Tafuta

Ni muhimu kuwa na ukaribu kwa watu wa Mungu katika janga hili la covid-19. Ni muhimu kuwa na ukaribu kwa watu wa Mungu katika janga hili la covid-19. 

Papa Francisko kwa maaskofu Ulaya:janga la Covid lishindwe kwa njia ya ukaribu!

Papa Francisko ametuma ujumbe wake wakati katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu waShirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya ambapo mwaka huu umefanyika kupitia mtandaoni tarehe 25 -26 Septemba.Papa ameandika kuwa lazima kung’amua nja za kuwa na ubaba na kuzingatia ukaribu wa watu wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kanisa la Ulaya baada ya Janga la corona, matarajio ya kuunda kwa upya na kwa ajili ya jumuiya ndizo mada zilizo changuliwa na Maaskofu kwa ajili ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Ulaya CCEE. Mkutano huo ulikuwa unatarajiwa kufanyika huko Praga kuanzia tarehe 25-27 Septemba 2020 na ambapo kwa sasa umefanyika kwa mtindo wa mtandao kwa  siku mbili  tu kuanzia tarehe 25 na 26 Septemba kutokana na kuzidi kuongezeka kwa maambukizi ya covid-19 katika Jamhuri ya Ceca.

Katika fursa hiyo, Papa Francisko amewafikishia ujumbe wake kwa washiriki wa mkutano huo wa kila mwaka ukaribu wake kwa njia ya ujumbe aliomwelekeza Rais wa Ccee, Kardinali Angelo Bagnasco. Katika meneno ya Papa, anawapongeza kwa uchaguzi wa mada ya maaskofu na kutoa mwaliko wa kila mtu na kuendelea kwa ujasiri njia ya kutoa huduma ya kichungaji. Hata hivyo njia ambazo Papa anaelezea zinajikita katika uzoefu wa Covid.

Papa amendika: “Kifo cha wazee wengi, janga la familia zilizoshikwa na mshtuko wa ghafla na maumivu makubwa na ya kutishia, janga la watoto na vijana walifungwa nyumba, liturujia za ibada za kidini na michakato ya kozi za malezi ya Kikristo kusimamishwa, lakini hazikuzuia mapadre na watawa kadhaa kugundua njia za ujasiri za kutoa huduma ya kichungaji, wakishuhudia ukaribu wa ubaba kwa watu wa Mungu. Mbele ya uchungu mkubwa hivi na ule ambao Papa ameubanisha kama umaskini mpya ambapo ni lazima kuwa na ubunifu huu wa upendo uendelee kujionesha daima na kuwa makini na wakarimu wa ukaribu kwa walio wadhaifu zaidi.

Kufuatia na umuhimu kwa ajili ya jumuiya za kikristo ili zisipoteza kile ambacho waliikiishi lakini kusoma ishara hizi za nyakati kiroho, kwa namna ya ya kufanya mang’amuzi ya matarajio ya wakati ujao. Picha ambayo Papa Francisko anaitumie ni ile ya kiinjili ya “ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale (Mt 13,52). Na kwa kuhitimisha Papa Francisko amesema: “Ninawahakikishia sala zangu kwamba, kupitia maombezi ya Bikira Maria na Watakatifu wasimamaizi  Benedikto, Cyril na Methodius,Wachungaji wa Kanisa ambalo ni Ulaya wanaweza kuwawakikishia waamini uhakika wote wa imani, kulingana na chochote kinachoweza kutokea  na ambacho hakuna kitu kinachoweza kututenganisha na upendo wa Kristo”.

26 September 2020, 16:02