Tafuta

2019.11.15 Imam Mkuu  Ahmed Al-Tayeb Sheikh wa  Al-Azhar. 2019.11.15 Imam Mkuu Ahmed Al-Tayeb Sheikh wa Al-Azhar. 

Al-Tayyeb:dhamiri ya ubinadamu imerudishwa tena na Ndugu yangu Francisko!

Katika ujumbe wa Imam di Al-Azhar akigusia kuhusu Waraka wa Kitume wa Papa Francisko “Fratelli tutti” yaani wote ni Ndugu uliotangazwa na Papa katika Siku ya Maadhimisho ya Mtakatifu Francis wa Assisi tarehe 4 Oktoba 2020 anasema Dhamiri ya ubinadamu imerudishwa tena na Ndugu yangu Francisko!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika waraka wa kitume ni uliotangazwa ni ujumbe ambao unarudisha kwa mara nyingine tena kuhusu dhamiri ya ubinadamu. Kuna maoni mengi na maalum kati ya wengi ambayo yamechapishwa mtaondoni katika masaa machache mara  baada ya kuchapishwa kwa Waraka wa Kitume wa  Papa Francisko  wa “ Fratelli Tutti” yaani “ Wote ni Ndugu”. Mojawapo  ya  ujumbe ni katika  Twitter  ya   Imam Mkuu wa Al-Azhar, Ahmad Al-Tayyeb, aliyesaini na Papa Francisko katika Hati juu ya ‘Udugu wa kibinadamu kwa ajili ya amani ya ulimwengu na kuishi pamoja’, iliyotiwa saini huko Abu Dhabi mnamo Februari 2019.  

Waraka wa tatu wa Papa Francisko kuanzia tamko hilo la pamoja na Al-Tayyeb ametajwa mara kadhaa katika maandishi hayo. Katika maneno ya Imam Mkuu kwenye mtandao wa kijamii uliotangazwa tarehe 4 Oktoba 2020, anasema ni nyongeza ya waraka juu ya udugu wa kibinadamu na inafunua ukweli wa ulimwengu ambamo msimani na maamuzi kwa wastani bado yanawatazama watu watu walio katika mazingira magumu na waliotengwa na ambao  wanaolipa gharama kubwa(...)  Ni ujumbe ambao umewasilishwa kwa watu wenye mapenzi mema na dhamiri hai  katika kurudisha dhamiri yao tena ya ubinadamu.

Kwa ujumbla katika uwasilishaji wa wa Waraka huo ambao afla yake ilifanyika katika Ukumbi mpya wa Sinodi ya Maaskofu  Vatican, alishiriki hata Jaji Mohamed Mahmoud Abdel Salam, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Hati ya ‘Udugu wa Binadamu’.

05 October 2020, 13:25