Tafuta

Vatican News
HATARI YA WAHAMIAJI KUKATISHA BAHARI YA MEDITERRANEA HATARI YA WAHAMIAJI KUKATISHA BAHARI YA MEDITERRANEA 

Papa Francisko:haikubariki watu wafe baharini wakitafuta tumaini

Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa Mpango uitwao“Snapshots from the Borders,“sauti na uzoefu kutoka Mipakani”ambao ni mpango unaofadhiliwa pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya kwa ajili ya wakimbizi.Papa amesema Changamoto ni nyingi na zinazokumba wote.Hakuna mtu anayeweza kubaki bila kujali majanga ya wanadamu ambayo yanaendelea kutokea katika maeneo tofauti ya ulimwengu.

Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amekutana na wawakilishi wa Mpango wa “Snapshots from the Borders yaani “sauti na uzoefu kutoka Mipakani” na kumshukuru Meya wa Mji wa Lapendusa na Linosa, Bwana Salvatore Martello kwa hotuba yake kwa niaba ya wote na kuwashukuru kwa zawadi ya msalaba na ambayo amesema ni wenye maana! Mpango wao ni wa kudumu ambao unapendekeza kuhamasisha uelewa wa kina wa wahamiaji na kuwezesha jamii ya Ulaya kutoa jibu zaidi la kibinadamu na ambao unakumbwa na changamoto za wahamiaji. Mtandao huu unajumuisha mashirika mbalimbali na asasi za kiraia na ambao wanajitahidi kwa uchanya kuchangia maendeleo ya sera za kisiasa ili uhamiaji uendane na hatima hiyo. Kwa njia hiyo katika hotuba hiyo mambo muhimu hasa umuhimu wa makutano, mshikamano na sera za kisiasa zenye kuwa na mapokezi na ufungamanishwaji barani Ulaya ndivyo amesisitizia zaidi.

Papa Francisko amebainisha juu ya suala la uhamiaji wa sasa lilivyo na ugumu na mara nyingi linawakilisha majanga. Utegemezi wa ulimwengu ambao huamua wingi wa uhamiaji unahitaji kusomwa na kuueleweka vizuri. Changamoto ni nyingi na zinaguswa wote. Hakuna mtu ambaye anayeweza kubaki na sintofahamu za kutojali majanga ya wanadamu ambayo yanaendelea kupotea katika maeneo tofauti ya ulimwengu. Kati ya hizi mara nyingi tunaalikwa kuona changamoto na wale ambao Mediterranean imekuwa kama ukumbi wa tamasha, katika bahari ya mipakani, lakini pia ni sehemu ya makutano ya utamaduni.

Papa Francisko amekumbuka mkutano wa mwezi Febrauri ambao anasema ulikuwa chanya na maaskofu wa kimediterranea huko Bari, ambapo alikumbua njinsi wale ambao wanaishi karibu na mediterranea wanapata ugumu, kwa maana kuna wale ambao wanakimbia vita au wanaacha nchi zao katika kusaka maisha yenye hadhi ya binadamu (…). “Tunao utambuzi kuwa katika mantiki nyingi za kijamii kumeenea sintofahamu hadi kufikia kubagua (…). Jumuiya ya Kimataifa imejikita kuingilia kati suala la wanajeshi na wakati inatakiwa kujenga taasisi ambazo zihakikishe usawa wa fursa na mahali ambamo wazalendo wanao uwezekano wa kuchukua wajibu wa wema wa pamoja”. Papa Francisko amesema hatukubali kamwe kwamba yule anayetafuta tumaini kupitia baharini anakufa bila kupatiwa msaada (…). Ni wazi mapokezi na hadhi ya ufungamanishwaji ni hatua msingi ya mchakato ambao siyo rahisi Papa amebainisha lakini amesema paamoja na hayo ni lazima kuweza kukabiliana tabia za ujenzi wa kuta. ( Hotuba 32, feb 2020)

Mbele ya changamoti ni wazi kwamba mshikamano wa dhati ni muhimu na uwajibikaji shirikishi kwa ngazi iwe kitaifa na kimataifa. Janga la sasa limeonesha utegeemezi wetu. Sisi sote tumeuganishwa mmoja na mwingine, iwe katika ubaya na katika wema (Katekesi 2 Septemba 2020). Ni lazima kutenda kwa pamoja na siyo peke yetu. Papa Francisko amesena ni msingi kabisa wa kubadili namna ya kuishi na kusimulia uhamiaji. Hii ina maana ya kuweka katikati mtu, sura na historia.  Kwa njia hiyo mpango wao unapata maana yake kama vile wao wanavyohamasisha na wanatafuta namna ya kuendesha shughuli hiyo kwa njia mbalimbali ambayo inaongozwa na utamaduni wa makutano ambayo yanaunda safari kuelekea ubinadamu mpya. “Ninaposema ubinadamu mpya simaanishi tu kama falsafa ya maisha bali ni kama tasaufi moja na mtindo mmoja wa kimwenendo”, Papa Fracisko amesisitiza.

Wakazi wa miji na wa maeneo ya mipakani, jamii, jamuiya, makanisa wanaalikwa kuwa mstari wa mbele katika kipindi hiki cha mabadiliko, na shukrani kwa sababu ya fursa zinazoendelea za kukutana na historia hiyo. Mipaka, ambayo imekuwa ikijulikana daima kama vizuizi vya kugawanya, badala yake inaweza kuwa madirisha, nafasi za maarifa ya pamoja, ya utajiri wa pande zote, ya muungano katika utofauti; mahali ambapo mitindo mipya inajaribiwa ili kushinda matatizo ambayo hujitokeza kwa wageni wanapofika kwa jamii za wenyeji. Kwa kuhitimisha anawatia mouo wa kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya utamaduni wa makutano na mshikamano. Bwana awabariki jitihada zao kwa maana hiyo na Bikira Maria awalinde wao na watu wote ambao wanafanya kazi nao.

Ikumbukwe kuwa  Mpango wa “Snapshots from the Borders yaani “sauti na uzoefu kutoka  Mipakani” ni mpango  wa miaka mitatu unaofadhiliwa kwa pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (DEAREuropeAid budget line), inayosimamiwa na washirika 35, mamlaka za mipaka mahalia na mashirika ya kijamii. Chombo hiki “Sauti na uzoefu kutoka Mipakani” kinakusudia kukuza uelewa muhimu wa watunga sera za Ulaya, kitaifa na sehemu mahalia na maoni ya umma juu ya utegemezi wa ulimwengu ambao huamua uhamiaji kuelekea mipaka ya Ulaya, kwa matarajio ya kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs, kwa namna ya pekee, malengo ya kifungu 1, 5, 10, 11 na 16. Hasa, katika mpango huo unakusudia kuimarisha mtandao mpya wenye usawa na kazi kati ya miji ambayo inashughulikia moja kwa moja mtiririko wa wanaohama katika mipaka ya Ulaya (EU), kama njia ya kukuza mshikamano mzuri wa sera kwa ngazi zote (Ulaya, kitaifa, wilaya).

10 September 2020, 14:22