Tafuta

Sala ya Malaika wa Bwana mjini Vatican Sala ya Malaika wa Bwana mjini Vatican  

Papa Francisko:Tusindikize kiroho maandalizi ya Kongamano la Ekaristi Kimataifa!

Kufuatia na tukio huko Budapest,Papa Francisko amekumbusha juu ya kuahirishwa kwa Kongamano la Ekaristi Kimataifa hadi tarehe 5-12 Septemba 202 nchini Hungary.Anaomba waamini kufuatilia kwa kuungana kiroho katika mchakato wa safari ya maandalizi.Anawatia moyo na kuunga mkono Chuo Kikuu Katoliki katika fursa ya kusheherekea siku yake nchini Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana Jumapili, tarehe 20 Septemba 2020 akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro ameanza kusema “Kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imepangwa kabla ya janga, siku chache zilizopitia ilikuwa lifanyike Kongamano la Ekaristi kimataifa huko Budapest. Kwa maana hiyo ninapenda kuwapa salamu zangu Wachungaji na waamini wa Hungary na wale wote waliokuwa wanasubiri kwa imani na furaha tukio la Kikanisa.  Akiendelea Papa amesema “ Kongamano limeahirishwa hadi  mwaka kesho kuanzia tarehe 5 hadi 12 Septemba huko huko Budapest. Tufuatilie kwa kuungana kiroho katika mchakato wa safari ya maandalizi na kupata kutoka katika Ekaristi kisima cha maisha na utume wa Kanisa”.

Siku ya Chuo Kukuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, Italia

Papa Francisko vile vile akikumbuka tukio moja la siku amesema" Leo nchini Italia ni Siku ya Chuo Kikuu cha Katoliki cha Moyo Mtakatifu. Ninawatia moyo na kuunga mkono taasisi hii muhimu ya kiutamaduni, inayoitwa kutoa mwendelezo na nguvu mpya kwa mpango ambao umeweza kufungua mlango wa siku zijazo kwa vizazi vingi vya vijana. Ni muhimu zaidi kwamba vizazi vipya vifundishwe kutunza utu na hadhi ya kibinadamu na nyumba yetu ya pamoja".  Kwa kuhitimisha amewasalimu waamini wote kutoka sehemu mbali mbali, familia makundi ya kiparokia, vyama na waamini binafsi. Amewatakia Dominika njema na wasisahau kusali kwa ajili yake.

Kardinali Bassetti:kuwekeza kwa vijana

Siku ya Chuo Kikuu katoliki ilikuwa ifanyike tarehe 26 Aprili mwaka huu ambapo iliharishwa kwa sababu ya janga. Wakati huo, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Italia Kardinali Guartiero Bassetto alikuwa ameandika ujumbe wake akisisitizia  umuhimu wa kuwekeza kwa vijana ili kujenga maisha ya baadaye. Kwa mujibu wa Kardinali aliandika kwamba Vijana, wanatafuta waalimu na maeneo ambayo yanajua jinsi gani ya kuwasaidia kukomaa kwa   mtazamo wa kibinadamu, kitaaluma, kitamaduni na kiroho ili wawe wahusika wakuu au kuwa mstari wa mbele wa siku zijazo.Na akiendelea  aliandika: “Matukio mapya yaliyoainishwa na akili bandia, teknolojia mpya za kidigitali, sayansi ya fahamu na kwa ujumla, mabadiliko ya uhusiano kati ya wanadamu na mashine ni ya kufurahisha lakini pia inahitaji uangalifu sana.

Kufuatia na hilo mahitaji ya maana na vigezo vya maadili yanaongezeka, hasa kati ya vijana. Kuna haja ya kuunga mkono utafiti huu. Aidha rais wa Baraza la Maaskofu Italia(CEI) alisema kuwa: “Kama ilivyo  leo hii na zaidi ya  zamani, jumuiya ya makanisa ya Italia inaona katika Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, taa na nguvu ya kuwasindikiza  vijana kukabiliana na changamoto kubwa za wakati wetu. Kanisa na Jamii ya Italia wanatarajia Chuo Kikuu Katoliki kujua jinsi gani ya kuandaa wanaume na wanawake wa siku zijazo. Na haya ni mahitaji ya haraka alihimitimisha Kardinali Bassetti.

20 September 2020, 14:58