Tafuta

Vatican News
2019.03.28 Njia iliyo safi, asili, mazingra na miti. 2019.03.28 Njia iliyo safi, asili, mazingra na miti. 

Papa Francisko:Dunia ni fumbo la tafakari ya furaha na sifa!

Katika ujumbe wa Papa kupitia mitandao ya kijamii anakazia fumbo la dunia kuwa ni furaha.Na Askofu Mkuu Perego akitoa hotuba huko Jolanda amekazia ujumbe wa siku ya maombi ya kazi ya uumbaji kuwa:mazingira ni nyumba ya Mungu,ni sakramenti,mahali ambamo tunaendelea kuona uwepo wake.Kuishi katika Nyumba ya Mungu maana yake ni kukubali kuishi mtindo mmoja wa maisha mapya

Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Jumatatu tarehe 7 Septemba 2020 katika ujumbe wake Papa Francisko kwenye mitandao ya kijamii anasema: “Dunia ni jambo kubwa zaidi ya matatizo ya kutatua, ni fumbo la furaha ambalo tunapaswa kutafakari kwa kina, kwa furaha na sifa”. Ni katika muktadha wa kipindi cha Kazi ya uumbaji kinachoendelea hadi tarehe 4 Oktoba 2020. Katika mantiki hiyo, Baraza la Maskofu nchini Italia wanasema hiki ni kipindi cha kuishi ulimwengu na kiasi, haki na uchaji wa Mungu kwa mitindo mpya ya maisha kama ibainishavyo mada ya mwaka huu iliyochaguliwa. Dharura inayohusiana na mgogoro wa janga la corona ambayo inaendelea umefanya kutambua zaidi na haraka umuhimu wa kuwa na maono fungamani ya mwanadamu kuhusu kazi ya uumbaji, ili kuachilia mbali mtindo ule  wa kuendelea kurarua na wakati huo kwa kujikita kupanga katika jamii yenye uwezo wa kugundua kwa upya uhai wote na kushirikishana katika mtazamo wa haki.

Kanisa nchini Italia limeweza kutoa tafakari katika Mkutano wa umma uliofanyika tarehe 5 na tarehe 6 Septemba 2020 huko Savoia, nchini Italia. Mkutano huo imewakilisha siku ya 15 ya Kitaifa kwa ajili ya Ulinzi wa Mazingira, unaoongozwa na kauli mbiu: “Kuishi katika ulimwengu huu kwa kiasi, kwa haki na kwa uchamungu”(Tt 2:12). Kwa mitindo mipya ya maisha”. Jumapili tarehe 6, Misa ya moja kwa moja imeadhimishwa katika Kanisa Kuu la Comacchio, kwa kuongozwa na Askofu Mkuu Gian Carlo Perego wa jimbo Kuu la Ferrara-Comacchio, Italia.

Askofu Mkuu Perego akitoa hotuba yake huko Jolanda kwenye mkutano huo amesema umuhimu siyo tu wa kulinda mazingira bali ni namna mpya ya kuweza kuishi katika nchi, kuwa na mitindo ya kweli ya  maisha. Dunia, kama asemavyo Papa Francisko katika ujumbe wake wa Siku ya Kuombea Kazi ya Uumbaji, iliyofanyika tarehe Mosi Septemba, “ni nyumba ya Mungu, ni sakramenti, mahali ambamo tunaendelea kukaribisha na kuona uwepo wake”. Kuishi katika  Nyumba ya Mungu maana yake ni kukubali kuishi mtindo mmoja wa maisha mapya, yaliyosimika mzizi wake juu ya uwajibikaji na ambao kitovu chake ni mpango wa pamoja wa jumuiya”. Ni kwa njia hiyo tu tutaweza kujua umuhimu wa kukabidhi nyumba ya Mungu kwa kila ndugu zetu kaka na dada na vizazi vipya”.

Vizazi vilivyoadhibiwa na uchaguzi mbaya uliotekelezwa katika miongo ya hivi karibuni, kama ilivyo tafakariwa na  Padre  Bruno Bignami, mkurugenzi wa Ofisi ya Kitaifa ya Matatizo ya Jamii na Kazi ya  Baraza la Maaskofu Italia (CEI): “Mfano wa maendeleo ya miongo ya hivi karibuni umeshindwa kwa sababu umejikita tu juu ya  wingi na siyo kwenye ubora wa mahusiano kijamii na ya kibinafsi”.  “Bila undugu hakuna uhuru” Akitaja kitovu cha hayo ni kile cha undugu, unaofanywa kweli na wakati huo huo kama ilivyo tangazwa kwa waandishi wa habari juu ya saini ya tarehe 3 Oktoba itakayotiwa huko Assisi na Papa  Francisko katika  Waraka wake wa kitume wa "Ndugu wote" ambao unajikita kwenye tafakari juu ya udugu na urafiki kijamii.

Katika hotuba nyingine pia ilikuwa ni ya Stefano Zamagni, profesa wa Uchumi wa Siasa katika Chuo Kikuu cha Bologna na rais wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi ya Jamii  amesema nchini Italia kama ilivyofanywa mwaka 1950 na Adenauer huko Ujerumani ingekuwa vizuri kurekebisha Mkataba Kikatiba kwa kuingiza, jukumu la kila uchaguzi wa Serikali kama uamuzi kwa vizazi vijavyo, hasa kwa sababu ya matokeo ya kiekolojia.  Kwa maana hiyo kuna mabadiliko ya aina nne msingi: mpito wa nishati, uchumi, utamaduni na elimu ya viumbe.

07 September 2020, 16:50