Tafuta

2020.09.21 Papa Francisko na watoto wa wa kituo cha Sonnenschein (Austria) 2020.09.21 Papa Francisko na watoto wa wa kituo cha Sonnenschein (Austria) 

Papa Francisko akutana na wahusika na watoto wa kituo Sonnenschein cha Austria!

Francesco katika kukutana mjini Vatican na wahusika wa wageni wa kituo cha Sonnenschein”,‘mwangaza wa jua’kinachojikita kusaidia watoto na vijana wenye matatizo ya usonji amesema nyumba yao utafikiri ni bustani ya ajabu iliyochanua mwangaza wa jua na mau ya nyumba hiyo ni wao wenyewe.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Papa Francisko tarehe 21 Septemba 2020 amekutana na wazazi na watoto wadogo wa kituo cha Usonji(autism) cha “Sonnenschein” nchini Austria ambapo amewashukuru ujio wao mjini Vatican. Ameonesha furaha kuwaona wote uso kwa uso wakiwa na furaha ya kukaa kidogo na yeye. Papa Francisko akianza kuelezea wasifu wa mahali wanapoishi amesema Nyumba yao inaitwa ‘Sonnenschein’ maana yake “mwangaza wa jua”. Anatambua ni kwa nini wahusika walichagua jina hilo. Kwa sababu nyumba yao ni ya maajabu kwa kwani ni kama bustani yao imechanua maua yanayoangazwa na jua, na maua ya nyumba hiyo ni wao wenyewe! Mungu aliumba ulimwengu ukiwa na maua mengi ya rangi. Kila ua lina uzuri wake na ambao ni wa kipekee, amefafanua Papa. Kutokana na mkutadha huo, Papa anasisitiza kwamba wote wanasema asante Mungu! Asante kwa zawadi ya maisha, kwa ajili ya viumbe vyote! Asante kwa ajili ya Mama na Baba! Asante kwa ajili ya familia zetu! Na asante kwa ajili ya marafiki wa Kituo cha Sonnenschein”!

Kusema asante kwa Mungu ni sala nzuri, Papa Francisko amefafanua. Mungu anapenda mtindo huo wa kusali. Ili kufanya hivyo hata hivyo wanaweza kuongeza hata ombi dogo. Kwa mfano, ameshauri “Yesu mwema unaweza kumsaidia baba na mama katika kazi zao? Mnaweza kumwambia ampatie nguvu kidogo bibi ambaye anaumwa? Wanaweza kuwafikiria watoto wote ulimwenguni ambao hawana chakula? Au Yesu ninakuomba umsaidiei Papa aweze kuongoza vizuri Kanisa. Ikiwa ninyi mtaomba kwa imani, Bwan kwa hakika atawasikiliza.

Hatimaye Papa ameonesha utambuzi kwa wazazi wao, wahudumu wao wanaowasindikiza, mhudumu Rais na wawakilishi wote waliokuwapo. Amewashukuru kuanzisha shughuli hiyo na jitihada kwa ajili ya kusaidia hao waliokabidhiwa. Yote ambayo walifanya kwa ajili ya walio wadogo wamefanya kwa ajili ya Yesu! Papa amesisitiza. Anawakumbuka katika sala.Yesu awabariki daima na Mama Maria awalinde. “Und bitte vergesst nicht, für mich zu beten. Diese Arbeit ist nicht einfach. Betet für mich bitte. Dankeschön!

21 September 2020, 14:31