Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kila mwaka ifikapo tarehe 2 Oktoba, Kanisa linawakumbuka na kuwaenzi Malaika Walinzi, kimbilio la waamini wengi wakati wa shida na mahangaiko. Baba Mtakatifu Francisko anasema, kila mwaka ifikapo tarehe 2 Oktoba, Kanisa linawakumbuka na kuwaenzi Malaika Walinzi, kimbilio la waamini wengi wakati wa shida na mahangaiko. 

Papa Francisko: Tarehe 2 Oktoba Sikukuu Ya Malaika Walinzi!

Papa Francisko anasema kila mwaka ifikapo tarehe 2 Oktoba, Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya kuwaenzi na kuwashangilia Malaika Walinzi. Sikukuu hii ilianzishwa na Papa Clementi X kunako mwaka 1670. Tangu katika Agano la Kale, Mwenyezi Mungu aliwaweka Mababa wa imani, watumishi wake waaminifu na taifa zima la Israeli chini ya ulinzi na tunza ya Malaika Walinzi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake, Jumatano tarehe 30 Septemba 2020 amewakumbusha waamini kwamba, kila mwaka ifikapo tarehe 2 Oktoba, Mama Kanisa anaadhimisha Sikukuu ya kuwaenzi na kuwashangilia Malaika Walinzi. Sikukuu hii ilianzishwa na Papa Clementi X (1670-1676) kunako mwaka 1670. Malaika walinzi, “Anghelos” kwa Lugha ya Kigiriki ni wajumbe wa Mungu, ambao wameelezwa katika Maandiko Matakatifu na katika historia ya kazi ya ukombozi. Tangu katika Agano la Kale, Mwenyezi Mungu aliwaweka Mababa wa imani, watumishi wake waaminifu na taifa zima la Israeli chini ya ulinzi na tunza ya Malaika Walinzi. Rej. Mwa. 18; na 32: 25-29.

Kwa ufupi, Malaika Walinzi wamekuwa wakihusishwa na kazi ya Uumbaji, Tasaufi, Kipaji cha akili, Utashi, Dhamana na wajibu; kupanda na kushuka kwa mtu! Baba Mtakatifu Francisko anasema, Malaika Walinzi ni wale ambao waamini wanawakimbilia mara kwa mara katika sala zao, ili waweze kuwalinda na kuwaokoa katika hatari zote za kiroho na kimwili. Malaika Walinzi wanawasaidia waamini kumwangalia Kristo Yesu, Mkombozi pekee wa ulimwengu.

Malaika Walinzi

 

01 October 2020, 15:01