Tafuta

2020.10.22 Misa ya kuanza utume wake Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe  22 ottobre 1978. 2020.10.22 Misa ya kuanza utume wake Mtakatifu Yohane Paulo II, tarehe 22 ottobre 1978. 

“Msiogope" ni mwangwi wa maneno ya Karol ambayo bado leo hii yanasikika!

Tarehe 22 Oktoba 1978 Papa Yohane Paulo II alianza utume wake ambapo katika maneno yake ya kwanza “Msiogope”,hayatasahulika na ambayo leo hii ni ishara ya imani na ujasiri.Ni kwa mujibu wa Monsinyo Oder ambaye amesisitiza kwamba katika janga la virusi vya sasa ulimwenguni mwangwi wa maneno hayo bado unasikika kwa nguvu zote.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Katika ulimwengu uliojeruhiwa na janga la virus linawataabisha walio wengi kutokana na ukosefu wa usalama. Kishawishi katika haya yote ni kutafuta njia za kuondokana na hali ngumu na ambapo kwa namna ya pekee tangu kuzuka kwake Papa Franisko amekuwa akiwaalika Jumuiya ya kimataifa wasitengane, na kusisitizia juu ya mantiki ya kuokolewa kwa pamoja na wala siyo pekee. Kwa bahati nzuri ni mazungumzo na hotuba mbali mbali zinazojirudia kusisisitiza maneno hayo. Kwa maana nyingine ni kusema ni sauti nyingine kuu inayofanana na Papa ambaye kunako tarehe 22 Oktoba miaka 42 iliyopita, mbele ya umati mkubwa ukiwa nyuso zake zimelekeza juu huku zikitazama ubaraza wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa shauku kubwa ya kuona Papa mpya Yohane Paulo II na ambaye alitamka maneno mazito “Msiogope! Funguka, na zaidi fungulieni milango Kristo!”.

Hii ni kutoa kichocheo wakati wa kuta na mifumo ya ukandamizaji kwa kiwango cha juu cha kutegemeana kwa nguvu ya kuokoa ambayo inatakiwa iwe kubwa. Leo hii ukuta unaohitajika kubomolewa ni virusi vidogo visivyo na kipimo, ambavyo kwa namna moja ndiyo ulikuwa wito wa Karol Wojtyla yaani Mtakatifu Yohane Paul II na ambapo bado unarudia kusikika wazi katika umuhimu wake.  Haya yamesemwa katika mahojiano na Vatican News na Monsinyo Slawomir Oder msimamizi wa mchakato wa kutangazwa Mtakatifu Yohane Paulo II katika siku ambayo liturujia ya siku, Mama Kanisa anamkubuka Mtakatifu Yohane Paulo II inayoadimishwa kila tarehe 22 Oktoba ya kila mwaka.

Monsinyo Oder anakumbuka hata sentensi ambayo alikutana nayo kwenye maandishi yake wakati anaanza shughuli ya kuongoza Kanisa, wakati anapitia mchakato wa historia yake anahitimisha kwa kuandikia: “Debitor factus sum”, yaani “nimekuwa mdeni” kwa maana hiyo sentensi hiyo anaifikiria kama ufungo wa kile ambacho baadaye yeye alikuwa  katika matukio mbali mbali ya Mtakatifu Yohane Paulo II. Yeye alilipa gharama ya maisha yake kwa madeni ya upendo hasa mbele ya Kristo na kwa maana hiyo “fungukeni na mfungulieni milango Kristo.

Maneno hayo ni yenye thamani kubwa katika programu na ambayo  basi bado yanafaa hata leo hii. Kwa sababu kama vile yalivyokuwa maisha ya Mkatifu Yohane Paulo II yalikuwa deni ya kulipa kwa upendo wa Mungu, kwa njia hiyo hata leo hii, ni kukubali  huo mwaliko ambapo  tunaweza kwa namna fulani kufanya sehemu yetu katika kulipa deni mbele ya yule  papa, na katika  historia tunayoishi leo hii. Ikiwa leo hii, hata katika muktadha wa ulimwengu ulioathiriwa na janga la corona, tunakimbilia Kristo, tunaweza pia kufungua mioyo yetu na akili zetu, dhamiri zetu na kufungua mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kiserikali, kiutamaduni, uwanja mkubwa ambao unafanya kazi kwa ajili ya mtu na kwa ajili ya ujumbe wa Kikristo kwa watu wote.

22 October 2020, 17:19