Tafuta

Msaada wa Shirika la Msalaba Mwekundu kimataifa katika harakati za wanaoteseka Msaada wa Shirika la Msalaba Mwekundu kimataifa katika harakati za wanaoteseka 

Dk.Maurer na Papa kwa ajili ya kujenga jamii ya mshikamano na shirikishi!

Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba mwekundu,Dk.Peter Maurer,katika mahojianao na Vatican News amezungumzia kuhusu Mkutano na Papa Francisko na jitihada za pamoja za kujenga ulimwengu ulioungana na mshikamano kwa wenye majeraha yanayoumiza ubinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kubadilishana maoni, maadili na matarajio katika ulimwengu uliojeruhiwa na kugawanyika na sasa hata kukumbwa na janga jipya la virusi vya  corona ambalo linazidi kuleta matatizo ya maisha na mengine ndiyo yanabainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu, Dk. Peter Maurer baada ya kukutana na Papa Francisko na baadaye Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican, tarehe 19 Oktoba 2020 mjini Vatican akihojiwa na Vatican News na Osservatore Romano. Dk. Maurer akizungumzia juu ya mkutano wa Papa Francisko  amesema awali ya yote, mkutano wake na Papa akiwa Roma ni kipindi mwafaka. Kiukweli ni fursa nzuri sana kwa sababu ni mikutano michache aliyo nayo ulimwenguni inayompatia  fursa kama hiyo ya kubadilishana maoni, mitazamo, maadili hata matarajio ambayo wanawakilisha. Iwe katika kuzungumzia juu ya tathimini na majibu kwa ajili ya migogoro ulimwenguni, kwa mtazamo wa imani tofauti za kidini, au iwe hata katika kuzungumzia mtazamo wa haki za kibinadamu kimataifa na ambazo hatimaye zinaingia ndani ya  makumi miaka na karne katika maadili mema ya kutenda kazi katika jamii. Kwa maana hiyo kuja kwake Roma amesisitiza, ni uzoefu chanya na zaidi ya hayo kuweza kuzungumza na Papa Francisko na kuwa na utambuzi  wa kweli wa kuungwa mkono naye kwa kile ambacho wao wanaendelea kutekeleza na kupeleka mbele kwa watu walioguswa na vita na kutumia nguvu, kwa maana hiyo amebainisha maana ya kupata nguvu mpya na chanya ambayo anarudi nayo nyumbani kwao.

Vatican news katika swali jingine  hakukosa kuuliza ni mtazamo gani alio nao kuhusu Waraka wa hivi karibuni wa Papa Francisko "Fratelli tutti" hasa masuala yanayokwenda sambamba na shughuli za Msalaba Mwekundu Kimataifa. Dk Maurer  amesema ni kuanzia na Wote ni ndugu, akiamini kuwa  ndiyo kauli mbiu na ufunguo ambao umeweza kutoa chachu  katika mchakato wa miaka mingi ya Kazi ya Msalaba Mwekundu.  Aidha anaamini msingi wa imani wanayoisimamia kama Msalaba Mwekundu, Vatican na Baba Mtakatifu, na hatimaye ni katika hitaji la  kupambana dhidi ya kugawanyika kwa jamii, kwani amekiri kuwa ni  migawanyiko ambayo inaleta uchungu kwa namna inavyoonesha  matokeo mabaya kwa  raia, kwa walioathirika, kwa wahamiaji na waliohamishiwa ndani kwa sababu ya vita na kutumia nguvu; kwa watu walioshambuliwa na mbio za ununuzi wa silaha katika jamii, kwa ajili ya watu waliopata pigo la mabadiliko ya tabia nchi, nchi ambazo bado zinaendelea, watu waliobaguliwa , umaskini na ukosefu wa haki. Aidha Dk huyo amesema ni vema kwenda kinyume na mantiki ya sasa kama ni kutumia lugha ya kisasa ili kuendelea na maoni katika jamuiya ambayo inakuwa tofauti, shirikishi, inaunganisha watu, inajenga madaraja mahali ambapo hali halisi  inagawanya jamii. Hii ndiyo anaamini kuwa  moyo wa mtazamo wao na maono yao, ya pamoja na katika jitihada zao za pamoja. Kama Mwenyekiti wa Shirika la Msalaba mwekundu amesema wanajivunia sana kuwa karibu na Vatican na Baba Mtakatifu kwa maana ya jitihada hizo.

Dk. Maurer akijibu kuhusu changamoto za Msalaba Mwekundu wanazokabiliana nazo hasa katika msaada kwenye mantiki ya sasa ya janga, anaamini kuwa vurusi vya coroana vimeongezea sana matatizo mengi ambayo yalikuwapo tayari na yanajulikana na sasa matatizo yameongezea mara dufu yale ambayo wamekuwa wakipambana nayo kwa miaka ya mwisho. “ Tumeona vita na kutumia nguvu vilivyo shambulia jamii; tumeona umaskini, na mabadiliko ya tabia nchi jinsi ambavyo yameleta matatizo makubwa na  ambayo tayari yalikuwapo hasa katika mantiki ya walio tayari athirika  kama vile Ukanda wa Sahel, Ziwa Chad au Pembe ya Afrika na Pasifiki… Leo hii tunaona jinsi gani covid inayo ongezea matatizo kwa hayo yote  na kusababisha mantiki zote  kuwa ngumu", amesisitiza. Kwa njia hiyo Bwana Maurer anaamini kuwa lipo janga halisi  hasa kwa kutazama migawanyiko iliyopo na kwamba matajiri wameongezea utajiri na maskini kuwa maskini zaidi, pia waliobaguliwa kuwa wengi zaidi. "Hi ni changamoto kubwa ambalo lazima kukabiliana nali. Hata matokeo ya covid, kama vile ukosefu wa ajira mbao umezikumba nchi  zote na zaidi watu walio maskini sana kiasi cha  kuzidisha hali kuwa mbaya sana".

Akijibu swali kuhus kanda ambazo bado zimekumbwa na vita ulimwenguni na ambapo Shirika la Msalaba mwenkundu wanaendelea kutoa msaada amesema, ikiwa  wanaangalia bajeti yao na eneo la watu wengi, wanaona kuwa zaidi ya asilimia 40 ya shughuli zinazotendeka ni  barani Afrika na zaidi ya asilimia 30 ni katika Nchi za Mashariki ya Kati. Hii ina maana kuwa migogoro katika Nchi za Mashariki ya Kati na barani Afrika zinanachukua nafasi za mbele  katika shughuli za msalaba mwekundu. Hii ni katika kuzungumzua Ukanda wa Sahel,  Ziwa Chad, Sudan zote mbili, Congo zote mbili, Pembe ya Afrika,  ni wazi hata Libia nyo ni Afrika; baadaye kuna Nchi za Mashariki ya Kati katika migogoro yake nchini Siria na Yemen na ile ya Iraq, ambazo zimo ndani ya kiini cha shughuli za Msalaba Mwekundu. Hata hivyo kuna maeneo mengine ya ulimwengu ambayo ni wageni kwenye orodha  aliyoitajana  ambayo pia ni orodha ya zamani ya takwimu. Kwa miaka sita ya mwisho, amesema nchini Ukraine, Shirika la Msalaba mwekundu wameanza jitihada zao msingi za Kimataifa; na hivi karibuni, huko Nagorno Karabakh na migogoro ya Armenia ambayo imeibuka kwa ghafla na kuzidisha shida nyingi, bila kusahau kujitoa kwao kwa muda mrefu huko Afghanistan na Amerika Kusini.

20 October 2020, 13:53