Tafuta

2020.09.11 Papa Francesko katika mkutano kwenye Ukumbi wa Paulo VI na washiriki wa Mkutano Komataia wa Magonjwa ya saratani ya Kike. 2020.09.11 Papa Francesko katika mkutano kwenye Ukumbi wa Paulo VI na washiriki wa Mkutano Komataia wa Magonjwa ya saratani ya Kike. 

Papa Francisko:Tusiruhusu uchumi uingilie kwa nguvu afya hadi kufikia hatua ya kuadhibu uhusiano na wagonjwa!

Umuhimu wa kukuza uhusiano wa mshikamano,heshima ya hali ya kisaikolojia na kiroho kwa kila mgonjwa na kuwahusisha ndugu na wahudumu wa kiafya katika uhusiano mmoja ndiyo imekuwa kiini cha hotuba ya Papa Francisko alipokutana na washiriki wa Mkutano kimataifa magonjwa ya kike na saratani.Hatupaswi kuruhusu kwamba uchumi uingilie namna hii kwa nguvu katika ulimwengu wa kiafya hadi kufikia hatua ya kuadhibu uhusiano na wagonjwa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 amekutana na washiriki wa Mkutano kimataifa wa magonjwa ya wanawake (Oncological gynecology),  ambapo amewakaribisha na kuwashukuru kwa matembezi yao katika fursa hii ya Mkutano wao wa Mwaka wa “International Gynecologic Cancer Society), yaani “Chama cha kimataifa cha Saratani ya wanawake.  Akiendelea na hotuba yake amesema ugeni wao umempa fursa ya kujua na kupongeza jitihada za Chama chao kwa ajili ya wanawake ambao wanakabiliwa na magonjwa haya magumu sana. Amemshukuru Rais wao Profesa Roberto Angioli ambaye alianzisha mpango huu. Papa Francisko hakusahau hata wawakilishi wa mashirika mengine, hasa miongoni mwao waliopona na ugonjwa huo ambao wanasaidia kushirikishana katika mchakato wa upamoja wa tiba. Katika huduma yao msingi, wao wanatambua vema umuhimu wa kukuza uhusiano wa mshikamano kati ya watu walio na magonjwa magumu sana, kwa kuwahusisha ndugu na wahudumu wa kiafya katika uhusiano mmoja wa kutoa msaada. Hiyo inageuka kwa mra nyingine kuwa tunu msingi na inasaidia kutia moyo kwa wagonjwa ambao wanaweza kuwa hatarini zaidi au kutelekezwa, uzazi na umama. Katika hali hizo ambazo zinakumba maisha ya mwanamke, Papa Francisko ameongeza kushauri kwamba ni muhimu kuwa na tiba, kwa unyeti sana na heshima ya hali ya kisaikolojia, uhusiano na  ya kiroho kwa kila mgonjwa.

Kwa sababu hii Papa Francisko amewatia moyo jitihada zao kwa ajili kufikiria ukuu wa kazi ya tiba fungamani, hata katika kesi ambayo tiba shufaa (palliative care) ni muhimu na kuhitajika. Katika matarajio haya, inakuwa lazima sana kuhusisha watu wenye uwezo wa kushirikishana mchakato wa safari ya kutibu kwa kutoa msaada wa imani, matumaini na mapendo. Papa pia ameongeza “sisi sote tunatambua na hata kujionesha kwamba kuishi na uhusiano mwema unasaidia na kutia moyo mgonjwa wa siku nyingi katika mchakato wote wa kupata matibabu, kwa kuwangazwa tena au kuongezea kwao matumaini. Ni ukaribu huo wa upendo ambao unafungua milango ya matumaini na hata kwa uponyaji. Mtu mgonjwa kila wakati na ni zaidi ya itifaki ambayo imewekwa kutoka katika maoni ya kliniki. Uthibitisho wa hili ni ukweli kwamba wakati mgonjwa anatambuliwa hali yake, uzoefu wao unaweza kuthibitishwa na kukuzwa imani yake kwa timu mzima ya kidaktari na kwa kufafanua ndani mwake maono chanya. 

Shauku ya Papa Francisko na ambayo anafikiri hata wao isibaki kama kielelezo cha wazo tu, bali ipate daima na zaidi kutambuliwa ndani ya mfumo wa kiafya. Mara nyingi amesema, ithibitishwa kuwa uhusiano, na makutano na mtu wa afya ni sehemu ya tiba. Ni faida kubwa inayotolewa kwa wagojwa kuwa na fursa ya kujifungua moyo wao kwa uhuru wote na kuwambia hali zao kwa imani na hali halisi. Pamoja na hali katika uhalisia huo, ni kwa namna gani  ya kuendeleza  ulazima huu wa hitaji kubwa la ndani ya shirika la hospitali, lililowekwa vizuri na mahitaji ya utendaji? Papa Francisko katika kujibu hili amebainisha uchungu wake na wasi wasi, unaohusu hatari hasa iliyoenea ya kuwacha kutunza ukuu wa kibinadamu kwa watu wagonjwa kwa mapenzi mema, ya daktari binafsi, badala ya kufikiriwa kama sehemu fungamani ya shughuli ya kutibu inayotolewa na muunda wa kiafya. “Hatupaswi kuruhusu kwamba uchumi uingilie namna hii kwa nguvu katika ulimwengu wa kiafya hadi kufikia hatua ya kuadhibu mambo muhimu kama vile uhusiano na wagonjwa. Kwa maana hii, vyama visivyo vya faida ambavyo vinaweka wagonjwa katika kituovu vinapaswa kupongezwa kwa kuunga mkono na kusaidia  mahitaji yao na maombi yao  halali na pia kutoa sauti kwa wale ambao, kwa sababu ya udhaifu wa hali yao ya kibinafsi, kiuchumi na kijamii, hawawezi kusikilizwa

Kwa hakika utafiti unahitaji jitihada kubwa ya uchumi. Lakini Papa Francisko anaamini kwamba licha ya uchumi huo inawezekana kupata njia kutoka katika  mantiki tofauti.  Nafasi ya kwanza inapaswa kutambuliwa ya watu, katika kesi hiyo wanawake wagonjwa, lakini hatupaswi kusahau hata watu ambao kila siku wanawasiliana nao na ili waweze kufanya kazi katika hali zinazostahili. Hata kama wanaweza kuwa na muda wa kupumzika ili wawe na nguvu ya kuendelea mbele. Papa Francisko anawatia moyo wa kueneza ulimwenguni kote tunu ya matokeo ya mafunzo yao na tafiti zao , kwa ajili ya wanawake ambao wanawasaia tiba.  Wao licha ya matatizo yao, lakini wanakumbusha mantiki ya maisha ambayo wakati mwingine tunasahau, kama vile hatari ya uwepo wao  hitaji la kila mmoja, kutokuwa na maana ya  kuishi inayozingatia ubinafsi tu, ukweli  halisi wa kifo kama sehemu ya maisha yenyewe. Hali ya ugonjwa inaalika ile tabia ya uamuzi wa kweli kwa ajili a kuwa binadamu ambaye anatakiwa aamini. Kuamisni kaka na dama mwingine, na mwingine ambaye ni Baba Yetu wa Mbinguni. Ugonjwa pia unatukumbuka hata thamani ya ukaribi, wa kujifanya karibu kama anavyotufundisha Yesu katika msema wa Msamaria Mwema (Lk 10,25-37). Ni jinis gani bembelezo linavyoponesha wakati muafaka! ninyi mnatambua vema zaidi yangu…”

Kwa kuhitimisha Papa Francisko amewatakia matashi mema ya kazi yao. kwa familia zao kazi zao, vyama vya na wote ambao wanatunza wagonjwa amewapa bara ya Mungu kila mmoja katika imani yake, kisima cha matumaini, nguvu na amani ya ndani. Anawathibitishia sala na kwamba mapadre daima wanaomba, lakini mimi ninaishia kuwaomba kusali kwa ajili yangu kwa sababu nina mahitaji.

11 September 2020, 15:02