Tafuta

2020.09.26 Misa ya Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican 2020.09.26 Misa ya Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa ajili ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama mjini Vatican  

Papa Francisko:Vikosi vya Ulinzi Vatican vihudumie kwa unyenyekevu na udugu!

Mamlaka ni huduma ambayo hufanyika kwa moyo wote.Ndiyo ushauri wa Papa Francisko katika mahubiri yake rahisi aliyowalekeza Jumamosi jioni,26 Septemba kwa Vikosi vya Ulinzi na usalama katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.Tafakari yake amejikita juu ya njia ambayo Mungu aliichagua katika Kristo ili kutusamehe na uongofu na ambayo ni huduma.Yote hayo ni kuiga mfano wake ambao huwezi kukosea katu.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi jioni, tarehe 27 Septemba 2020, ameadhimisha misa kwa ajili ya vikosi vya ulinzi na usalama vya Vatican katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Katika mahubiri yake yamejikitakufafanua masomo ya Dominika ya 26 ya mwaka na kwamba masono hayo yanaelezea juu ya uongofu. Uongofu wa moyo. Uongofu wa moyo maana yake ni kubadili maisha kwa kuacha njia mbaya na kufuata ile iliyo nzuri. Lakini uongofu huo  sio wetu  tu bali hata uongofu wa Mungu. Katika somo la kwanza linasema “Tena, mtu mwovu atakapoghairi, na kuuacha uovu wake alioutenda, na kutenda yaliyo halali na haki, ataponya roho yake, nayo itakuwa hai” (Ez 18,27-28). Hii ina maana ya mwovu anaongoka. Na kwa urahisi ni kusema mdhambi anaongoka na Mungu anaongokea mdhambi, Papa amesema. Mkutano na Mungu ni uongofu wa sehemu zote mbili na ambazo zitafuta namna ya kukutana. Msamaha siyo tu kwenda pale na kubisha mlango: “nisamehe na katika dirisha unasikia sauti inasema nimekusamehe, nenda zako”, hapana, Papa anafafanua. Msamaha ni mkubatio daima wa Mungu. Lakini Mungu anatambea kama sisi tunavyotembea ili kukutana nasi. Huo ndiyo msamaha wa Mungu kwa namna ya kuongoka.

Maswali. Je mimi nitakwendaje kwa Mungu wakati mimi ni mdhamb? Hicho ndicho Mungu anataka kwamba uende kwake. Je baba wa mtoto mpotevu alifanya nini? Na ambaye aliondoka na fedha  zake na midekezo yake,  baba huyo alifanya nini? Alipomwona kwa mbali hakuwa na sababu za kusita bali alikuwa anahisi kwamba mwanae lazima arudi; alikuwa arudi kwa sababu ya mahitaji. Akiwa katika  ngazi alishuka kwa haraka na kwenda kukutana na mwanae. Yeye hakusubiri mlangoni akimwelekeza kidole, bali alimkubatia! Wakati mtoto alipokuwa kuzungumza na kuomba msamaha, alifunga mdomo wake kwa mkumbatio. Huo ndiyo uongofu. Huo ndiyo upendo wa Mungu. Ni safari ya kukutana mmoja na mwingine, Papa Francisko amefafanua. Akiendelea na mahubiri hayo  Papa amependa kusisitiza juu ya hilo kwamba moyo ambao uko wazi kila wakati hukutana na Mungu na ndiyo ni uongofu.

Kuwa  wazi kukutana na Mungu  mfano wake ni nini? Mfano wake ni ni ule wa  Injili, wa  tajiri, wa masikini, kwa maana nyingine mfano ni Yesu Kristo. Yeye alitoka nje  ili kukutana nasi. Katika somo la Pili linasema “Iweni na hisia sawa na za Kristo Yesu: yeye, licha ya kuwa katika hali ya Mungu, Yesu alikuwa Mungu lakini  hakuona kuwa ni upendeleo kuwa kama Mungu  ambapo ni kusema, kubaki pale, bali alijikana na kuchukua  hali ya mtumishi na kuwa sawa na watu. […] Alijinyenyekeza na kuwa  mtii hata  kifo na kifo msalabani ”(Fl 2,5-8). Njia ya uongofu ni kukaribiana, ni ukaribu, lakini ukaribu ambao ni huduma.  Papa Francisko amependa neno hili kuwasisitizia hao ndugu wapendwa wa  vikosi vya usalama. Papa amesema kuwa wakati wowote wanapo karibia kutumikia, wamuige Yesu Kristo. Kila wakati wanapochukua hatua ya kuleta utaratibu, wafikirie wanafanya huduma, wanafanya ubadilishaji ambao ni huduma.

Papa Francisko amesema kuwa ni kwa jinsi ambavyo wanafanya, watakuwa wanawatendea wengine mema. Na kwa hilo, amependa  kuwashukuru. Huduma yao ni uongofu maradufu, kwanza ni uongofu wao binafsi  kama ule wa Yesu Kristo wa kuacha raha zao, kuacha ... ili kwenda kutumikia na ya pili ni uongofu wa mwingine , ambaye hajisikii kuadhibiwa katika dakika za kwanza, japokuwa anasikilizwa sawa, kwa unyenyekevu kama wa Yesu. Kwa maana hiyo Yesu amewaomba wawe kama yeye, yaani hodari, wenye nidhamu, lakini pia wanyenyekevu na watumishi. Papa Francisko ametoa  mfano mmoja ya kwamba alisikia mzama mmoja akilalamika kuhusu kukaripia watoto wake na kusema "mtoto wangu hajuhi kuwa kukaripia watoto ni kupoteza mamlaka".

Ppa kwa kufafanua hili amesema mamlaka yao yako katika huduma. Kuweka mipaka, kufanya mambo yanatimiziwa, lakini kwa huduma, kwa upendo na kwa fadhili. Na huu ni wito wao mzuri. Kwa upande wa Papa amesema itakuwa huzuni kubwa ikiwa mtu atamwambia kuwa "Kikosi chako cha Ulinzi ..., ni wafanyakazi, ambao hufanya ratiba zao halafu hawajali .... “Hapna hii siyo njia ya uongofu na kufanya ongofu kwa wengine. Njia yenu ni ile ya kutoa huduma, kama baba anayekwenda kumtembelea mtoto wake, kama kaka anayeona kitu na kusema: hiki siyo swa cha kutendwa na hivyo siyo nzuri". Hiy ndiyo njia, ya kusahihisha, lakini ni kusema kwa  moyo, kwa unyenyekevu na  kwa ukaribu".  Kwa sababu huduma ni upendo, ni ukaribu. Huduma ni njia ambayo Mungu amechagua katika Yesu Kristo kutusamehe na  kutufanya tuongoke. Biblia  katika Injili inasema, kwamba Yesu alikuwa daima na wenye dhambi, pamoja na watenda maovu pia, lakini wao walihisi kuwa karibu na Yesu, hawakuhisi kuhukumiwa. Japokuwa  Yesu hakuwahi kusema uwongo, Hapana Papa amesisitiza. Hii ndiyo ukweli, hiyo ndiyo njia.  Na kwa hakika alisema kwa fadhili, alisema kwa moyo wake, na alisema kama kaka.

Papa amewashukuru kwa huduma yao na kwa sababu anaona huduma yao ikiendelea kwa njia hii. "Wakati mwingine mtu anaweza kuteleza kidogo, lakini ni nani hasiye teleza maishani? Wote! Lakini tunaamka", amesema Papa.Kwa kutoa mfano mwingine: "Sikuweza fanya vizuri, lakini sasa…?" Jibu: "Daima endelea na safari hiyo kwa uongofu kwa watu pia kwa uongofu binafsi. Katika huduma ndiyo Mungu alichagua kwa njia ya Yesu  Kristo ili kutusamehem na kutuongoa daima".

27 September 2020, 12:15