Tafuta

Vatican News
2020.09.06 Angelus 2020.09.06 Angelus  (Vatican Media)

Papa Francisko atoa salamu kwa wanariadha wanawake wenye ulemavu wa viungo!

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana,Papa Francisko Jumapili tarehe 6 Septemba 2020 ametoa salamu kwa wanariadha wanawake walio na ugonjwa wa viungo mbalimbali (sclerosis) na mahujaji wote kwa ujumla waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro kushiriki naye sala hiyo ya Mama Maria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Dominika tarehe 6 Septemba 2020 Papa Francisko kama kawaida yake, mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, katika salamu zake amewasalimu kwa namna ya pekee wanariadha wanawake walio na ugonjwa wa viungo mbali mbali (sclerosis) ambao wamefanya hija kupitia  njia ya Francigena kutoka Siena hadi  Roma, na vijana kutoka Mtakatifu Stefano Lodigiano, ambao wamekuja kwa baiskeli kama anzisho la hisani. Papa amesisitiza kuwa makundi yote mawili ni ya kijasiri na kuwashauri waendelee mbele kwa furaha na imani.

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana

Papa Francisko katika salam hizo lakini hakuwasahau mahujaji wote kuanzia waroma na wengine kutoka nchi mbali mbali, familia, makundi ya kiparokia na vyama mbali mbali. Aidha kwa namna ya pekee amewasalimu waseminari kutoka Chuo cha kipapa cha Amerika Kaskazini Roma, vijana wa Seminari kuu ya Lubiana nchini Slovenia na makundi mengine mengi ya vijana ambapo  amewashauri wote wamkubatie sana Yesu, jiwe hai la pembeni na mchungaji mwema.

Picha wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Picha wakati wa sala ya Malaika wa Bwana

Salam pia zimewaendeea waamini wengine kama vile wapoland, watu kutoka Albania, Ufaransa na Mexico waliokuwapo katika uwanja huo. Kwa wao pia amesema ni wenye ujasiri kwa Mama Maria mkingiwa dhambi ya asili na hivyo waendelee mbele! Amehitimisha kwa kuwatakia Dominika njema, lakini wasisahau kusali kwa ajili yake. 

06 September 2020, 15:39