwani amesema "Waliniteka nyara nikiwa katika nguo za kulala, lakini nilitengeneza rozari ya kitambaa ambacho nilikifunga na kusali kila siku, asubuhi na jioni, nikimkabidhi ‘Maria  anayefungua mafundo’. Hapa, nafikiri kuwa  mtandao wa udugu tunausuka kwa pamoja: sisi wamisionari wa mipaka na nyinyi jumuiya ambazo mlitutuma na kutuunga mkono kwa sala, kwa upendo mwingi na kwa hisani." "Niruhusu kusema asante kwa kila mtu, kupitia masafaya Redio ya Vatican ambayo imenisindikiza kwa miezi minne iliyopita. Walikuwa wametupatia redio ndogo mnamo  tarehe 20 Mei 20, tu na hii ilikuwa kama shukrani katika siku yangu ya kuzaliwa. Kiukweli ningependelea kuwa wangetupatia habari za ukombozi ambazo tulilazimika kusubiri tu, lakini kila jioni nilikuwa ninasikiliza Radio Vatican, hasa Jumamosi ilinipatia msukumo wa kiroho wa Injili ambao sikuwa nayo katika maandalizi ya Jumapili.

Kwa kuhitimisha Padre amesema "Hapa, ningependa kukushukuru kwa kile mnachofanya. Na nina mengi zaidi ya kuwaambia, lakini natarajia wakati nitakapokuja Roma na labda nitakuja na kuwatembelea. Lakini, pia mmeniunga mkono kwa matangazo yenu na kwa habari kwamba nilisikiliza kwa shauku halisi, kwa sababu mlinifungulia dirisha katika kifungo ambacho sisi Waitaliano tunaita "bis bis", kwa sababu kweli tulikuwa tumetengwa sana, bila mawasiliano yoyote na nje. Lazima niseme tu asante: asante, asante, asante kwa wale wote ambao waliniunga mkono kwa sala zao na shukrani ziwe kwa Mungu. Mungu alisikiliza maombi yetu".

19 October 2020, 13:49