Tafuta

2020.09.20 Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana 2020.09.20 Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana  

Papa Francisko:Ni bora Kanisa kutoka nje kuhudumia kuliko kujifungia binafsi!

Kwa kutujalia neema,Bwana anapanua na kukirimia zaidi ya yale tunayostahili.Kanisa linaitwa kutoka nje.Ikiwa Kanisa halitoki nje linaugua na ni magonjwa mengi tuliyo nayo ndani ya Kanisa.Ni tafakari ya Papa Francisko katika Injili ya Siku ya Jumapili ya 25 ya Mwaka kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican tarehe 20 Septemba 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Sura ya Injili ya Siku kutoka Mt, 20,1-16, inasimulia kuhusu wafanyakazi walioitwa kufanya kazi kwa siku katika shamba. Katika  maelezo hayo, Yesu anatuonesha mshangao kwa utendaji wake Mungu, akiwakilisha tabia mbili za Bwana. Kwanza  kuitwa na tuzo. Awali ya yote Kuitwa. Kwa mara tano Bwana wa shamba alitoka afajiri kwenda kwenye uwanja na kuwatafuta wafanye kazi kwa ajili yake. Alitoka mnamo saa kumi na mbili, saa tatu, saa sita, saa kenda na saa kumi na moja jioni. Bwana huyo anawakilisha Mungu ambaye anaita wote na daima anaita. Mungu ndivyo anatenda   hata leo hii  na anaendelea kuita kila mmoja, kila saa, ili kuwaalika kufanya kazi katika ufalme wake. Huo ndiyo mtindo wa Mungu, ambaye kwa mara nyingine  tena tunaalikwa kutambua hili na kuiga. Yeye hajafungwa katika ulimwengu wake binafsi, bali ‘anatoka’ mara nyingi kutafuta watu, kwa sababu anataka hasiwepo hata mmoja wa kubaguliwa katika upendo wake. Ndivyo Papa Francisko ameanza tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Kiwanja cha Mtakatifu Petro Jumapili tarehe 20 Septemba 2020, ikiwa ni Dominika ya 25 ya Mwaka.

Jumuiya zetu zitoke nje ya vizingiti kutangaza neno la Yesu

Hata katika jumuiya zetu Papa Francisko anahimiza  kuwa zinaalikwa kutoka nje ya vizingiti vya kila aina ambavyo vinawezekana kuwapo ili kuwapatia Neno wote neno la wokovu ambalo Yesu alikuja kutuletea. Hii inahitaji kufungua maono zaidi ya maisha ambayo yanatoa matumaini kwa wale ambao wanaishi pembezoni mwa maisha na hawajafanya uzoefu bado au wamepoteza nguvu na mwanga wa kukutana na Kristo. “Kanisa linaitwa kutoka nje, ikiwa Kanisa halitoki nje linaugua na ni magonjwa mengi tuliyo nayo ndani ya Kanisa. Lakini ni kwa nini magonjwa haya ndani Kanisa? Ni kwa sababu halijatoka nje. Ni kweli kwamba unapotoka nje kuna hatari ya kupata ajali. Lakini ni vizuri Kanisa ambalo limepata ajali kwa sababu limetoka nje kutangaza Injili, kuliko Kanisa ambalo limefungwa. Mungu anatoka nje daima, kwa sababu ni Baba na kwa sababu anapenda. Kanisa lazima lifanye hivyo hivyo yaani litoke nje”, Amesititiza Papa Francisko.

Malipo ya Mungu ni Ufalme wa Mungu na wema wake

Tabia ya pili ambayo Papa Francisko amebainisha kuhusu Bwana huyo na ambayo inamwakilisha Mungu amesema ni namna ya kutuza wafanyakazi. Je anawalipa namna gani Mungu? Yeye bwana  huyo naahidiana nao kuwapa dinari moja kwa wafanyazi wa kwanza aliowaajiri. Na waliofuata baadaye akawambia “kile kilicho cha haki nitawapatia (Mt 20,4). Mwisho wa siku, Bwana wa shamba anawaamuru wapewe wote mshahara sawa yaani dinari moja. Wale waliofanya kazi kuanzia asubuhi wakakasirika na kumlalamikia bwana, lakini yeye alitaka kutoa kiasi cha   juu kwa wote hata wale waliofika wakiwa wa mwisho(Mt 20,8.15), Mungu daima anatoa  kilicho cha juu sana. Yeye abakizi nusu. Analipa yote. Papa Francisko amebainisha kuwa hapa kuna utambuzi kwamba Yesu hakuwa anaelezea juu ya kazi na wala mshahara wa haki,   hata hivyo nayo ni shida nyingine, badala yake anazungumzia juu ya Ufalme wa Mungu na wema wa Baba wa mbinguni ambaye anaendelea kutoka nje mara kwa mara ili kuwaalika na kuwalipa kwa kiasi cha juu wote. Kwa hakika tabia yake ndivyo ilivyo maana hatazami muda na matokea, anatazama uwezekano na ukarimu kwa namna tunavyojikita katika huduma yake. Kutenda kwake kuna haki zaidi, maana ni kwenda zaidi ya haki na kujionesha katika neema. Kila kitu ni neema. Wokovu wetu ni neema na Utakatifu wetu ni neema.

Mungu anatukirimia zaidi ya yale tunayostahili

Kwa kutujalia neema, Bwana anapanua na kutukirimia zaidi ya yale tunayostahili. Kwa maana hiyo anayefikiria kwa mantiki ya kibinadamu, yaani kufikiria kustahili kwa sababu ya akili yake binafsi, atajikuta akiwa wa mwisho.  Papa Francisko ametoa mfano wa malalamiko ambayo yanaweza kutokea “ lakini mimi nimefanya kazi sana, nimefanya Kanisani sana na kusaidia sana, lakini wananilipa sawa na aliyefika akiwa/wakiwa wa mwisho. Tukumbuke kuwa aliyekuwa wa kwanza kuwa mtakatifu katika Kanisa “ ni jambazi. Aliiweza kupata mbingu katika dakika za mwisho wa maisha yake: Hiyo ni neema na ndivyo afanyavyo Mungu. Hata kwa wote. Kinyume chake anayefikiria kustahili anashindwa, lakini  yule ambaye anajikabidhi kwa unyenyekevu katika huruma ya Baba badala ya kuwa wa mwisho  atajikuta akiwa wa kwanza kama jambazi( Mt 20,16). Papa Francisko ameongeza. Bikira Mtakatifu atusaidia kuhisi kila siku furaha na mshangao wa kuitwa na Mungu kufanya kazi kwa ajili yake, katika shamba ambalo ni ulimwengu na katika mizabu ambayo ni Kanisa. Na kuwa kama  kama tunu moja ya upendo wake, na wa urafiki na Yesu.

20 September 2020, 14:49