Tafuta

2020.09.22  Papa Francisko pamoja na Vina wa Argentina mano Julai 2013 huko Rio. 2020.09.22 Papa Francisko pamoja na Vina wa Argentina mano Julai 2013 huko Rio.  

Papa Francisko:vijana muwe na mawazo ya kuubadili ulimwengu!

Papa Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa Hija ya 41 ya vijana wa Kaskazini Mashariki mwa Argentina na kuwataka wawe na mawazo ya kuubadili ulimwengu.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kuweni watu wanaoishi, watu wenye maadili, watu wanaobadilisha ulimwengu. Msikae kimya, msiwe kama sanamu. Ni maneno ya papa Francisko aliyowatia moyo vijana wa Argentina. Katika ujumbe kwa njia ya video na kutangazwa tarehe 19 Septemba 2020  na Jimbo kuu la Corrientes, Papa Francisko amewasalimu vijana walioshiriki, Jumamosi iliyopita, katika Hija ya  41 ya Vijana wa mkoa wa Nea (Kaskazini mashariki mwa Argentina). Mwaka huu, tukio hilo imefanyika karibu kwa njia ya mtandao kutokana na janga la virusi vya corona. Na hili ni jammbo ambalo limekumbukwa na Papa mwenyewe.

Kwa mujibu wa Papa amesema “hija hii inafanywa kwa njia isiyokuwa ya kawaida, lakini hata ikiwa ni kwa njia hii ya mtandao ninyi mnaifanya kwa njia ile ile na mnaweka moyo wote kuelekeza katika safari hii halisi, ili kukutana na Mama. Ninawasikindikiza katika safari hii mpya, lakini ambayo daima ni muhimu na msisahau kamwe kuwa maisha ni safari”. Kadhalika Papa Francisko akiendelea kusisitiza amesema licha ya shida na makosa ambayo kila mtu anaweza kukutana njiani, lazima kila wakati tujaribu kuamka na kurudi kwenye njia, kwa sababu kukaa bado kuna hatarisha kuwa kama  sanamu, kama  vile Mke wa Lutu, ambaye aligeuka kuwa nguzo ya chumvi baada ya kugeuka nyuma, kwenda Sodoma. Hatimaye Papa Francisko aliwapa baraka zake vijana, akiwakumbusha kwamba, Bikira Maria anajua kinachotokea katika kila mioyo yao, kwa sababu yeye ni Mama na anawajali.

22 September 2020, 14:53