Tafuta

2020.09.23 Katekesi ya Papa Francisko 2020.09.23 Katekesi ya Papa Francisko 

Papa Francisko:tutaondokana na mgogoro ikiwa tutashirikiana na wadhaifu!

Katika katekesi ya Papa Francisko,amesisitizia kuhusu mashirika ya kimataifa au kampuni kubwa za dawa kusikilizwa zaidi kuliko harakati za kijamii au wafanyakazi wa afya.Amekazia kuheshimu uhuru na uwezo na mipango ya wote hasa familia,vyama na wafanyabiashara wadogo.Ameomba kuwapongeza kwa makofi hata kwa walio wadhaifu na kubaguliwa kama wazee,watoto yaani kiungo chote cha kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Papa Francisko akianza tafakari yake inayohusu janga la virusi vya corona au covid -19 hasa kwa kutazama matokeo yake katika jamii nzima kwenye katekesi yake Jumatano tarehe 23 Septemba 2020, kwa waamini na mahujaji waliokaa katika uwanja wa Mtakatifu Damas mjini Vatican ameendeleza mada hiyo ya umakini kwa kuongozwa na Injili na Kanuni za Mafundisho jamii ya Kanisa. Papa Francisko amesema ili kuondokana na mgogoro vema kama ulivyo wa sasa na ambao ni mgogoro wa kiafya na wakati huo huo mgogoro wa kijamii, sera za kisiasa na kiuchumi na kila mmoja wetu anaitwa kuwa sehemu ya uwajibikaji yaani kushirikishana na uwajibikaji. Lazima kujibu si tu kama mtu binafsi, bali hata kuanzia na kikundi chetu, nafasi zetu tulizo nazo katika jamii, kutoka misimamo yetu na ikiwa ni waamini wa imani katika Mungu. Mara nyingi lakini watu wengi hawawezi kushiriki  katika ujenzi wa wema wa pamoja kwa sababu, wametengwa, wamebaguliwa na kudharauliwa. Papa amesema kuwa baadhi ya makundi mengine ya kijamii hayawezi kuchangia kwa sababu ya kusongwa kiuchumi au kisiasa. Baadhi ya jami, watu wengi hawana uhuru wa kujielezea imani yao na thamani zao binafsi, mawazo yao na ikiwa wanajifafanua kwa uhuru basi wanapelekwa magereza. Mahali pengine hasa katika ulimwengu wa magharibi, watu wenye kujitosheleza hujikandamiza imani zao za kimaadili au kidini. Kwa maana hii haiwezekani kabisa kuondokana na mgogoro au tuseme haiwezekani kuondokana kuwa bora. Tutatoka humo vibaya zaidi.

Papa Francisko akiendelea na katekesi hiyo amesema ili kuweza wote kushiriki utunzaji  na kuzaliwa kwa upya kwa watu wetu ni haki kila mmoja awe na rasilimali za kutosa kufanya hivyo ( taz hati ya mafundisho jamii ya Kanisa [CDSC], 186). Baada ya mgogoro mkubwa wa kiuchumi wa mwaka 1929, Papa Pio XI alielezea jinsi gani ilivyokuwa muhimu kwa ajili ya ujenzi mpya wa misingi ya ushirishika (Wosia wa Quadragesimo Anno ambao  ulikuwa ni wa  kwanza kijamii na neno kijamii kufafanuliwa   rasmi ya kanuni ya ushirika (n 79 – 80). Kanuni hii ina nguvu mbili moja kutoka juu hadi chini na kutoka chini hadi juu. Labda hatujua nini maana yake lakini ni kanuni hii kijamii ambayo inatufanya kuunganazaidi, Papa Francisko amebainisha na kusisitiza kuwa ataeleza vizuri.

Kwa upande mwingine hasa katika kipindi cha mabadiliko, ikiwa watu binafsi, familia, vyama vidogo vidogo au jumuiya mahalia havina uwezo wa kufikia malengo msingi, hapo kuna haki ya kuweza kuingilia kati kutoka ngazi ya juu zaidi katika kiungo cha kijamii, kama Taifa, ili kutoa rasilimali za lazima kwenda mbele. Kwa mfano kwa sababu ya karantini, kutokana na virusi vya corona, watu wengi, familia na shughuli za kiuchumi zimejikuta hata sasa katika matatizo makubwa kwa njia hiyo, taasisi za umma wanajaribu kusaidia kwa hatua zinazofaa. Kijamii, kiuchumi, kiafya… hiyo ndiyo inayofanya kazi na ndiyo wanayotakiwa kufanya. Kwa upande mwingine lakini viongozi wakuu wa kijamii lazima waheshimu na kuhamasisha kwa ngazi za kati au za chini.  Hii kiukweli, mchango wa watu binafsi, familia, vyama, biashara, vyombo vyote vya kati na hata Makanisa ni maamuzi. Vyombo hivi kwa rasilimali zake za kiutamaduni, kidini, kiuchumi au asasi za kiraia, huhuisha na kuimarisha mwili wa kijamii (taz. CDSC, 185).  Yaani kuna ushirikiano kutoka juu kwenda chini, kutoka Serikalini kwenda kwa watu na kutoka chini kwenda juu. Ikiwa na maana ya kutoka Taasisi za watu walio wa juu,nda  ndiyo kweli kazi msingi ya ushirika inavyotakiwa kufanyika.

Kila mmoja lazima wawe na uwezo wa kuchukua uwajibu wake katika mchakato wa uponywaji wa kijamii ambamo anashiriki. Ikiwa unaanzishwa mpango fulani ambao unatazama moja kwa moja au la kwa vikundi vya kijamii, hawa hawawezi kuachwa nje katika ushiriki; Papa Francisko ametoa mfano: Je wewe unafanya nini hapa? Ninakwenda kufanya kazi kwa ajili ya maskini, hili ndilo jibu zuri! Na mwingine,  je unafanya nini? Jibu “ Mimi ninafundisha maskini  wanachotakiwa kufanya” … Papa ameongeza kusema  “hiyo hapana , hatua ya kwanza ni kuacha kwamba maskini waseme jinsi wanavyoishi, na nini wanahitaji… kuacha wazungumze wote! Na hivyo ndivyo inafanya kazi kanuni za ushirika. Hatuwezi kuacha nje watu hawa wasishirikishwe”. Na hekima yao, yaani  hekima ya watu ya makundi yaliyo manyenyekevu hayawezi kuwekwa pembeni (Wosia baada ya Sinodi Querida Amazonia [QA], 32; Wosia Laudato si’, 63). Kwa bahati mbaya ukosefu wa haki huu unaonekana mara nyingi mahali ambapo kuna masilahi makubwa ya kiuchumi au kijiografia, kwa mfano shughuli zingine za uchumbaji wa madini katika maeneo mengine ya sayari(taz QA, 9.14) amebainisha Papa.

Sauti za watu asilia, utamaduni wao na maono ya ulimwengu havizingatiwi. Ukosefu huo leo hii wa heshima ya kanuni ya kushirikishana imeenea kama virusi. Papa Francisko amependa kufikiria kwa mfano vipimo vikubwa vya msaada wa kifedha vinavyofanywa na Mataifa. Papa amesema hapa wanasikilizwa zaidi makampuni makubwa ya kifedha kuliko watu au wale ambao wanaendesha uchumi halisi. Ni kusikiliza zaidi makampuni ya kigeni kuliko harakati za kijamii. Kwa kuzungumza lugha rahisi , kusikiliza zaidi wenye nguvu kuliko wadhaifu,  hiyo siyo njia na siyo njia ya kibinadamu, siyo njia ambayo alitufundisha Yesu, na siyo msingi wa kufanya ushirika. Kwa njia hii hawaruhusu watu kuwa mstari wa mbele wa kujikomboa wenyewe. Au tufikirie hata kwa jinsi ya kutibu virusi. Wanasikiliza makampuni makubwa ya kutengeneza dawa kuliko wahudumu wa kiafya, walio mstari wa mbele katikamahospitali au katika makambi ya wakimbizi.  Hii siyo njia nzuri, amesisitiza Papa. Ili kutoka katika  mgogoro huo vema, kanuni ya ushirika lazima ifanye kazi, kuheshimu, na uwezo wa kuanzishwa mambo  kwa wote, hasa walio wa mwisho. Sehemu zote katika mwili ni za lazima, kama asemavyo Mtakatifu Paulo, kuwa sehemu ambayo inaweza kufikiriwa ni dhaifu zaidi na kutokuwa muhimu kiukweli ndiyo ya lazima (taz 1Kor 12,22). Katika mwanga wa picha hii tunaweza kusema kuwa misingi ya ushirika inaruhusu kila mmoja kuchukua nafasi yake ili kutumiza  na hatima ya jamii. Kuifanyia kazi ni hekima kwa ajili ya wakati mzuri zaidi na wa haki; na wakati ujao tunaujenga pamoja kwa kuongozwa na mambo makubwa zaidi, kwa kuongeza peo zetu na mawazo yetu

Katika katekesi iliyotangulia, Papa Francisko amesema kuwa  waliona jinsi mshikamano ni njia ya kuondokana na mgogoro, unatuunganisha na kuturuhusu kupata mapendekezo thabiti ya ulimwengu wenye afya.  Lakini zafari hizi za mshikamano zinahitaji ushirika. Kiukweli hakuna mshimamo bila ushiriki kijamii, bila mchango wa mihimili ya kati, yaani familia, vyama vya ushirika, biashara ndogo ndogo, na maonyesho ya asasi za kiraia. Ushiriki huo unasaidia kuzuia na kusahihisha baadhi ya mantiki hasi za utandawazi na matendo ya Mataifa kama inayotokea hata katika utunzaji wa watu waliopatwa na ugonjwa wa virusi. Mchango huu kutoka chini, lazima uhimizwe . Wakati wa karantini kulianzishwa ishara za hiari ya kuwapigia makofi madaktari na wauguzi kama ishara ya kuwatia moyo na matumaini. Kwa maana hiyo Papa Francisko amependa kuongezea makofu hayo kwa wajumbe wote wa kiungo cha  kijamii kwa mchango wao wenye thamani hata kama ni kidogo. “Tuwapigie makofu wazee, watoto, watu walemavu, wafanyakazi na wote wambao wanajikita katika huduma. Lakini tusibaki tu katika makofi: Tumaini ndilo muhimu na kwa maana hiyo tuwatie moyo ili kuota ndoto kubwa wakitafuta mawazo ya haki na upendo kijamii ambao inazaliwa ndani mwake tumaini.  Tusijaribu kujenga wakati uliopita, hasa ule uliokuwa mbaya na tayari umeugua. Tujenge wakati ujao mahali ambapo ukuu wa mahalia na wa ulimwengu vinatajirishana pamoja, mahali ambamo uzuri na utajiri wa makundi madogo yanaweza kuchanua na mahalia ambamo kuna jitihada  zaidi za kufanyika katika kuhudumia na kutoa zaidi aliye na kidogo.

23 September 2020, 13:58